Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 31, 2017

DC TUNDURU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI MRUSHA NA SEMENI`


```Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera ameanza ziara ya kufuatilia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi ya shule za msingi, katika ziara hio Mhe. Homera aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Bw. Chiza Marando.```

```Ziara hio ilianzia shule ya Msingi Semeni iliyopo kata ya Mtina ambapo Mkuu wa wilaya alikutana na kamati ya ujenzi wa shule hio, Mwenyekiti wa kamati hio Bw. Hamidu Saidi alimueleza Mkuu wa wilaya kuwa wamepokea shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja na wapo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi.```

```"Mkuu wa wilaya mbele yako ni kamati ya ujenzi ya shule ya msingi semeni na tunakiri kupokea shilingi milioni kumi ambayo tunatarajia kujenga darasa moja".```

```DC Homera aliagiza ujenzi uanze mara moja kwa kuwa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ilitoa fedha toka mwaka jana lakini cha kushangaza hadi sasa ujenzi haujaanza, alieleza kuna tatizo kwenye uongozi wa kijiji na alitoa agizo ujenzi uanze ndani ya siku sita.```

 ```"Naagiza ndani ya siku sita mchanga uwe umefika ili ujenzi uanze mara moja, na Mwenyekiti wa kijiji hiki cha semeni Bw. Yusuf Kanduru Mpelembe namuagiza aje ofisini kwangu kwa kuwa nimepata taarifa zake za kuendekeza migogoro kijijini na shilingi milioni kumi mliopewa na Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inatosha kujenga vyumba viwili vya  madarasa na ofisi moja kwa kuwa kijiji kina benki tofali hii itasaidia kupunguza garama".```

```Aidha akiwa shule ya msingi Mrusha iliyopo kata ya Mchesi Tarafa ya Lukumbule alikagua ukarabati wa sakafu ya madarasa mawili na kuagiza darasa lililobomoka ukuta lianze kujengwa upya.```

```"Nakuagiza Mwalimu Mkuu ndani ya wiki mbili sakafu ya vyumba viwili vya madarasa ukarabati ukamilike na hela itakayo bakia uanze ujenzi wa msingi wa darasa jipya".```

```Mkuu wa wilaya alimalizia kwa kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mrusha kwa kuwapa motisha na kuwa sisitizia umuhimu wa elimu ili waweze kufanikiwa hapo baadae na aliwachangia shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kununua sukari ya uji ambayo wanafunzi hao hunywa saa nne muda wa mapumziko.```

```Kwa upande wake Dc Homera alifurahishwa na hatua ya shule ya msingi Mrusha kuvuka lengo la agizo lake la kila shule kupanda hekari tano za miche ya mikorosho, shule hio imepanda hekari nane.```

FIFA YABARIKI KUONGEZA TIMU HADI 48 KATIKA KOMBE LA DUNIA 2026


Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.
Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo na ila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.Mapendekezo hayo yapo hivi

Afrika - 9 kutoka timu za awali 5
Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali

Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi


Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.

LIJUAKALI:NILIPATA MATESO MAKALI SANA GEREZANI UKONGA

Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero
PETER Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, (Chadema) amesema akiwa mfugwa kwa yake kwa siku 79 katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, aliteswa na kunyimwa haki zake, anaandika Pendo Omary.
Lijualikali ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online leo mchana baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”
“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.
“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.
“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.
Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”
Ameeleza kuwa wakati akifanyiwa vitendo vya kikatili na baadhi askari wa jeshi hilo, asilimia kubwa ya wafugwa walimpokea vizuri na walimpa ushirikiano.
Amesema: “Wafugwa ni watu wazuri, wamekuwa ni walimu wangu, wazazi wangu, washauri wangu na wasiri wangu. Walinipa mashuka.
“Walinipikia chakula pale walipoona nashidwa kula chakula kilichopikwa kwa ajili ya wafugwa. Ambacho ni dagaa waliojaa mchanga na dona tena lililosagwa na mabuzi ya mahindi. Walinisaidia kazi nzito. Ingawa wapo baadhi ambao tulikuwa hautuelewani. Nadhani ni sababu za kisiasa,” ameeleza Lijualikali.
Lijualikali amesema Tanzania bado ina safari ndevu kufikia nchi ambayo inaamini katika uhuru, haki na demokrasia kwa maana halisi. Hivyo amewataka Watanzania kuacha kunyamazia ukiukwaji wa haki dhidi ya raia.
 
CREDITY:mwanahalisi

MAHAKAMA YA KENYA YAWAKATAA MADAKTARI WA TANZANIA

Image result for MADAKTARI


Baada ya madaktari wa Kenya kufanya mgomo kuanzia December 2016 kwa madai ya kutaka nyongeza ya mshahara, March 18 2017 serikali ya Tanzania ilikubali kuwapeleka madaktari 500 kukabiliana na uhaba wa madaktari nchini humo, uamuzi ambao ulipingwa na watu mbalimbali hasa wananchi wa Kenya.
Leo March 31 Mahakama nchini Kenya imekubaliana na pingamizi la Chama cha Madaktari nchini humo juu ya kuajiri madaktari 400 kutoka Tanzania kwani ndani ya nchi yao kuna zaidi ya madaktari 1,400 ambao hawajaajiriwa.
Mahakama imechukulia suala hili kama jambo la haraka na kuipa Serikali muda wa siku 21 kufanya maamuzi. Mpaka sasa madaktari zaidi ya 400 kutoka Tanzania waliomba nafasi Kenya.


NI YANGA NA AZAM KESHO UWANJA WA TAIFA


yanga-vs-azam-fc_1q8iwsed2cfgz1i0e4rzd6zky8
Baada ya kusimama kwa muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.
Michezo ya kesho Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam – mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi, zitafanyika saa 10.00 jioni.
Ligi hiyo itaendelea tena kwa siku ya jumapili ambapo wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa ugenini mkoani Kagera kumenyeana na Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.
Mechi nyingine Mwadui itakuwa nyumbani ikiwakaribisha maafande wa JKT RUVU ya mkoani Pwani iliyo chini ya mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden kwa wakati huu baada ya kocha Bakari Shime kujiunga na timu ya vijana ya Serengeti Boys.

ETHIOPIA KUIPA TANZANIA NISHATI YA UMEME


A 4
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Tanzania inategemea kupata Megawati 400 za umeme kutoka Ethiopia ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyofikiwa baada ya ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Haile Mariam Desalegn. 
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya makubaliano na mikataba ambayo nchi za Tanzania na Ethiopia wametiliana saini leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Tukitaka kujenga uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na umeme wa kutosha,wenzetu Ethiopia wametuonyesha njia na mimi nimemuomba Mhe.Waziri atusaidie wataalamu kutoka nchini kwake ili  waje  tuwaonyeshe maeneo mbalimbali watusaidie katika kupata umeme wa uhakika kwa kujenga mabwawa ya umeme ambayo yamesaidia sana katika kupatikana kwa umeme wa kutosha nchini kwao.”Aliongeza Rais Magufuli.
Aidha amesema kuwa kupatikana kwa umeme huo kutasaidia kuleta changamoto kwa shirika la umeme nchini katika kuwapatia wananchi bei ya chini na hivyo kuleta ushindani katika upatikanaji wa umeme nchini.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Haile Mariam Desalegn amesema kuwa wana mengi ya kujifunza kutoka Tanzania kwani nchi hizi mbili zina historia inayofanana na kuongeza kuwa hakuna haja ya wao kwenda nje ya Afrika kupata uzoefu katika masuala mbalimbali.
Ameongeza kuwa lengo kuu la kuja nchini ni kwa sababu anahamini nchi hizi mbili zinaweza kuunganisha nguvu zake na kuwa nguzo kuu katika maendeleo katika eneo la ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
“Tanzania na Ethiopia ni nchi ambazo zina ushirikiano mzuri sana,sisi sio washindani bali tunasaidiana katika masuala mbalimbali kwani tumekuwa katika hatua mbalimbali za kuwaondoa wananchi wetu katika umaskini katika hatua zinazofanana,na huu ni wakati muafaka katika kuimarisha ushirikiano wetu kwa faida ya watu wetu kwa ujumla”Alisisitiza Mhe.Desalegn.
Aidha amesema  kuwa  mabadiliko  ya  kilimo  katika  nchi  zetu ndio  msingi  wa  maendeleo  pamoja  na  utumiaji  wa  teknolojia  bora utasaidia katika maendeleo ya viwanda vidogo vidogo.
Viongozi hawa wamekubaliana kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu juu ya namna sekta mbalimbali zitakavyoleta manufaa ya kiuchumi zikiwemo huduma za benki, madini na gesi, elimu na  mawasiliano.
Ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Haile Mariam Dessalegn imekuwa ya manufaa makubwa kwa Tanzania na amesisitiza kuwa wakati umefika wa kukuza biashara kati ya nchi hizi ambazo kwa sasa thamani ya biashara kati yake ni Dola za Marekani milioni 2.24 tu.

TUHUMA ZA SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUKUZA WAKENYA NCHINI


A
Kumekuwepo taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa, Serikali ya Tanzania inafanya operesheni maalum inayolenga kuwaondoa Raia wa Kenya wanaoishi nchini bila kuwa na Vibali halali huko Wilayani Longido, Mkoa wa Arusha, huku wakimhusisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika utekelezaji wa ‘zoezi’ hilo.
Taarifa hizi zimezua tafrani na kutishia hali ya usalama iliyopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu Taarifa hizo zinazoendelea kuenezwa kuwa:-
  1. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijafanya operesheni yoyote inayolenga kuwakamata na kuwaondoa nchini raia wa Kenya au Taifa lolote lile wanaoishi katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha kama inavyoenezewa kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao mbalimbali ya kijamii.
  1. Shughuli za udhibiti wa raia wa kigeni wanaokiuka Sheria za Uhamiaji nchini hazifanywi kwa kulenga Taifa lolote lile, bali hufanywa kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi. Wahusika wanaokiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za uhamiaji hukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa makosa yao binafsi na sio kwa msingi wa utaifa wao.
  1. Kukamatwa kwa raia wa kigeni ambao walibainika kuwa ni raia wa Kenya ni sehemu ya shughuli za kawaida za Idara ya Uhamiaji kama Chombo cha Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha kwamba raia wa kigeni wanatambuliwa na kuishi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
  2. Suala la kukamatwa kwa raia hao wa Kenya ambao walibainika kukiuka Sheria ya Uhamiaji nchini halihusiani kwa njia yoyote ile na Serikali ya Tanzania kulenga kuwakamata raia wa nchi yoyote na wala si agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoripotiwa, bali ni utaratibu wa kawaida ambao unafanywa na nchi yoyote katika kuhakikisha kwamba ukaazi wa wageni unazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi husika. Kwa mfano, katika mwezi Februari 2017, Idara ya Uhamiaji imewakamata wageni 396 kutoka mataifa mbalimbali kwa makosa ya kiuhamiaji na kuwachukulia hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria.
  1. Tanzania na Kenya tunao uhusiano mzuri sana ambao ni wa kihistoria na nchi hii ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa uhusiano huo, wapo watanzania wengi wanaokwenda nchini Kenya kwa sababu mbalimbali kama vile matembezi, biashara, masomo nk. Pia wapo raia wengi wa Kenya wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa sababu kama hizo hizo na hatuna tatizo nao, alimradi hawavunji Sheria za nchi yetu.
  1. Mwisho, tunatoa wito kwa Wageni wote wanaoishi hapa nchini kwa shughuli mbalimbali kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za uhamiaji nchini. Wapo baadhi ya wageni wanaoingia nchini kihalali, lakini wanaendelea kuishi nchini hata baada ya muda waliopewa kuishi nchini kumalizika. Aidha, wapo baadhi ya wageni wengine wanaoingia nchini kinyume cha sheria na kuendelea kuishi nchini kinyume cha Sheria. Wale wanaobainika kukiuka Sheria, Kanuni na taratibu za uhamiaji nchini watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria bila kujali utaifa wao.
  1. Taarifa zinazoenezwa kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya kijamii kwamba Tanzania inawalenga raia wa Kenya, kuwakamata na kuwaondoa nchini si sahihi na zipuuzwe kwani zinalenga kuchafua na kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi zetu mbili na wananchi wake, pamoja na kudhoofisha shughuli za udhibiti wa wahamiaji haramu nchini.
  1. Tunafahamu kuwa Tanzania haiwezi kuishi kama kisiwa. Hivyo, tutaendeleza na kuimarisha ushirikiano na Mataifa mengine pamoja na kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wageni kuja na kuishi nchini kwa shughuli mbalimbali, zikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, matembezi na nyinginezo.
Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
BARABARA YA LOLIONDO, KURASINI,
 S.L.P 512, DAR ES SALAAM.
31 MACHI, 2017.
 


 
 

MBUNGE COSATO CHUMI APONGEZA JAPANI KWA KUSAIDIA HOSPITALI YA WILAYA YA MUFINDI


MBUNGE wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi amepongeza ubalozi wa Japan nchini kwa kutolea kusaidia jimbo lake kwa kusaini mkataba shilingi milioni 230 kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wenye lengo la kuwezesha ujenzi wa jengo la Upasuaji katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

Akizungumza baada ya kusainiwa mikataba huo Mbunge Chumi jana mbali ya kumshukuru balozi Masaharu Yoshida na Serikali ya Japan kwa kuendelea kufadhili miradi hasa inayolenga kuwafikia watu wa chini bado alisema msaada huo ni mkubwa na umelenga kuwasaidia wananchi wa jimbo lake na wilaya nzima ya Mufindi. Chumi alisepongeza waziri wa wizara ya Fedha Dr Philip Mpango kwa kuridhia kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka wa Fedha wa Japan March 31.

Alisema misaada mikubwa imekuwa ikitolewa kupitia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yaani bilateral cooperation, bado Japan imeendelea kutoa na kufadhili miradi inayotekelezwa katika ngazi za chini kabisa, hili ni jambo jema na tunaopokea Fedha hizi tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa' Alisema Chumi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Mafinga ,Saada Mwaruka alisema kuwa msaada huo ni ukombozi kwa watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba Hospital hiyo inahudumia Wilaya ya Mufindi na hata Wilaya za jirani kama Mbalari na Iringa Vijijini. Wakati Balozi wa Japan hapa nchini Yoshida alisema kwamba msaada huo ni matokeo ya ombi la mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi aliloliwasilisha Ubalozini mwaka uliopita.

Balozi Yoshida alimpongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano alioutoa hasa katika kufuatilia katika ngazi mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata ridhaa ya kusaini mkataba wa msaada huo. Pamoja na msaada huo, Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake hapa nchini, umetoa msaada kwa Halmashauri za Bukoba, Temeke na Chuo cha Ufundi Yombo.

Halmashauri ya Bukoba imepewa msaada wa milioni 238 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwenye shule za Msingi za Nyakato na Kashozi ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi. Alisema kuwa kwa upande wa Temeke wamepokea msaada wa usd 137,837 (Tsh 274m) kwa ajili ya kuboresha Jengo la huduma ya dharura kwenye Hospital ya Rufaa ya Temeke na Chuo Ufundi Yombo wamepokea msaada wa usd 64,499(Tsh 130m) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye ulemavu.

Alisema kuwa jumla ya usd 408,496 (Tsh 900m) zimetolewa katika misaada hiyo inayolenga kuwasaidia wananchi ngazi za chini yaani Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects Hospitali ya wilaya ya Mufindi ni moja ya Hospitali zinazotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo na wananchi mbali mbali wa nchi nzima na nchi jirani kutokana na kuwepo kando kando
ya barabara kuu ya ya inayoelekea nchi za kusini mwa Tanzania .

CHIKU ABWAO ASHINDA TUZO YA MALKIA WAGUVU TANZANIA

MBUNGE mstaafu wa viti maalum mkoa wa Iringa Kupitia Chadema chiku Abwao ashinda tuzo ya malkia wa nguvu kutoka kituo cha Clouds Media Group. 

Akizungumza leo na mtandao wa matukiodaimablog Abwao ambae kwa sasa ni mwanachama na mjumbe wa baraza kuu Taifa la chama cha ACT wazalendo alisema kuwa amepigiwa simu na waandaaji wa tuzo hiyo kutoka Clouds Media Group kujulishwa na kutakiwa kufika Dar es  salam Kesho jumamosi kupokea tuzo hiyo. 

"nimepokea kwa furaha kubwa taarifa hiyo nachotaka kusema tuzo hii imekuja kwangu ila ni heshima kwa chama changu na heshima kwa wanawake wote wa mkoa wa Iringa"

Alisema kuwa kutokana na kubanwa na majukumu kesho hataweza kushiriki hafla hiyo jijini Dar es Salama ila atamtuma mtoto wake kwenda kupokea tuzo hiyo ya heshima. 

Hata hivyo amepingeza kituo cha Clouds media Group kwa kuandaa tuzo hiyo huku akiwataka wanawake kuendelea kujiamini kwani wanaweza hata bila kuwezeshwa. 

Katika uchaguzi uliopita Chiku Abwao alikuwa mmoja kati ya wagombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia Chama cha ACT wazalendo ila kura hazikutosha na sasa anajishughulisha na biashara kwa kufuata vifaa vya maofisini kutoka nchini China na kuziuza  hapa nchini. 

CCM YAIKOSOA CHADEMA NA CUF UBUNGE WA AFRIKA YA MASHARIKI


 boss7
Ndugu waandishi wa habari,
 
Tunawashukuru
kwa kupokea wito wetu na  kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba
 tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.
 
Aidha
Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini
kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na
kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya
maendeleo,   mikakati, sera na malengo ya Serikali  na mipango ya vyama
vya siasa.
 
Ndugu Waandishi wa habari.
 
Tumewaita
leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa
demokrasia katika  mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la
Jumuiya ya  Afrika Mashariki  (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya
upinzani  nchini.
 
Bunge
la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya
pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua
dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi
wa Mataifa yote yaliyomo  katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja
ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.
 
Ni
jambo la heri na faraja kuona EAC  ya  sasa ikiwa ni yenye kufikia
malengo ya  utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na
kiusalama kama vile  kuwa na  Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya
wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata
 viwango sawia vya ushuru wa Forodha.
 
Masuala
mengine ni kuona  maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa
hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana
kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko
Burundi yamekuwa yakiendelea  chini ya mpatanishi mkuu  Rais mstaafu
Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama
tukishuhudia  wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.
 
Ni
katika jumla ya mambo yanayofurahisha na pengine yakiwasuta na
kuwaaibisha maadui na vibaraka ambao aghalab  hutumiwa kwa malipo yenye
ujira wa dhambi  toka kwa mabeberu katika kuhakikisha  mipango batili ya
kutaka kudhoofisha, kuigawa na kukwamisha juhudi za EAC isiimarike..
 
Aidha
kuibuliwa na kupokewa kwa mpango uitwao ” One Stop Boarder” yaani (OSB)
 sasa umefanikiwa huko mipakani baina ya nchi wanachama.  Pia
kuanzishwa  miradi mikubwa ya kiuchumi mfano bomba la mafuta toka
Kampala (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) ujenzi wa reli toka kigali hadi
Uganda huku EAC ikielekea kuwa na sarafu moja kabla ya kufikiwa azimio
la  uundwaji wa Shirikisho moja.
 
Umoja
wa Vijana wa CCM tumelazimika kuyataja na kuyaainisha maeneo hayo
yaliopata mafanikio kwa uchache  lengo likiwa ni kuonyesha  uwepo na
ustawi wa EAC pamoja na umuhimu wa bunge lake kama ni jambo nyeti na
wala si suala dogo au la mchezo mchezo kama ambavyo baadhi ya vyama vya
siasa nchini vimeonyesha udhaifu.
 
Ndugu Waandishi wa Habari,
 
Baadhi
ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa hata  kuteua wagombea ubunge
wengi ili kuwania nafasi katika bunge hilo  la Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa sababu zinazotokana  aidha na ubinafsi, umimi na udikteta.
 
Tunachukua
fursa hii kwanza kukipongeza Chama Cha Mapinduzi na wanachama wake wote
450 ambao kwa ujasiri, uwezo na kujiamini kwao wamethubutu kujitokeza
na kuchukua fomu za  kuwania nafasi za ubunge wa EAC.
 
Kitendo
cha wanachama hao wa CCM kujitokeza kwa wingi kimsingi
 kimeidhihirishia dunia kwamba chama chetu bado ni cha kidemokrasia
kinachoungwa mkono na kuaminiwa na wananchi wengi wakiwemo  Vijana,
wanawake na wana taaluma mbali mbali wakitambua ndicho chama pekee imara
chenye kujali, kuthamini na kufuata misingi ya usawa na demokrasia ya
kweli.
 
Wanachama 450 wa
CCM walichukua fomu kwa kufuata taratibu baada ya mchujo wa kidemokrasia
kufanyika ndani ya CCM,  wanachama   12 wamebahatika kuteuliwa na vikao
vya kikatiba  ambapo sasa wagombea hao watasimama mbele ya wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaka ridhaa  kwa kujieleza na
kuomba kura.
 
Ndugu Waandishi wa habari,
 
Umoja
wa Vijana CCM  kwa  tunasikitishwa sana na mwenendo wa demokrasia ndani
ya vyama vya upinzani  katika uteuzi wa kuwapata wagombea wa ubunge  wa
bunge la Afrika Mashariki (EALA)   Chadema, CUF  na NCCR Mageuzi kwa
jinsi walivyowasilisha  uwakilishi haba na finyu lakini pia kujitokeza
kwa wagombea wachache hali inayoonyesha uminyaji wa demokrasia ndani ya
vyama vyao.
 
Chadema na
washirika wao mara kadhaa hujigamba vichochoroni na kujionyesha kuwa wao
ni  watetezi  wa demokrasia lakini unapofikia wakati wa utekelezaji wa
jambo hilo  kwa vitendo, ndani ya chama hicho humea ukandamizaji wa haki
na kujitokeza  upendeleo, ukanda, kubebana  aidha kwa asili, ujamaa na
urafiki au kulipana fadhila.
 
Katu
huu si mwenendo mwema ulioonyeshwa na vyama vya upinzani. Vimejipaka
matope ya fedheha kwa kushindwa  kuonyesha kama ni waumini wa kweli wa
demokrasia badala yake havikujali wala kuheshimu dhana ya demokrasia na
kujikuta  vimejianika na kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa  vyama
hivyo ni vya watu maalum vya kibwanyenye na vya kiimla .
 
Kufanya
uteuzi wa wanachama wanaogombea nafasi za kidemokrasia kwa kumtazama
asili yake, anatoka  kanda ipi, kabila, imani yake au nasaba licha ya
 kwenda kinyume na misingi ya Taifa letu lakini pia ni kinyume na
matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
UVCCM
kwa kauli moja tunawaamsha na kuwatumia ujumbe watanzania wenzetu
hususan Vijana mahali popote walipo wavikatae na kuvikwepa vyama vya
aina hiyo, wasikubali kugawanywa kwa asili zao, imani au rangi na
nasaba.
 
Taifa letu ni
alama pana ya kuenzi na kudumisha demokrasia si tu barani Afrika lakini
vile vile duniani kote, hivyo kwa umoja wetu, kwa nguvu zetu, akili na
maarifa tulionayo, abadan tusijaribu kuichezea amani yetu, umoja na
mshikamano wetu  uliojengwa na waasisi wa Taifa letu na kukubali
 kuvishabikia vyama na viongozi wasaka madaraka kwa hila ambao ni
 wafujaji na wakandamizaji wa misingi ya demokrasia ndani ya vyama kama
ilivyojionyesha  kwa vyama vya upinzani vya Tanzania katika uteuzi wa
wabunge EAC.
 
Mchakato wa Uchaguzi ndani ya UVCCM.
 
Uchaguzi
Mkuu wa CCM wa mwaka 2017, unafanyika wakati ambapo CCM inatimiza miaka
40 tokea kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari, 1977 na ni wakati ambapo
nchi yetu inatimiza miaka 25 ya Mfumo wa Vyama Vingi ulioridhiwa na
Mkutano Mkuu wa CCM kutokana na busara za Viongozi wake.
 
Ratiba
ya Uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake inaonesha mchakato wa
Uchaguzi wa Jumuiya za CCM kuwa unaanza kabla ya ule wa CCM. Utaratibu
huu unalenga kuwawezesha wanachama wa Jumuiya za CCM ambao watakuwa ni
wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika CCM, au wale
waliochaguliwa kuwakilisha Jumuiya zao katika Vikao vya CCM ili waweze
kuhudhuria mikutano ya Chama inayowahusu.
 
Umoja
wa Vijana wa CCM umekamilisha maandalizi yote ya msingi ya awali kwa
ajili ya Uchaguzi unaotarajia kuanza tarehe 1 April, 2017 ikiwemo
kusambaza vifaa katika Mikoa na Wilaya zote nchini wa ajili ya
kufanikisha uchaguzi kwa wakati.
 
Aidha
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
imekamilisha mapitio na uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika
Jumuiya ambao watakuwa ndio wakurugenzi wa Uchaguzi katika maeneo yao.
 
Tunaendelea
kuwakumbusha Watendaji wetu muda wote kusimamia haki, ukweli na usawa
lazima vijana wa CCM muda wote tuishi katika maneno na maagizo ya
Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Hatutamvumilia
mtendaji yeyote atakayekiuka Kanuni, Taratibu na miongozo kwa makusudi
ili kufurahisha kikundi au watu fulani. Uchaguzi huu 2017 UVCCM tunataka
kuidhihirishia dunia na Vyama vya Upinzani kuwa CCM ni Chuo Cha
Demokrasia ulimwenguni.
 
Mwisho
niendelee kuwahamasisha vyema wote nchini yenye sifa kujitokeza kwa
wingi kugombea nafasi mbali za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake
kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa.
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
 
KAIMU KATIBU MKUU
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wana Habari Makao Makuu UVCCM Upanga (PICHA NA FAHADI SIRAJI)

NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA NAIPENDA TANZANIA

Watanzania waliowengi ni watu wenye mapenzi mema na Taifa lao na wengi wao hupenda mavazi yenye nembo ya Taifa kama ilivyo Kwa kijana Onno Mella mkazi wa Mtwivila mjini Iringa

Mapenzi mema ya Taifa ni nguzo kubwa ya uzalendo japo hadi sasa bado vazi rasmi la Taifa halijatanganzwa pamoja na kuwepo kwa mchakato wa mapendekezo ya vazi la Taifa kufanyika.

Wito wangu Kwa watanzania kutenga japo siku mbili za Wiki kuvaa vazi la Taifa 

UMAKINI UNAHITAJIKA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII

Image result for www.mitandao wa kijamii

Zaidi ya asilimia 60 ya watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 wanatumia zaidi ya masaa mawili kila siku kuangalia mitandao ya kijamii pamoja na vipindi mbalimbali vya Televisheni mwandishi  Benjamin Sawe wa Maelezo Dar es Salaam ameandika.


Hii inaweza kuwa njia kubwa ya kuunganisha, lakini pia kuna hatari zinazohusiana na kutumia muda mwingi sana kwenye vyombo vya habari kijamii.

Leo hii ni nadra kukuta familia ambazo watoto na vijana wake hawajaathirika na vyombo vya habari na elektroniki kama vile televisheni, intaneti na michezo mingine tofauti ya kompyuta.

Hata hivyo utumiaji mkubwa na wa masaa mengi wa vyombo hivyo hauwahusu watoto na vijana tu, bali watu wazima pia wameathirika na jambo hilo.

 Kutokana na sababu kadhaa za kimwili, kisaikolojia na kiroho, kuna udharura kwa watoto kusimamiwa vyema na wazazi, mashirika na taasisi za kielimu na kiutamaduni na kadhalika vyombo vya habari ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi mabaya ya vyombo hivyo vya elektroniki.

Licha ya kompyuta kuwa na pande chanya tofauti za kimaendeleo, hasa katika nyanja za kielimu na huduma za mawasiliano, lakini chombo hicho pia kina nafasi hasi kwa watoto na hata kwa watu wazima.

Utumiwaji usio na udhibiti wa chombo hicho na kadhalika vyombo vingine vya elektroniki kama vile televisheni, unaweza kuyaweka hatarini maisha ya watoto kutokana na athari zake mbaya kwa ustawi wa kiroho, kisaikolojia na kijamii wa watoto hao.

Harakati zetu za kifizikia na miamala yetu tofauti ya kijamii, ni umuhimu yenye taathira kubwa kwa afya na tabia za mtoto. Kinyume chake, ikiwa mtoto atatumia muda wake mwingi katika matumizi ya michezo ya kompyuta, basi hawezi kunufaika na upande chanya wa kujenga akili yake wala harakati bora kwa ajili ya kuufikia ukamilifu wake kijamii.

Mbali na hayo, watoto pia wanaweza kukabiliwa na hatari ya kutekeleza vitendo vya ukatili na visivyo vya kikatili hata katika umri wao mdogo. 

Hali hiyo ambayo inaweza kufikiwa ghafla au hata kwa makusudi, huwaletea watoto na vijana madhara yasiyoweza kufidika hasa kuhusiana na masuala ya kiafya, kisaikolojia sambamba na kueneza kwa kiasi kikubwa matatizo ya kimwili na kiakili kama vile utovu wa maadili, vitendo vya ukatili, madawa ya kulevya, tabia mbaya katika jamii, kuzorota thamani za familia na kuenea jinai na uhalifu wa kila aina katika jamii.

Ukweli ni kwamba, wazazi hawajawachwa peke yao katika jukumu la kutoa malezi bora kwa watoto wao, bali wataalamu wa mambo wamefanya utafiti wa kina katika uwanja huo na kuwasaidia katika suala hilo kwa kuwasilisha njia bora za malezi ambazo zinawavutia watoto na kuwafanya waishi maisha bora katika jamii.

Watafiti hao wanasema kuwa, licha ya kwamba haiwezekani kuwatenga watoto na ulimwengu wa michezo ya kompyuta lakini tunaweza kuwaepusha na madhara ya michezo hiyo kwa kutumia njia na mbinu zinazofaa.

Udhibiti fulani wa matumizi ya kompyuta kila siku au kwa wiki, ni moja ya njia hizo. Kwa mbinu hiyo, mtoto anaweza kutumia chombo hicho kwa muda na kiwango kilichoainishwa na kila pale anapokwenda kinyume na kiwango hicho, basi anapasa kuzuiwa na kuadhibiwa.

Hata hivyo utumiaji mabavu na nguvu hauna nafasi katika hapa. Katika kesi kama hiyo njia ya mazungumzo sanjari na kumzuia kwa muda, kutumia vitu anavyovipenda mtoto huyo, inafaa kutumiwa hapa.
Wakati mwingine mtoto hutumia vyema kompyuta kwa kujinufaisha kielimu na chombo hicho muhimu cha teknolojia na kwa kweli katika hali kama hii wazazi hawapaswi kumzuia mtoto kutumia chombo hicho cha kompyuta. Lakini jambo linalopaswa kuzuiwa ni tabia ya mtoto huyo kutumia wakati wake mwingi katika kichezo isiyofaa ya kompyuta.

Moja ya nyenzo zingine za udhibiti ambazo zinaweza kutumiwa na wazazi katika kusimamia mienendo ya mtoto, ni uwezekano wa kutumia mbinu zinazodhibiti mfumo wa kompyuta. Kwa utaratibu huo watoto hawawezi kuingiza program mpya au kuweka windozi tofauti ambazo ni rahisi kuweza kuwaharibu watoto.

Njia nyingine ni pamoja na kuzuia kuondolewa program zilizopo katika kompyuta au kuzizuia zisifanye kazi, ni moja ya njia ambazo zinaweza kutumiwa katika kuwadhibiti watoto.
Miongoni mwa njia nyepesi zaidi kwa wazazi katika kumlinda mtoto wao wakati wa kutumia njia na nyenzo zinazohusiana na ulimwengu wa intaneti, ni kuweka mfumo wa kompyuta nje ya chumba chake cha kulala. Njia hiyo itawasaidia wazazi wakati wa kutumia mtoto chombo hicho nao waweze kushuhudia na kufuatilia kwa karibu michezo na shughuliza zote za mtoto huyo anapotumia kompyuta.

Kwa hakika vivutio vya kompyuta na michezo mingine ya kielektroniki kwa watoto havina kikomo, na ikiwa hakutakuwepo usimamizi madhubuti wa wazazi kwa mtoto wao, basi huenda mtoto bila kujijua, akatumia wakati mwingi zaidi kuliko inavyotakiwa na hivyo kuathiri lishe, usingizi na hata masomo yake.

 Hapo ndipo wazazi wanapotakiwa kuwa macho na kuhakikisha wanasimamia vyema malezi ya mtoto wao sanjari na kumuandalia ratiba nzuri ya maisha yake na kuchunga sheria watakazomuainishia kila wiki.

Aidha wazazi wanatakiwa kumuweka mbali mtoto wao na ulimwengu wa elektroniki na michezo ya kompyuta wakati wa kipindi cha masomo. Watafiti wanasema kuwa,  kuna ulazima mkubwa wa kuzingatiwa wakati wa matumizi ya watoto kwa vyombo vya umeme kama vile kompyuta,

 labtop na tablet na kile ambacho kinahusiana na ulimwengu wa kielektroniki, kwani utafiti unaonyesha kwamba matumizi mengi ya vyombo hivyo kupita kiasi na kufikia kiwango cha uraibu, hupunguza uwezo wa kifikra wa mtoto.

 Na kukithiri kwa  maradhi hayo kwa watoto ndio mwanzo wa kufeli katika hatua zao za kielimu sanjari na kushindwa kukabiliana na mikikimikiki mingine ya kimaisha ambayo anapaswa kukabiliana nayo katika mustakbali wa maisha yake ya mbeleni.

 Katika matumizi ya michezo ya kompyuta au ulimwengu wa intaneti, kuna udharura wa kujitenga na mambo machafu yasiyofaa. Aidha inaelezwa kuwa, kutumia sana kompyuta na intaneti, taratibu huibua tatizo la unene, ambalo mara nyingi hupelekea watoto na hasa vijana wengi kujichukia wenyewe kutokana na tatizo hilo.

 Hivyo kuna haja kwa wazazi kuwaepusha watoto wao na unene na uzembe unaosababishwa na matumizi ya muda mrefu ya vyombo vya umeme hasa michezo ya kompyuta.
Wataalamu wengi wanaamini kuwa, ni muhimu kuwatenga watoto walio na umri wa chini ya miaka mitatu na aina yoyote ya matumizi ya kompyuta. Kwa maana nyingine ni kwamba, umri huo hauoani na matumizi ya kompyuta au video.

 Hata hivyo ikiwa mtoto aliye na umri wa chini ya miaka mitano ataingia katika ulimwengu wa matumizi ya vyombo hivyo na kuvizoea, basi lazima awekewe sheria na vidhibiti maalumu vya kumuwezesha kukabiliana na hatari ya ulimwengu huo. Kwanza anapasa kufahamishwa ni kwa kipindi gani anatakiwa atumie vyombo hivyo na kisha baada ya hapo ajishughulishe na kazi nyingine.

Watafiti wanapendekeza kuwa, mtoto mwenye umri wa kuinukia anatakiwa atazame kwa saa moja au masaa mawili filamu na katuni, upekuzi katika intaneti na michezo mingine ya video katika kompyuta. Ikiwa mtoto kwa siku atatumia dakika 45 kucheza mchezo wa kompyuta na muda mwingine mdogo kutazama televisheni na mwingine mfupi kujishughulisha na harakati za kifizikia, basi hakutakuwepo na wasi wasi wa kuathirika afya yake. Lakini ikiwa atatumia masaa mengi kujishughulisha na michezo ya kompyuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa, basi hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo.

Madaktari wanashauri kwamba, watoto wanatakiwa kutumia masaa mawili tu kwa siku kutazama televisheni. Televisheni ina athari nyingi muhimu kwa watoto wengi wanaosoma na hasa katika kupumzisha mwili na fikra zao.

Hivyo wazazi na walimu wanatakiwa kusimamia ni kiasi gani watoto wanapaswa kutazama televisheni. Hii ni katika hali ambayo katika miaka ya awali watoto wanaosoma shule za msingi, huwa hawana uwezo wa kupanga vyema ratiba za kutazama televisheni.

Mwisho

GHANA KUTUA, SERENGETI BOYS KUIVAA TENA BURUNDI

Timu ya taifa ya vijana ya Ghana wenye umri wa chini ya umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Black Starlets, inatarajiwa kutua kesho Jumamosi Aprili mosi saa 9.40 usiku kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Serengeti Boys ambayo ni timu ya taifa ya vijana ya Tanzania.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, kati ya wageni The Black Starlets na Serengeti Boys unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10.00 jioni. Timu hiyo itafikia Hoteli ya Southren Sun.
Huo utakuwa ni mchezo wa tatu wa kimataifa kwa Serengeti Boys ndani ya wiki moja tangu timu hiyo ianze kambi mwishoni mwa Januari, mwaka huu kwani jana Machi 30, mwaka huu ilicheza mechi yake ya kwanza na kuilaza Burundi mabao 3-0.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jana, Serengeti Boys iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi kwenye Uwanja huo wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na fainali za vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi wa Kimataifa - Mtanzania, mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa, wenyeji walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza 2-0.
Mabao hayo yalifungwa na Mshambuliaji Muhsin Makame na beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyepanda kusaidia mashambulizi.
Makame alifunga dakika ya 19 akimalizia pasi ya Kelvin Nashon kutoka upande wa kulia, wakati Kibabage alifunga dakika ya 38 baada ya kupanda na mpira upande wa kushoto na kuingia nao ndani kabla ya kumtungua kipa Djuma Bitiyaweho.
Pamoja na wenyeji kurudi vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0, lakini timu hizo zilishambulkiana kwa zamu na labda tu Burundi walikwamishwa na uimara wa safu ya ulinzi ya Tanzania.
Kipindi cha pili nyota ya vijana wa kocha Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ anayesaidiwa na Mshauri wa Ufundi, Kim Poulsen kutoka Denmark, iliendelea kung’ara baada ya kufanikiwa kupata bao la tatu, lililofungwa na Yohana Mkomola katika dakika ya 72.
Mkomola  alifunga bao hilo kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Burundi kuunawa mpira uliopigwa na beki wa kushoto, Nickson Kibabage.
Serengeti Boys iliendelea kucheza vizuri kwa kushambulia kusaka mabao zaidi, lakini waliishia kupoteza nafasi. 

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Dickson Nickson, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Henrick Nkosi, Ally Ng’anzi, Shaaban Zubery, Muhsin Makame, Asad Juma, Kevin Naftali na Yohana Nkomola/Ibrahim Abdallah dk79.
Burundi; Djuma Bitiyaweho, Omar Nzeyimana, Paul Amayungo, Djuma Ndayisenga, Blandin Muhimpundu, Simon Akabeza, Hugue Ininahazwe/Pierre niyonkuru dk60, Jean Noel Nzoyiha/Angelo Buberintwari dk46, Theodore Ngabirano/Fiston Uwizeye dk85, Akbar Asumani/Djuma Minani dk59 na Frank Nzojibwami.

HUU HAPA MZUNGUKO WA 25 LIGI KUU YA VODACOM

Baada ya kusimama kwa muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.
Michezo ya kesho Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam - mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi, zitafanyika saa 10.00 jioni.
Mechi za ligi hiyo ambazo huoneshwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho ni mdhamini mwenza wa VPL, itaendelea Jumapili ambako Kagera Sugar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huo utakuwa saa 10.00 jioni 
Mchezo mwingine utazikutanisha timu za African Lyon ya Dar es Salaam dhidi Stand United ya Shinyanga utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huu, utaanza saa 8.00 mchana kwa kuwa kanuni zinaridhia.
Mtibwa Sugar ya Morogoro watakuwa wageni wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo wakati Mwadui FC, kwa upende wake watawaalika JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga huku Majimaji wakiwa ni wenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea