February 13, 2017

MSANII CHID BENZI ANA HALI MBAYA


   Na  Francis Godwin, Iringa
WAKATI  mkuu  wa  mkoa  wa Dar es Salaam Paul Makonda  akimtaka msanii wa Bongofleva  Rashid Makwilo (Chid Benzi ) kujisalimia katika  kituo  cha Polisi Dar es salaam  kwa  tuhuma  za dawa
za kulevya ,hali ya  kiafya  ya msanii  huyo si  nzuri na yupo  mkoani Iringa katika usimamizi wa  karibu wa madktari bingwa wa madawa  ya  kulevya  kupitia  kituo cha Iringa Sober House gazeti hili limeelezwa .
Mwandishi  wetu ambae  alitembelea  eneo hilo maalum ambalo anapatiwamatibabu  msanii Chid Benzi na kuzungumza na meneja  msaidizi wa  kituo hicho  cha Iringa Sober House Bw Wilibart Mzee jana  alisema  kuwa  ni kweli msanii  yupo yupo chini ya uangalizi wa karibu  wa kituo hicho baada ya hali  yake  kuwa mbaya  zaidi tofauti na alivyofikishwa  kituoni  hapo  siku ya Alhamisi Desemba 29 mwaka jana  kwa usafiri wa ndege .

Alisema  kuwa mganga  mkuu  wa  kituo  hicho ambae ni mkurugenzi wa  kituo Dkt  Ally Ngalla ambae ni bingwa wa magonjwa ya akili  baada  ya  kuona hali yake  kuwa mbaya  kwa  kusumbuliwa na matatizo ya afya ya  akili walilazimika  kumpeleka nje ya mji  wa Iringa  sehemu maalum kwa  ajili ya uangalizi wa karibu .

" wakati  akiwa hapa kituoni kwetu mjini Iringa Chid Benzi  alikuwa mkorofi hataki  kunywa dawa kwa wakati  wala kuchomwa  sindano  ....alikuwa ni mbishi na  mtata  sana na  hiyo si hali ya  kusudi ila  ilitokana na ubongo  wake  kuathiriwa  zaidi na dawa  za  kulevya  hivyo  njia  pekee ni  kumtoa hapo na kumpeleka sehemu maalum kwa uangilizi wakaribu yupo kwenye uanglizi wa karibu kwa kulazimishwa kutumia dawa na akili itakapopona ataletwa  tena hapa kituoni kuendelea na matibabu mengine na tiba ya  Saikolojia pia"

Alisema  kuwa  kimsingi  baaa ya  kutoka huko katika uangalizi wa karibu  atakakokaa kwa mwezi mmoja atarejeshwa  hapo kituoni  kuendelea na matibabu yatakayochukua muda wa  miezi sita ili  kurejea katika hali yake ya  awali .

Alisema kuwa iwapo angecheleweshwa kufikishwa kituoni hapo huenda hali yake  ingekuwa mbaya zaidi ya sasa maana dawa  hizo za  kulevya huchangia kuharibu akili  na mtumiaji huwa kama kichaa.

Bw  Mzee asema shida kubwa ya mastar wengi wanaofikishwa katika Vituo hivyo vya sober House huwa hawavumilii matibabu kwa kutaka kuendeleza ustar wao  vituoni jambo ambalo halitakiwi.

"chid  Benzi alikuwa akiendelea vema ila baadaye alianza kuingiza umaarufu wake wa usanii kwa kugoma kujitambua kuwa yupo kwa ajili ya matibabu....kifupi hata uwe maarufu sana ila unapofika hapa umaarufu wako unapaswa kuuacha nje na unaingia wewe kama wewe "

Alisema kuwa mfadhili mkuu  wa Msanii Chid Benzi ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu  Nchemba ndie aliyemfikisha kituoni hapo na muda wote anafuatilia Maendeleo take

Mzee alisema kituoni hapo wana waathirika wa dawa za kulevya 9 na wote wanaendelea vizuri japo  kuna waathirika watatu ambao walikatisha matibabu na mmoja kurejea matumizi ya dawa za kulevya na baadae alikutwa amejiua.

Kuhusu wito wa mkuu  wa Mkoa Makonda kumtaka Chid Benzi kujisalimisha Polisi ,meneja  huyo alimwomba mkuu  huyo  wa Mkoa kutambua kuwa Chid Benzi ni mgonjwa hivyo amwache apone  kwanza kwani hali yake  kiafya bado si nzuri .
mwisho
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE