February 20, 2017

MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MANYARA

mbul1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafa, Mama Sanka baada  ya kuwasili  kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara  mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mbul2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017.  Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia  nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa  Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mbul3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu  wakati alipotembelea moja ya darasa  la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
mbul4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama  (kulia)  wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mbul5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya  wilaya ya Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE