February 17, 2017

MASOGANGE KUPANDISHWA KWA PILATO IJUMAA YA LEO


Agnes Gerald “Masogange”

KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa, Agnes Gerald maarufu Masogange na wenzake 15 wamepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya damu ili kubaini kama wanatumia dawa za kulevya.

Staa huyo wa video za wasanii wa Bongo Fleva anayetajwa kama ni miongoni mwa mastaa wanaochukua fedha nyingi kama ujira wa kucheza katika nyimbo mbalimbali za wasanii kama video queen, anahushishwa na madawa ya kulevya kwa mambo matatu ambayo atachukuliwa vipimo. ni pamoja na kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya.


“Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, “ amesema Kamishna Sirro.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE