February 16, 2017

UVCCM NA NIA YA KUKUZA MUZIKI NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu  UVCCM Taifa  Ndg Shaka Hamdu Shaka kwa nyakati  tofauti leo 15 Februari  amekutana na kufanya mazungumzo na wasanii wa muziki  nguli hapa nchini  akiwemo  Msanii Banana Zoro na msanii  mwanadada Stara Thomas waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya UVCCM, Jijini Dare es Salaam.
Katika mazungumzo yake na wasanii hao nguli na wenye mafanikio makubwa nchini katika medani ya mziki Kaimu Katibu  Mkuu alipokea Ushauri na namna bora zaidi ya kuboresha bendi ya UVCCM  VIJANA JAZZ BAND wana “Saga rumba” ambayo hufanya maonesho yake kila siku ya Jumapili eneo la Vijana Social Kinondoni.
Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, wote kwa pamoja wameahidi ushirikiano mkubwa katika maboresho makubwa na stahiki kwa bendi ili sasa ijiendeshe kitaalam.
“Vijana jazz ni bendi iliyojijengea heshima miaka mingi hivyo ni tuna kila sababu ya kuimarisha ili iweze kujitangaza na kufikia mafanikio kulingana na mahitajio ya muda tuliona ” alisema Banana.
Kwa upande wake Stara Thomas katika maongezi yake na Kaimu katibu mkuu alisema “Hii ni bendi inayopaswa sasa kuwa chuo cha muziki kwa vijana waje wajifunze mziki na kusambaa kwingineko”
Katibu mkuu Ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa kwake na wanamuziki hao kwa ukizingatia kauli mbiu ya CCM Mpya Tanzania Mpya sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana kupitia mziki wa dance.

Kaimu Katibu Mkuu  UVCCM Taifa  Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwa katika mazungumzo hayo

Kaimu Katibu Mkuu  UVCCM Taifa  Ndg Shaka Hamdu Shaka akifanya mazungumzo na msanii BananaZorro

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE