February 11, 2017

SHULE YA SUN ACADEMI IRINGA YAJIWEKA SAWA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KITAIFA

mwalimu  wa taaluma katika  shule ya  Sun Academi Bw Petro Joseph  Nzalla  akitoa  taarifa ya shule  hiyo ,kulia ni mkurugenzi mtendaji wa shule  hiyo Chengulla Nguvu
 Mkuu  wa  shule ya  Sun Academi James Staff Mwakamela  akitoa  pongezi  zake kwa wazazi

 ................................................................................................................................................
 UONGOZI  wa shule ya  Sun  Academi  Iringa  umewahakikishia wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika shule  hiyo  kuendelea  kuwa na imani  kubwa ya watoto wao  kufaulu  mtihani wa darasa la  saba pia  kuendelea  kufanya  vizuri  katika mitihani  mbali mbali ya  kitaifa .

Mwalimu  wa  taaluma  shuleni hapo Peter Joseph Nzalla  aliwaeleza  wazazi  leo  wakati  wa hafla ya  kuwapongeza  wanafunzi 35  wa  darasa la tano ambao  walifanya  vizuri  katika  mitihani  ya Taifa  ya  darasa la nne mwaka jana na kuifanya  shule   hiyo  kushika nafasi ya pili kwa  wilaya ya  Iringa .

Alisema  kuwa  mafanikio ya  shule  hiyo  kufanya  vizuri  inatokana na ushirikiano  uliopo kati ya  wazazi ,walimu na  wanafunzi  wenyewe  ambao  wamekuwa  wakionyesha  ari ya  kujifunza na kuelewa kile  wanachofundishwa .

Nzalla alisema  kuwa mikakati ya  shule  hiyo ni kuona  shule  inaendelea  kufanya  vizuri na ikiwezekana kwa  mwakani  kuona  shule  hiyo inashika nafasi ya  kwanza  kitaifa  ama  kuingia katika  shule  10 bora .

Mwalimu  mkuu  wa  shule  hiyo Bw  James Mwakamele aliwataka  wazazi kuhakikisha  wanalipa kwa  wakati ada  ili  kuwezesha  shule  hiyo  kuweza  kuendesha shule  hiyo bila usumbufu .

Kwani  alisema  shule  hiyo  inamipango  mbali mbali ya  kielimu  kama ya  mitihani ya  moku ambayo  itafanyika mara kwa mara  ili  kuwaandaa  watoto kufanya  vema  zaidi.

Huku  mkurugenzi     mtendaji  wa   shule  hiyo  ya Sun Academi  Bw  Chengula  Nguvu  akitumia nafasi hiyo  kumpongeza  Rais  Dkt  John Magufuli kwa mapambano makubwa ya rushwa ,ufisadi na dawa  za  kuleva
  0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE