February 8, 2017

WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA IRINGA ..............

Kamanda  wa  polisi mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi
...................................................................................................................................................
 
NA MATUKIDAIMA BLOG , IRINGA
JESHI  la  polisi  mkoa  wa  Iringa limewakamata  wafanyabiashara  wawili  akiwemo  mwanamkemmoja kwa  tuhuma  za   kuhusika na  biashara  ya  dawa  za  kulevya  na  kufanya  idadi ya  waliokamatwa  hadi  sasa  kufikia  watu 21  .

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  Iringa  Julius Mjengi  alimweleza  mwandishi  wa mtandao huu wa matukiodaimablog  kuwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa  linaendelea  na oparesheni kali ya  kuwakamata  wale  wote wanaojihusisha na  biashara  za dawa za  kulevya pamoja na watumiaji wa dawa   hizo.

Alisema  kuwa  oparesheni   hiyo  imekuwa  ikiendeshwa  maeneo mbali mbali  vikiwemo  vijiwe ambavyo  wanashinda  watumiaji wa dawa  za  kulevya pamoja na nyumba mbali mbali na maeneo ya  biashara ambayo  yametajwa  kuhusika na biashara  hiyo .

Hata  hivyo  alisema hadi juzi  jumla ya  watumihiwa 19  walikuwa  wamekamatwa kati yao   wapo  wafanyabiashara watano na watumiaji  14 ila  kufikia  jana  Februari 8  jumla  ya watu 21  wamekamatwa baada  ya kuongezeka  wafanyabiashara  wawili .

  Jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa halilali lipo kazini  muda  wote  na tumefanikiwa  kupata majina ya  watu  mbali mbali  wanaojihusisha na utumiaji wa dawa  za kulevya na wauzaji  tunaendelea kuwasaka mmoja baada ya mwingine “

Hivyo  alipongeza ushirikiano mkubwa ambao  wananchi  wanaendelea  kuutoa kwa  jeshi la polisi  mkoa wa Iringa  dhidi ya vita   ya dawa za kulevya na  kuwataka  wananchi  kuendeleza ushirikiano  huo  ili kuhakikisha  mkoa  wa Iringa unakuwa mkoa  salama  usio na watumiaji ama  wauzaji wa dawa za  kulevya .
Kamanda  huyo  wa  polisi alisema  kuwa majina ya  watuhumiwa hao watatajwa  baada ya  zoezi la  kuwahoji  na  kuwakamata   watuhumiwa  wengine  kukamilika kwani iwapo watawekwa hadharani  sasa  itakuwa  vigumu  kuupata mtandao mzima  wa dawa  za  kulevya  mkoa  wa Iringa .
 
“ Watuhumiwa wote hawa  watafikishwa mahakamani  wakati  wowote  mara  baada ya  upelelezi  kukamilika ..ombi la jeshi la  polisi wananchi  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa  kuwafichua  wale  wote wanaojihusisha na dawa  za kulevya “
 
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE