February 25, 2017

Kauli za Manara ni chochezi zipuuzwe, Simba inaweza kufungwa na Yanga

 

 
 
Na Eric Mkagulu
Assalaam Alleykhum ndugu zangu wapenda soka.Naamini roho zinawadunda wote wakati huu kuelekea katika pambano la watani wa jadi.Mechi hii imekuwa gumzo kila pande sii tu ya jiji bali Tanzania nzima,ni mechi inayovuta hisia hata za wale wasiopenda soka wanataka kusikia ninj kitatokea.
Tambo zimekuwa nyingi sana,huyu akimshambulia yule na yule akimshambulia huyu.Haji Manara akiiponda kambi ya Kimbiji ya Yanga huku Yanga nao wakidai Simba wanakula kwa mama ntilie,hii ni kawaida ya watani na tuwaache tu na utani wao.
Mimi sio mtani na sipendi matani lakini nikikwazwa na jambo sina budi kuliongea.Hadi sasa haieleweki ni muamuzi yupi atayechezesha mtanange wa Yanga dhidi ya Simba ni jambo jipya kwa kuwa mechi zilizopita tulimjua mapema mno.Tff wanamficha muamuzi kwa madai kwamba ni kuogopa hujuma za mechi hiyo.
Mimi nionavyo ni sawa na kwa kiasi fulani inapunguza nafasi ya hujuma.Mtamhongo nani wakati hamujui anayeenda kuchezesha mechi hiyo?Kutangaza muamuzi wa mechi hiyo mapema inajenga nafasi kubwa sana kwa muamuzi wa mchezo huu kuhujumiwa kwa kununuliwa au hujuma yoyote.
Simba wamekuwa na kilio cha muda mrefu kuhusu hujuma za waamuzi.Niliamini hili lingepunguza hofu kwao,lakini laa hasha Manara hofu imemjaa tena.Manara anataka muamuzi wamjue mapema ili wamfanye nini?Manara amesema kumficha muamuzi ni kuwajengea mazingira Yanga ya ushindi.Bado kichwa kinaniuma kwani Manara yeye anatakaje yaani yeye kila TFF wanachofanya kuhusu mechi hii ni favour kwa Yanga?
Kutotajwa kwa muamuzi kunazichinja timu zote mbili Yanga na Simba.Pengine Manara aumizwe na hili labda wana jambo lao binafsi walilotaka kumfanyia muamuzi.Mimi naamini TFF walichofanya hakiwabebi Simba hakiwabebi Yanga ila ni faida kubwa kwa sisi waumini tusiopenda hujuma.Unasemaje umechoshwa na hujuma za soka huku unasikitika muamuzi kufichwa ili asihujumiwe.
Manara hataki muamuzi bora kwa sasa,anataka muamuzi atakayeifanya Simba ishinde.Tunataka muamuzi atakayekuwa fair katika mechi hii hatutaki muamuzi anayetakwa na Manara.Na tupunguze malalamishi na uoga inawafanya mashabiki kuwa na jazba na ni kama kuwaandaa na shari.
Tayari Manara ameshaanza kuzungumzia matukio ya kuvunja viti,msemaji mwenye maadili alipaswa kuwandaa mashabiki kushuhudia mchezo huu kwa hali ya usalama na amani.Unapoanza kujenga mazingira ya kuhujumiwa hata vichwani kwa mashabiki wanaenda taifa akili zao zikiwa zimeamini kuhujumiwa.
Simba na Yanga viwango vyao msimu huu havitofautianj sana.Kwanini uaminishe watu kwamba Yanga hawawezi kuwafunga kama muamuzi akiwa fair.Unataka watu waaminj kuwa Yanga uwezo wao ni mdogo sana kuwafunga?Yanga huyu bingwa wa Tanzania na bingwa wa FA?Yanga anaweza kumfunga Simba kwa sasa sio kwa sababu ya marefa ila uwezo wao uwanjani.Mashabiki twendeni uwanjani na matokeo yote matatu yanaweza tokea kufunga,kufungwa au sare tujiandae kwa hilo.

 

 

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE