February 17, 2017

MWANAMKE WA MIAKA 64 AJIFUNGUA MAPACHAMwanamke mwenye umri wa miaka 64 amejifungua mapacha wawili ambao ni wa kike na wa kiume katika eneo la Burgos, kaskazini mwa Uhispania.

Mama huyo alijifungua kupitia upasuaji bila matatizo yoyote katika Hospitali ya Recoletas
Taarifa zilizopo zinasema mwanamke huyo ambaye hakutajwa alifanyiwa matibabu ya uzazi nchini Marekani na ndipo alipofanikiwa kubeba ujauzito huo wa mapacha wake.

Pamoja na hilo, mwaka 2012 mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike ambaye baadaye alichukuliwa na kulewa na huduma za kijamii kwakuwa alionekana kushindwa kumlea.

Hata hivyo Mnamo mwezi Aprili 2016 mwanamke mmoja wa Kihindi aliye na umri wa miaka 70 Dajlinder Kaur , alijifungua mtoto mwenye afya katika jimbo la Haryana nchini India baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kizazi chake.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE