February 16, 2017

IDADI YA WATUHUMIWA WA MAUWAJIYA KIM JONG-NAM YAONGEZEKA

   Kim alishambuliwa alipokuwa anasubiri kuabiri ndege kuendaHaki miliki ya picha AP                            

Kim alishambuliwa alipokuwa anasubiri kuabiri ndege kuenda
Washukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia.
Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malaysia ambaye anakisiwa kuwa mpenzi wake wote walikamatwa leo Alhamisi.
Mwanamke mmoja maabye alikuwa na hati ya kusafiri ya Vietnam naye amekamatwa.
Kim alifariki siku ya Jumatatau kutokana na kile kinachaoimiw akuwa aliwekeka simu wakati akisubiri kuabiri ndeg mjini Kuala Lumpur.
Polisi wanasema kuwa wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wake Kim licha ya matokeo kutotangazwa
Picha hii ya CCTV imepeperushwa nchini Korea Kusini na MalaysianHaki miliki ya picha REX/Shutterstock
                    Picha hii ya CCTV imepeperushwa nchini Korea Kusini na Malaysian
Washukiwa hao wawili wa wamezuiwa rumande kwa siku saba.
Kuna uvumi unaoenea kuwa Korea Kaskazini ilihusika na mauaji hao.

Picha moja kutoka kwa kamera za usalama ambayo imepepeshwa nchini Korea Kusini na Malaysia, inaonyesha mwanamke mwenye fulana nyeupe yenye jina "LOL".
Inaaminiwa kuwa Kim alishambuliwa kwenye ukumbi wa kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege na wanawake wawili waliotumia aina fulani ya kemikali
Kim Jong-nam na ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-unHaki miliki ya picha AP
                    Kim Jong-nam na ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Leo Alhamisi Korea Kaskazini inasherehekea kile kinachotajwa kuwa miaka 75 ya kuzaliwa kwa Kim Jong-il, mareheu kiongozi wa zamani na baba wa Kim Jong-nam na Kim Jong-un.
Familia inayoongoza Korea Kaskazini

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE