February 27, 2017

SERIKALI YA MKOA WA IRINGA YAPONGEZA CHUO CHA PERAMIHO ,YATAKA VYUO VYA VETA KUIGA MFANO WA CHUO HICHOMkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akizindua  bodi  mpya ya  chuo  cha  VETA kanda ya  nyanda za  juu  kusini  leo

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  wa  pili kulia akiwa na bo akizindua  bodi  mpya ya  chuo  cha  VETA kanda ya  nyanda za  juu  kusini  leo


 ...........................................................
Na  MatukiodaimaBlog 
MKUU  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza amevitaka vyuo vya  ufundi stadi nchini  (VETA) kanda ya  nyanda za   juu kusini kuiga mfano wa chuo cha Peramiho mkoani Ruvuma .
Akizunndua  bodi mpya ya VETA  kanda ya  nyanda za juu  kusini  uliofanyika  leo  ukumbi wa  VETA Iringa, kuwa kati ya vyuo  bora ni  pamoja na chuo   hicho  cha Peramiho ambacho wanafunzi wake wa kushona  wanaotoka katika  chuo  hicho ni mafundi  waliobobea  kuliko hata mafundi  wakongwe wa mitaani .
“ Mimi  mwenyewe  ni  shahidi  juu ya ubora wa  elimu  unaotolewa katika  chuo  cha Peramiho  kuna mwalimu  wao  yupo  pale  ukimwagiza akushonee suti  anashona suti bora  kweli kweli  huwezi linganisha na hizi  za  madukani ama  mitaani ….lazima  vyuo kama   hivyo viwepo Iringa , Tabora , Mwanza na maeneo mengine ya  nchi “
Hata  hivyo alishauri vyuo VETA kuepuka na kozi ndefu  miaka minne kuwa ni kozi zinazowachosha vijana  wanaohitaji kujifunza Stadi za Kazi  ili  kuweza kujishughulisha na miradi yao .
Alisema vijana hao ni wengi ukilinganisha na uwingi na uwezo wa Vyuo vya Ufundi Stadi vilivyopo kwenye Kanda  hivyo ni vema katika  kulipatia ufumbuzi hilo lazima kuumiza vichwa kwa kauli mbiu hatutashindwa kwa pamoja tunaweza kuona tatizo hilo  linapatiwa  ufumbuzi .
“Hivyo basi, ni vyema mkaongeza na kuboresha wigo wa kutoa Mafunzo ya muda mrefu na mfupi ili kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali hususani kwa wale vijana wetu wanaohitimu Elimu ya Msingi na Sekondari”
“ Jitazame Jiulize mbona Chuo cha Ufundi Peramiho kina jina kubwa igeni ili kusambaza ubora Tanzania”
Alisema nchi zote zilizoendelea zimefanya hivyo kwakupanga kutekeleza mipango madhubuti ya uzalishajimali na Utoajihuduma.
Kuwa uzalishajimali na Utoaji huduma kiuchumi kunahitaji nguvu kazi yenye Stadi za Kazi, nguvu kazi tunayotegemea VETA iiandae na kuiingiza kwenye Soko la Kazi tayari kwa utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo.
 Kama ilivyo kwa Nchi zote Duniani zikiwemo Japan, Ujerumani zimeendelea kwa kuwatumia watu wao waliopata Stadi za Kazi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE