February 11, 2017

UONGOZI WA SHULE YA SUN ACADEM IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA KUPAMBANA NA UFISADI PIA VITA YA DAWA ZA KULEVYA ..........

Mkurugenzi  wa shule ya  Sun Academi Chengula Nguvu kushoto  akimkabidhi  zawadi  mwalimu mkuu  wa  shule  hiyo  James Mwakamele  wakati wa hafla ya  kuwapongeza wanafunzi  wa darasa la tano na  walimu kwa  kuiwezesha shule hiyo kushika nafasi ya  pili  kiwilaya mtihani wa taifa wa   darasa la nne mwaka jana
Mkurugenzi wa  shule ya  Sun Academi  Iringa  Chengula  Nguvu  akitoa  pongezi  zake kwa  Rais Dkt John Magufuli  dhidi ya  vita ya dawa za  kulevya  leo
Mkurugenzi  huyo  akikabidhi  zawadi kwa  walimu
Timu  nzima ya  walimu  wa Sun Academi
Mmoja  kati ya wazazi  akimpongeza  mtoto  wake
Mkurugenzi  wa  Sun Academi  Iringa  akimwamasisha  mwanafunzi  kusoma  zaidi

Mmoja kati ya  wazazi  akitoa ufafanuzi wa zawadi  alizojitolea kwa ajili ya  wanafunzi
Na MATUKIODAIMABLOG
UONGOZI  wa  shule  ya  Sun Academi  Iringa  umepongeza  kazi  nzuri  inayofanywa na  serikali ya  awamu ya tano chini ya  Rais Dkt  John Magufuli katika  kupambana na vitendo vya  ufisadi ,rushwa na dawa  za  kulevya  kuwa   vita  hiyo  imerejesha   heshima ya Taifa .

Akitoa pongezi  hizo wakati wa hafala ya  kuwapongeza  wanafunzi  wanafunzi 35  wa  darasa la tano ambao  walifanya  vizuri  katika  mitihani  ya Taifa  ya  darasa la nne mwaka jana na kuifanya  shule   hiyo  kushika nafasi ya pili kwa  wilaya ya  Iringa kuwa Rais   anapaswa  kumpongeza Rais  Dkt  Magufuli na serikali yake  kwani kazi anayoifanya imeleta  heshima kubwa  kwa taifa .

Bw Nguvu  alisema kwa upande wa ufisadi na Rushwa  hivi  sasa watanzania  wote  wameunganishwa pamoja kwa  aliye nacho na asiyenancho  wapo  sawa  tofauti na  zamani  ambapo  kulikuwa na matabaka kati ya  wenye nacho  ambao  wanapata  kwa  njia  zisizo sahihi na masikini .

Kwani  alisema kubana minya ya  ufisadi na rushwa  hivi  sasa  kila mtanzania anaishi kwa heshima kubwa na kila mmoja anatafuta  pesa ya  haki na sio  pesa  za  ufisadi na rushwa .

Kuhusu  vita  dhidi ya  dawa za kulevya  alisema  matunda ya  vita  hiyo yanaonekana kwa  kila mmoja tena ndani ya kipindi  kifupi  sana na kuwa wanaobeza  jitihada  hizo  hawajakumbwa na madhara  ya  dawa  hizo  za  kulevya .

Alisema iwapo  ungeshuhudia  kuona  vijana  wanavyo haribika kwa dawa  hizo  za kulevya na jinsi ambavyo Taifa  linavyopoteza  nguvu kazi  hiyo basi kusingekuwa na mtanzania kusikika akibeza jitihada  hizo.

Hivyo  pamoja na kumpongeza Rais  Dkt Magufuli kwa kazi  hiyo bado  alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na wakuu wote wa mikoa pamoja na jeshi la polisi kwa  kuendelea na mapambano hayo dhidi ya  dawa za  kulevya .UONGOZI  wa shule ya  Sun  Academi  Iringa  umewahakikishia wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika shule  hiyo  kuendelea  kuwa na imani  kubwa ya watoto wao  kufaulu  mtihani wa darasa la  saba pia  kuendelea  kufanya  vizuri  katika mitihani  mbali mbali ya  kitaifa .

Mwalimu  wa  taaluma  shuleni hapo Peter Joseph Nzalla  aliwaeleza  wazazi  alisema  kuwa  mafanikio ya  shule  hiyo  kufanya  vizuri  inatokana na ushirikiano  uliopo kati ya  wazazi ,walimu na  wanafunzi  wenyewe  ambao  wamekuwa  wakionyesha  ari ya  kujifunza na kuelewa kile  wanachofundishwa .

Nzalla alisema  kuwa mikakati ya  shule  hiyo ni kuona  shule  inaendelea  kufanya  vizuri na ikiwezekana kwa  mwakani  kuona  shule  hiyo inashika nafasi ya  kwanza  kitaifa  ama  kuingia katika  shule  10 bora .

Mwalimu  mkuu  wa  shule  hiyo Bw  James Mwakamele aliwataka  wazazi kuhakikisha  wanalipa kwa  wakati ada  ili  kuwezesha  shule  hiyo  kuweza  kuendesha shule  hiyo bila usumbufu .

Kwani  alisema  shule  hiyo  inamipango  mbali mbali ya  kielimu  kama ya  mitihani ya  moku ambayo  itafanyika mara kwa mara  ili  kuwaandaa  watoto kufanya  vema  zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE