February 7, 2017

UPINZANI WAMKACHA DR TULIA,WATOKA NJE YA BUNGE KUPINGA MAAMUZI YAKE

Image result for wabunge watoka nje


Kutoka Dodoma Bungeni sasa hivi naambiwa Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya ukumbi wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Naibu Spika Dr. Tulia.
Inaripotiwa kwamba Naibu Spika Dr. Tulia aliamuru kutolewa nje kwa Mbunge Halima Mdee na mwenzake waliopaza sauti ndani ya bunge baada ya Naibu spika kukataa mwongozo wa kujadili sababu za kukamatwa kwa Mbunge Tundu Lissu jana.
 Related image

Baada ya amri ya kuwatoa nje Halima Mdee na mwenzake inaripotiwa na Wabunge wengine wa upinzani wakachukua uamuzi wa kutoka nje ambapo hapa chini kwenye hii video fupi wanaongea Zitto Kabwe na Halima Mdee.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE