February 22, 2017

RIDHIWANI KIKWETE AKANUSHA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amekanusha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Moja ya magazeti ya  wiki  yamechapisha habari inayomtaja mbunge huyo kujihuisha na bishara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Gazeti hilo limeandika kuwa, jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara.

Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa, anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. 
Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni ya uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE