February 8, 2017

WIZARA YA ARIDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YAZIDI KUTEKELEZA KWA VITENDO


Waziri  wa ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi akikabidhi hati ya ardhi kwa mkazi wa  wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro jana

Mkazi wa Mvomero akifurahia  kupewa hati ya ardhi  na  waziri Lukuvi

Waziri  Lukuvi  akiwa katika picha ya pamoja na  wananchi  waliopewa  hati ya ardhi


Na Afisahabari wilaya ya Mvomero

Serikali inaendelea kutekeleza ahadi yake kukamilisha kupima kila kipande cha ardhi na kumilikisha kwa wahusika na kukamilisha ndani ya miaka mitano.

Hayo yameelezwa jana  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa uzinduzi wa utoaji wa hati miliki za kimila katika vijiji vya Hembeti na Dihombo Wilayani Mvomero.

Hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kilamwananchi kwa kipande atakachomilikishwa apewe na hati ya kipande hicho cha ardhi anachomiliki.

Hata hivyo amewataka wakazi wa kijiji cha Kambala ambako zoezi hilo lilikuwa halijaanza kwa sababu ya kuwekewa zuio kupitia vyombo vya kisheria sasa kesi imeisha na wameruhusiwa kuendelea na zoezi na kwamba wakae mkao wa kula kwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kufanya sensa ya mifugo iliyopo ndani ya kijiji hicho.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE