February 17, 2017

QUEEN LATIPHA KUPEWA TUZO ZA HESHIM WEEKEND HII

Msanii, mwigizaji, TV na movie Producer kutoka Marekani Queen Latifah ni miongoni mwa mastaa watakaotunukiwa tuzo ya heshima za The American Black Film Festival Honors weekend hii.
Queen Latifah ambaye anawania tuzo kubwa ya The Oscars Awards mwaka huu anatarajia kupokea tuzo ya Entertainment Icon Award kwenye sherehe hizo za American Black Film Festival zitakazofanyika jijini Los Angeles, Marekani Ijumaa hii.
Akizungumzia tuzo hiyo, Queen Latifah amesema amefarijishwa sana na heshima hiyo aliyopewa na inampa nguvu ya kuendelea kufanya anachokifanya kwenye Entertainment industry.


Ukiachilia tuzo ya Oscar anayowania mwaka huu, Queen Latifah ameshawahi kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa za filamu nchini Marekani, The Emmy Awards na pia ameshawahi kushinda tuzo ya The Golden Globe.
Tuzo za The American Black Film Festival Honors zitaruka LIVE siku ya Ijumaa 22 Feb 2017 (tarehe 20 Feb. 2017 kwa nchi za Kiafrika) kupitia channel ya BET. Wasanii wengine wanaowania tuzo hizo ni pamoja na Terrence Howard maarufu kama Lucious Lyon kwenye series pendwa ya EMPIRE.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE