February 13, 2017

WACHIMBAJI WADOGO WAFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MGODI WA BUHEMBA


HABARI zilizotufikia hivi punde zimeelza kuwa wachimbaji sita wa madini wanadaiwa kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba madini kwenye mgodi wa Buhemba ulioko mkoani Mara.

Imeelezwa pia kuwa watu 11 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Butiama kwa ajili ya matibabu.

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi ambaye amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo, na hivi sasa nipo eneo la tukio. Kuhusu takwimu sahihi za watu waliofukiwa kwa sasa sina, mpaka uchunguzi wa jeshi la polisi utakapofanyika ndipo nitatoa ripoti kamili.” Alisema Kamanda Ng’anzi.


Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kifupi ambapo siku za hivi karibuni, wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa baada ya siku kadhaa katika Mgodi wa RZ, Nyarugusu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.

 (Chanzo Global Publishers )

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE