February 12, 2017

NYANGUMI 240 WAKWAMA UFUKWENI

  •      
Nyangumi waliofariki katika ufukwe wa bahari nchini New ZaalandHaki miliki ya picha AFP
Nyangumi waliofariki katika ufukwe wa bahari nchini New Zaaland
Wana mazingira nchini New Zealand, wanasema nyangumi wengine mia mbili na 40 wa aina ya "pilot", wamekwama katika ghuba ilioko mbali, kwenye kisiwa cha kusini cha New Zealand.
Kundi hilo jengine la nyangumi lilikwama kwenye ufukwe unaoitwa Farewell Spit, punde baada kundi la nyangumi mia moja kusaidiwa kurudi baharini maji yalipojaa.
Nyangumi mia tatu walikufa jana.
Eneo hilo la pwani la kilomita 20, lenye maji ya kina kifupi, ni gumu kwa nyangumi kuogelea.
Nyangumi 400 wakwama baharini New Zealand
Mamia wajitokeza kuwaokoa nyangumi waliokwama New Zealand
Indaiwa kuwa huenda nyangmi hao walisukumwa hadi ufukweni na papa baada ya alama za kung'atwa kupatikana katika mmojawapo wa nyangumi hao aliokufa.
Hathivyo haijulikani ni kwa nini nyangumi hao wanaendelea kuwasili katika ufuo huo wa kilomita 5 karibu na Golden Bay.
NyangumiHaki miliki ya picha AFP
Nyangumi
Wataalam wanasema kuwa nyangumi ambao hujipata ufukweni hutoa wito kwa wenzao ambao nao pia hujipata katika ufukwe.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE