February 7, 2017

POLISI WANASAMBAZA DAWA ZA KULEVYA MAGEREZANI-MREMAMwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.
Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.
"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema 
Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.
"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE