February 13, 2017

TAMASHA LA PASAKA KUMUOMBEA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA


1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka jijini Dar es salaam, Msama amesema maadalizi yanaendelea vizuri na wako kwenye mazungumo na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali kama vile Rwanda, Nigeria, Afrika Kusini Zambia na kwingineko ili kuboresha Tamasha hilo ambalo pia litafanyika katika mikoa kumi ya Tanzania.
Ameongeza kwamba Tamasha la mwaka huu pia lina kazi kubwa ya kumuombea Rais Wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta Maendeleo kwa watanzania lakini pia kupambana na vita mbaya ya Madawa ya Kulevya.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamashahilo wakati alipozungumza na jijini Dar es salaam jana.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE