February 24, 2017

MBUNGE RITTA KABATI AANZA KUSAIDIA UJENZI WA OFISI ZA CCM MATAWI YA KATA MBALI MBALI JIMBO LA IRINGA

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati ( CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi za CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa kama sehemu ya kukijenga chama hicho.

Akizungumza Leo wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya CCM .

Hata hivyo alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi kuwa na ofisi yake  ya tawi.

Alitaka wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pia shughuli nyingine za kijamii

Alisema amepata kuchangia mifuko ya saruji Tawi la Ruaha na Kigamboni wakati ofisi ya Tawi la Kitwiru Mdau wa Ccm amejitolea kujenga ofisi hiyo na kila tawi amechangia mifuko 10 ya Saruji.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE