February 15, 2017

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA ASUSIWA ARUSHA

Serikali ya Burundi inasema itasusia mazungumzo ya amani pamoja na upande wa upinzani, yaliyopangwa kuitishwa kesho nchini Tanzania. Mwanadiplomasia mmoja wa kiafrika ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa, anaejaribu kupatanisha katika mzozo huo, alialika kundi la wadau 33 muhimu, wakiwemo wawakilishi wa serikali na washirika wao na upande wa upinzani. Mazungumzo hayo yalipangwa kuanza kesho alkhamisi na kuendelea hadi jumamosi inayokuja katika mji wa kaskazini mwa Tanzania-Arusha. Rais huyo wa zamani wa Tanzania alidhamiria safari hii "kulizusha suala tete" kitovu cha mzozo wa Burundi ambalo ni kuhusu mhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza pamoja na uwezekano wa kuundwa serikali ya umoja wa taifa. Lakini serikali ya Burundi inaonyesha kupinga kuketi katika meza moja ya majadiliano pamoja na wawakilishi wa kundi la upinzani linalowaleta pamoja wanaharakati wanaopigania kuheshimiwa sheria pamoja na makubaliano ya Arusha-CNARED na mashirika ya kiraia.Uamuzi wa serikali ya mjini Bujumbura unazidisha makali ya mzozo wa kisiasa ulioripuka mwaka mmoja uliopita na kuangamiza maisha ya watu wasiopungua 500. Wengine zaidi ya laki tatu wameyahama maskani yao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE