February 16, 2017

TRA IRINGA YATAKA WAKULIMA WA MITI KULIPA KODI

Na matukiodaimaBlog
MAMLAKA ya mapato Tanzania ( TRA) Mkoa wa Iringa imewataka wakulima wa miti mkoani Iringa kutouza miti yao pasipo kufika TRA kulipa kodi.

Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Joseph Kahinga alitoa wito huo jana  wakati wa kikao Chake na wafanyabiashara wa mbao  pamoja na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto ofisini kwake.

Alisema kuwa ni sheria kwa mtu  yeyote wakiwemo wakulima kuhakikisha wanalipa kodi pindi wanapouza miti yao.

Kuwa kwa mkulima wa miti pindi anapohitaji kuuza miti anapaswa kufika TRA ili afanyiwe tathimini na kupangiwa kodi ya kulipa badala ya kuuza miti pasipo kulipia kodi.
 
"Haipaswi kwa wananuzi wa mbao  kununua mbao ama miti kwa wakulima pasipo kupewa risti ya TRA...hivyo ni wajibu wa wafanyabiashara wa miti na mbao  kuwaelimisha wakulima hao kufika TRA kabla ya kununua miti ama mbao"

Alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara wa mbao  wanaodhani kulipa ushuru wa halmashauri wa mazao ya mbao  ndio kodi ya TRA.

Pia alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao wanajidanganya kwa kutoa rushwa kwa watumishi wasio waaminifu wa TRA jambo ambalo wanajindanganya kwani mbali ya kutoa rushwa bado watabanwa kwa kodi kama kawaida.

Hivyo alimtaka mbunge wa Kilolo Mwamoto kuendelea kufikisha  elimu kwa wananchi wake juu  ya ulipaji kodi

Huku akisema  TRA Mkoa wa Iringa itaendelea kutoa kipaumbele kwa Kilolo ili kuona wilaya nzima wanapata elimu ya kodi 

Hata hivyo alimpongeza mbunge wa kilolo  kwa kuendelea kuwapa elimu wafanyabiashara na kutaka  wabunge wengine kuiga mfano huo.

Naye mbunge wa Kilolo Mwamoto aliomba kupewa mtaalam mmoja kila anapofinya ziara kwa lengo la kusaidia kutoa elimu kwa wananchi wake
Mwisho

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE