February 21, 2017

SERIKALI YAWATAKA MAAFISA HABARI KUTUMIA NJIA ZA KISASA ZA MAWASILIANO KUTANGAZA MAFANIKO YA SERIKALI

*Na Ismail Ngayonga*

*MAELEZO*

*Mwanza*

*21.2.2017*MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri nchini
wametakiwa kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo
matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na
mafanikio ya sera na mipango ya Serikali kwa wananchi.Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu
wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzinduzi wa tovuti za halmashauri
35 za mikoa 5 ya kanda ya ziwa inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara,
Shinyanga na Simiyu.


Dkt. Abbas alisema pamoja na kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari
vinavyotumika kufikisha taarifa za habari kwa wananchi ikiwemo magazeti na
redio, bado mitandao mitandao ya kijamii ikiwemo barua pepe imendelea
kutumia na wananchi wengi zaidi ulimwenguni kwa sasa.


“Kwa sasa nusu ya watu duniani wapo mtandaoni na hapa nchini kwa mujibu wa
ripoti ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) inaonyesha kuwa Watanzania
zaidi ya Milioni 19 wapo mtandaoni aidha kwa kutumia barua pepe au
kutembelea kurasa za facebook” alisema Dkt. Abbas.


Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema sifa za Afisa Habari na Mawasiliano wa
karne ya sasa ni mwenye uwezo wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano,
ambazo zitamwezesha kujibu hoja mbalimbali kwa haraka zaidi badala ya
kusubiri Serikali kulalamikiwa na wananchi.


Aidha Dkt. Abbas alisema uzinduzi wa tovuti katika mikoa na halmshauri hizo
ni kigezo muhimu kitakachotumiwa na Serikali katika kupima wa utendaji kazi
wa Maafisa Habari katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi.


Akifafanua zaidi Dkt. Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa
tovuti za mikoa na halmashauri za Wilaya nchini zinaendelea kuwa hai na
zenye taarifa zilizozingatia muda na wakati na hilo litawezekana iwapo
Maafisa Habari watatimiza malengo wanayopaswa kujiwekea katika maeneo yao
ya kazi.


“Litakuwa si jambo jema tunaona kuwa baada ya miaka 5 tovuti hizi
zimesimama, hii haitapendeza sana, hatuna budi tukatambua kuwa Serikali na
wafadhili wameweza fedha katika mradi huu, hivyo ni wajibu tukatimize
wajibu wetu” alisema Dkt. Abbas.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji wa Magu, Fundikira Fundikira alisema
Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari
ikiwem ukosefu wa vitendea kazi, ambapo hata hivyo suala hilo lisitumika
kama kigezo cha kuwakosesha wananchi taarifa.


Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Watendaji hao wa
Serikjali  ni deni kwao hivyo Maafisa Habari na TEHAMA hawana budi
kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao na kuleta tija iliyokusudiwa katika
maeneo yao ya kazi.


“Sisi kama Mkoa tutahakikisha kuwa tovuti hizi tunazisimamia na kuwa chachu
ya maendeleo kwa wananchi wetu, na kuhakikisha kuwa fedha za Serikali na
Wafadhili zinaleta tija kwa wananchi wetu”   alisema Fundikira.


Naye Mkurugenzi wa Miundombinu katika Wakala ya Serikali Mtandao (EGA),
Benjamin Dotto alisema Maafisa Habari na TEHAMA wanapaswa kuweka taarifa
mpya zilizozngatia muda na wakati kwa kuwa suala la upatikanaji ni
utekelezaji wa haki ya kimsingi ya binadamu pamoja na utekelezaji wa
mikataba mbalimbali ya kimataifa iliyosainiwa Serikali.


Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 13-20 Februari, yalifadhaliwa na Shirika la
Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE