February 14, 2017

​WAZIRI MKUU APOKEA SH. MILIONI 5.6 ZA MADAWATI

MAJALIWA MCHANGO MADAWATI CUE IN
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wawe wabunifu katika kusaidia kutafuta vyanzo vya mapato kwenye jamii inayowazunguka.
Ametoa wito huo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) ofisini kwake mjini Dodoma mara baada ya kupokea mchango wa sh. milioni 5.6 kwa ajili ya kununulia madawati 70 kutoka kwa watumishi wa TAMISEMI – Dodoma.
Amesema ubunifu huo uliofanywa na watumishi wa TAMISEMI, ni mfano mzuri wa kuigwa na watumishi wengine nchini kwani utaisaidia Serikali kuleta maendeleo.
“Hii ni mara ya tatu kwa TAMISEMI kuchangia huduma za jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini… lakini pia niwashukuru kwa kuchagua jimbo la Ruangwa kuwa miongoni  mwa maeneo ambayo ni wanufaika wa mchango wenu,” amesema.
“Mchango huu ni mkubwa na utasaidia mikondo miwili kwa shule za sekondari. Tunahitaji kupata mawazo mapya kama haya, na tunahitaji wafanyakazi wengine wajifunze kutoka TAMISEMI,” amesema.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wao, kiongozi wa ujumbe ulioenda kuwasilisha mchango kwa Waziri Mkuu, Bw. Filbert Rwakilomba amesema lengo lao ni kuchangia madawati 100 lakini wameamua kutanguliza mchango wa madawati 70 na baada ya siku mbili watakabidhi mchango wa madawati 30 yaliyobakia.
Bw. Rwakilomba ambaye anaongoza kamati ya watu 30 ambao ni watumishi kutoka idara tofauti za Ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma, amesema wametoa mchango huo kama ishara ya kuenzi kazi aliyoifanya Waziri Mkuu Majaliwa wakati akiwa Naibu Waziri (TAMISEMI – Elimu).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
DODOMA.
JUMANNE, FEBRUARI 14, 2017.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE