February 8, 2017

NYOTA YA SOKA YAZIDI KUNG'ARA IRINGA PANAMA KAMA LIPULI FC

 
mchezaji  wa Panama Girls Fc  akiwatoka wachezaji wa majengo quens fc ya  Singida
Na  MATUKIODAIMABLOG 
NYOTA ya  mkoa  wa  Iringa  kisoka yazidi  kung’ara  baada ya  timu ya  Lipuli Fc  kurejea  ligi  kuu  Tanzania bara  timu ya  wanawake ya Panama  Girls Fc  imefanikiwa  kuingia hatua ya sita bora  ligi kuu ya  wanawake  kwa kuigagadua (kuifunga)  timu ya Mjengo Quens Fc  ya mkoa  wa  Singida kwa  jumla ya magoli 8-1 .

Katika  mchezo huo   uliochezwa kweye  uwanja  wa Samora  juzi ambao ni ulikuwa ni mmoja kati ya  michezo muhimu  kwa  timu  tatu zilizokuwepo zikiminyana  vikali kutafuta  timu yenye pointi nyingi  zaidi  katika  kundi A kupata  timu  itakayoingia hatua ya  sita  bora , timu ya Panama Girls Fc iliweza  kuutumia vema  uwanja  wa nyumbani wa Samora kwa  kujihakikishia kuingia hatua hiyo ya  sita bora .

Pamoja na timu ya Majengo Quens Fc  ya Singida  kuanza kuliona lango la Panama Girls Fc dakika ya 5 kipindi kwa  kwanza  bado goli  hilo halikuwavunja nguvu zaidi ya  kuwaongezea kasi  wachezaji wa Panama Girls  Fc na  kupelekea  dakika ya 7 kipindi  cha  pili  kusawazisha  goli  hilo .

Hadi  timu  hizo zinakwenda  mapumziko  kipindi  cha kwanza  timu ya Panama Girls Fc ilikuwa  ikitoka kifua mbele kwa  kuwa na magoli 3-1   dhidi ya  watani  wao Majengo Quens Fc .

Wachezaji  wa  Majengo  Quens Fc  walionekana  kuingia  uwanjani kipindi  cha pili kwa  kukata tamaa zaidi hali  iliyopelekea   Panama kutumia nafasi hiyo  kujipatia magoli ya haraka  haraka matatu  na  ndani ya dakika 20  pekee ya kipindi  cha pili  ,wakati  wakiulizana na kujaribu kujipanga baadhi ya  wachezaji wa Majengo  walianza   kucheza rafu   zaidi na kupelekea mchezaji wake mmoja kuzawadiwa kadi  nyekundu na kuzalisha  penati  iliyopelekea Panama Girls Fc  kupata magoli 7  .

Kutolewa  kwa mchezaji   huyo  kuliifanya  timu ya Majengo Quens  kuongeza  nguvu ya  kujituma  zaidi kwa  kuwabana vilivyo Panama japo  bado  ilionekana si chochote kwani   tayari Majengo Quens Fc  ilishakuwa ni  sawa  na sikio la  kufa kwa Panama Girls  Fc na badala ya  kusaidiwa  kupata tiba bado  katika  kile  kilichoonyesha  Majengo Quens Fc  na Panama ni  sawa na mbinu  na ardhi  walijikuta  wakiongezwa goli la 8 dakika ya 42 kipindi cha  pili na kuifanya Majengo Quens Fc  kuaga mashindano hayo kwa kukubali  kichapo  cha goli 8- 1

Mwalimu  wa  timu ya Panama Girls  Fc, Miraji  Fundi alisema  kuwa  mchezo  wao  uliosalia  wa kati  yao na Victoria Quens ya  Kagera utakaochezwa Kagera Februari 11  ni mchezo ambao  kwao  wanakwenda kutimiza wajibu na kama  sehemu ya bonanza  tu kwani hadi sasa  timu ya Panama Girls Fc imekwisha  ingia hatua ya  sita  bora   na wanajiandaa na  ratiba ya TFF .

Kuhusu kutwaa ubingwa wa lingi hiyo ya wanawake Taifa  alisema bado hana  uhakika kama Panama Girls Fc  inaweza  kutwaa ubingwa kwani katika lingi  hiyo  wao ndio mara ya kwanza kuingia japo alisema watakomaa kuona wanaleta  kombe la ubingwa wa  ligi ya wanawake Iringa .
 
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE