February 13, 2017

PINDA AMFAGILIA RAIS DKT MAGUFULI

Mkuu  wa  chuo  kikuu  huria  cha Tanzania Mizengo Pinda  akiwa  chuo kikuu huria cha  Iringa  leo
Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa mwalimu Amina Masenza  kulia akifurahai na makamu  mkuu  wa  chuo huria  cha Tanzania leo


WAZIRI  mkuu  mstaafu  wa Tanzania  Mizengo  PInda amempongeza  rais  Dkt  John Magufuli kwa  kumteua  kuwa  mkuu wa chuo huria  cha  Tanzania na kuwa nafasi  hiyo alikuwa na usongo nayo zaidi na kuteuliwa  kwake ni jambo la  msingi na Rais hakukosea kumteua.

Akizungumza  leo katika chuo  kikuu  huria  Tanzania  Tawi  la Iringa  alisema  kuwa kuteuliwa  kwake  ni jibu sahihi  kwa  yeye  kuweza kufanya kazi hiyo kwa faida ya  watanzania katika  kuboresha  elimu kupitia chuo hicho kwa  kutoa mafunzo yenye  ubora  zaidi.

“Tangu  mheshimiwa Rais  aliponiteua  nimepata  kushiriki mahafali  mara moja  na mara yangu ya pili  itakuwa mkoani  Njombe na ipo siku mkuu wa  mkoa  wa Iringa atanialika kuja  Iringa pia ….kikubwa ni jambo moja  kuona  ubora  Wa elimu  unaohitajika  utazingatiwa  ila  kuona wanapata  elimu  bora  zaidi”

PInda  alisema kuwa Tanzania si nchi pekee ambayo inatoa elimu kwa njia ya masafa  ila zipo nchi nyingi ambazo zinatoa  elimu  kama  hii ya  njia ya masafa  ikiwemo nchi ya  China ambayo hadi sasa  inaendelea  kutoa elimu ya masafa .

Alisema  kuwa utaratibu  huo  wa  vyuo  huria  ulipoanza kazi kubwa ilionyeshwa  kufanywa  na  wakuu wa  mikoa nawilaya  ambao  walifanya jitihada  kubwa  kuhamasisha  hivyo kuwataka wananchi na  watumishi  wa umma kuendelea  kutumia  vyuo  vikuu huria  kwa  ajili ya  kupata  elimu bora.

Japo  alisema si njia  sahihi ya  watu kukimbilia vyuo  vikuu huria kwa  ajili ya  kupata  elimu kwa  njia ya  mkato kwani alisema lazimataratibu ziweze  kuzingatiwa  ili  kuwapata  wanafunzi  bora  watakaoweza  kuwa kioo katika kuifanya  elimu  kuwa bora zaidi.

“ Lazima  wanaokwenda  vyuo  vikuu huria  wawe  ni wanafunzi  wenye ubora kama  ilivyo kwa  wanafunzi wengine  waliojiunga na vyuo  vingine ….tunataka  wawe  bora  zaidi  ili kukifanya  chuo  kuwa bora kama vyuo  vingine “

Waziri Pinda  alisema lazima uongozi wa mikoa  kuangalia uwezekano  wa kuwahamasisha  watumishi  wa  umma kutumia nafasi hiyo kwa  kujiunga na vyuo  vikuu huria  ili  kuweza  kuongeza  CV  zao katika elimu na kuwa mwanafunzi  wa  kidato cha nne  mwenye  sifa ni nafasi yake  kujiunga na chuo kikuu  huria.

Aidha  alisema kuna haja  ya  kuendelea  kuhamasisha  wanawake  kuzidisha  juhudi zaidi ya   kujiendeleza katika  chuo  kikuu  huria kwani  hadi  sasa idadi yao haifurahishi  zaidi na upo  uwezekano  wa  wanawake  kuja  kulalamika  kuwa  wanahitaji uwezeshwaji  wa  asilimia hamsini kwa hamsini jambo ambalo kwa sasa lilianza  kupokea.

“ Kwa  pengo  lilivyo kwa  sasa  nilitamani kuona  wanawake ni  wengi zaidi wanajiunga na chuo kikuu huruia kuliko wanawake katika Nyanja ya udahiri  maana inanipa shata zaidi  kuona  idadi yao si  kubwa katika kujiunga na chuo  hicho”

Hata  hivyo  alisema hapendezwi  na utaratibu  wa  baadhi ya  wanafunzi  kusoma  Digrii  kwa zaidi ya  miaka sita kwa kuendelea  kubebwa na  kuwa ili  chuo  kuwa  bora  lazima  kuwe na ukomo na utaratibu wa   kusoma isiwe kusoma vile  mtu anavyojisikia .

Pia  alisema  kwa ajili ya kuboresha  elimu ya  vyuo vikuu huria  vya  Tanzania anafikiri kuna haja ya  kuwa nakompyuta mpakato  kwa ajili ya  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu ili  kuendelea  kusoma  popote  watakapo kuwepo.

 PInda ambae  amepongezwa   kwa  kuendelea  kufanya  uboreshaji  wa  vyuo huria Tanzania kwa  kutafuta  wahisani  wa  nchi  mbali mbali  ikiwemo  china kwa  ajili ya  kusaidia  chuo kikuu  huria cha Tanzania.

Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa mafanikio mbali ambayo yameendelea  kuonekana katika chuo  huria ni pamoja na ushirikiano uliopo kati ya  chuo ,wilaya ,mkoa na  Taifa .

Alisema  kuwa  ujio  wa  mkuu wa  chuo mkoa wa  Iringa kwenye tawi la Iringa iwe mwanzo  wa  kufungua milango wa  kuendelea  kutembelea  chuo  hicho kwa  lengo la  kuboresha  zaidi chuo hicho .

Mkuu  huyo  alisema serikali ya  mkoa wa Iringa  itaendelea  kuunga mkono  jitihada mbali mbali  za  chuo  kikuu  huria  cha Tanzania Tawi la  Iringa  ili  kuwawezesha  watanzania kuweza  kujiendeleza   kielimu  kupitia  chuo  hicho  cha  Iringa .
 Alisema  kuwa ziara  ya  Mizengo Pinda  katika  mkoa wa Iringa  ni  ziara  yenye  nguvu  zaidi kwa  mkoa huo kwani  alipata kuwa  kiongozi wa taifa  na mengi ameweza  kufanya katika  mkoa wa  Iringa  hivyo  ni matumaini yake kuona  mkoa wa  Iringa  kuendelea kusonga  mbele  zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE