Fatma Salum-MAELEZO
Serikali imedhamiria kuzalisha wataalamu wa maji
wa kutosha kukidhi mahitaji ya sasa na kuwafikishia wananchi wote maji safi na
salama kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na
Mkuu wa Chuo cha Maji cha Dar es Salaam Dkt. Shija Kazumba wakati wa mkutano na
vyombo vya habari uliolenga kueleza mikakati ya chuo hicho ya kuzalisha
wataalamu wenye sifa na weledi.
“Wanafunzi waliopo sasa ni 1849, kati yao 489 ni
wanawake na dhamira yetu ni kuhakikisha
kuwa kuna mafundi sanifu wa kutosha kulingana na mahitaji ya sasa na
ukuaji wa sekta ya maji”alisisitiza Dkt. Kazumba.
Alifafanua kuwa chuo hicho kimeanzisha mfuko
maalum kwa ajili ya kuwainua wanafunzi wa kike ili wajiunge katika masomo ya
uhandisi wa maji, mafundi sanifu, upimaji wa ubora wa maji, umwagiliaji na hali
ya hewa lengo likiwa ni kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.
“Dhamira ya kuwainua wanafunzi wa kike inaonyesha
nia ya Serikali kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika kukuza na
kuendeleza sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo sekta ya maji”. Aliongeza Dkt. Kazumba
Pia alibainisha kuwa Serikali imewezesha kuwepo
kwa maabara ya kisasa kwa ajili ya kupima ubora wa maji, kupima ubora wa mita
na maabara ya kukata mabomba zote zikiwa na lengo la kuboresha hali ya
upatikanaji wa maji safi na salama.
Dkt Kazumba alitoa rai kwa Halmashuri zote nchini kuajiri
Mafundi Sanifu na Wahandisi wa Maji kwa ajili ya kuongeza tija katika sekta ya
maji.
Alifafanua kuwa Mafundi Sanifu waliohitajika kwa
kipindi cha mwaka 2013 ilikuwa ni 3000 na mwaka 2014 ilifikia 6000 na dhamira
ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mhandisi mmoja anakuwa na mafundi 5 wa kumsaidia
kutekeleza majukumu yake.
Chuo cha Maji kilianzishwa mwaka 1974 kwa lengo la
kuendeleza na kuzalisha wataalamu wa sekta ya maji kupitia mafunzo, ushauri na
tafiti mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE