February 16, 2017

SERIKALI MKOA WA IRINGA YAPIGA MARUFUKU UPIKAJI POMBE ZA KIENYEJI

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akipanda  juu ya  kihenge cha  kuhifadhia mahindi  katika  kijiji cha Mawimbi Isimani Iringa kutazama akiba iliyopo kulia ni mkuu wa  mkoa Amina Masenza
Dc  Iringa  Richard Kasesela  akitazama akiba ya mahindi yaliyohifadhiwa na wananchi  wa kijiji cha Mawimbi tarafa ya Isimani
DC  Iringa  Richard Kasesela  akitazama mahindi  yalivyo nyauka kutokana na  mvua  kutonyesha katika  tarafa ya  Ismani wilaya ya  Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza (mwenye kilemba) akikagua kihenge  cha  kuhifadhia mahindi katika  kijiji  cha Mawimbi Isimani  wakati wa  ziara yake ya  kuhamasisha kilimo cha Mtama na kufanya tathimini ya chakula katika  tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa  ,wa pili kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela
RC  Iringa  Amina Masenza  akitazama mtama  unaoendelea  kunyauka katika tarafa ya Ismani  kutoka na mvua kunyesha kwa  kusua sua kulia ni mkuu wa  wilaya ya Iringa  Richard Kasesela
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliyetangulia akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela ,afisa takwim  mkoa wa Iringa Hildarda Kimaro na afisa  habari mkoa wa Iringa  Densi Gondwe wakikagua  mashamba ya mtama  kijiji cha Mawimbi tarafa ya  Isimani wilaya ya  Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza (mwenye gauni jekundu) akitazama mahindi yaliyooteshwa kwa ajili ya kutengeneza pombe ya  kienyeji aina ya komoni  katika  kijiji  cha Mawimbi tarafa ya Ismani wilaya ya  Iringa huku  akiwa amepiga marufuku matumizi ya mahindi kutengenezea pombe wengine  pichani  kulia kwake ni afisa habari mkoa  wa Iringa Denis Gondwe na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela

Na  MatukiodaimaBlog

SERIKALI Mkoa wa Iringa imepiga marufuku wananchi kutumia mahindi kutengeneza pombe ya kienyeji aina ya komboni na badala yake  kuhifadhi mahindi yaliyopo kwa ajili ya Chakula.

Agizo hili limetolewa  na mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa ziara yake  ya kukangua miradi ya elimu na uhamasishaji wa zao la mtama tarafa ya Ismani wilaya ya Iringa.

Alisema ni vema watendaji wa vijiji na Kata kuendelea kuhimiza wananchi kulima zao la mtama ila  pia kuchukua Kali kwa wananchi wanaochezea mahindi kwa kutengeneza pombe.

Kwani alisema kutokana na hali ya mvua kuonyesha kwa kusua sua  katika eneo hilo  la tarafa ya Ismani zao pekee ambalo linaweza kuwasaidia wananchi kwa Chakula ni mtama aina ya Serena .

Hivyo alisema ni wajibu wa halmashauri kwa mwaka huu kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa mbegu za muda mfupi za zao la mtama ili kila Mwananchi mbali ya kulima mazoa mengine kipaumbele cha Mkoa kuona kila kaya imelima hekari mbili za zao la mtama.

"mwaka Jana serikali iligawa mbegu za mtama kwa kila kaya ila  Matokeo yake baadhi yao wametumia mbegu hizo kutengeneza pombe na wachache wao ndio wameweza kulima"

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa mtendaji wa kijiji na Kata ama bwana shamba atakayeshindwa kusimamia vema zoezi la ugawaji mbegu na upandaji wa mashamba  mtama kila kaya hekari mbili atapaswa kujitathimini .

Pamoja na kuwataka watendaji kusimamia Kilimo cha mtama bado alishauri wakulima kuepuka kupalilia mazao yao mchana na badala yake  kupalilia kuanzia asubuhi zaidi mwisho saa  4 asubuhi ili kutoendelea kuyakausha zaidi mazao hayo kutokana na jua Kali linaloendelea kuwaka eneo hilo.

Alisema hali ya hewa si nzuri hivyo kwa ajili ya kutunza unyevu ili kuepusha mazao kuendelea kukauga lazima muda wa palili uwe asubuhi sana ama kuepuka kupalilia na jembe na badala yake  kung'oa majani kwa mikono.

Pia mkuu huyo aliwaagiza maofisi kilimo kusimamia upandaji wa mtama kuliko kuacha wananchi wanapanda kiholela kwa shina hadi shina  kuacha nafasi zaidi ya hatua tatu.

Afisa Kilimo halmashauri ya  wilaya ya Iringa Lucy Nyalu alisema kuwa halmashauri 
yake  kwa mwaka Jana imegawa mbegu  kilo 5650 kwa ajili ya wananchi wa halmashauri hiyo hasa  maeneo ambayo yana uhaba wa mvua pamoja na viazi Lishe kwa kijiji  cha Mkungugu na Malenga Makali kila kijiji kimepewa vipisi 3000 na kuwa jumla ya vijiji 21 ndio vinahitaji viazi lishe.

Alisema sababu ya vijiji vyote kutopewa  mbegu za viazi Lishe ni kutokana na uhaba wa mbegu hivyo vijiji hivyo viwili vitasaidia kuzalisha mbegu kwa ajili ya kuzisambaza maeneo mengine.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE