February 17, 2017

HUU NI UNYAMA MKE AMCHOMA MOTO MME WAKE HADI KUMUUAMfanyakazi wa mamlaka ya mapato nchini Malawi anapigania maisha yake hospitalini baada ya kuunguzwa na moto.

Alikuwa kazini zamu ya usiku, ghafla akajisikia vibaya akaenda hospitali, baada ya tiba akaamua kwenda nyumbani.
Alipofika nyumbani akakuta gari ya nguvu imepaki, baada ya uchunguzi wa muda mfupi akagundua kuna msaliti.
Mkewe alipatwa na hofu kuu mmewe kufika bila mategemeo na kufanya fumanizi hili!

Mke akaomba msamaha lakini mme akamtaka kuondoka kwa amani. Hata hivyo mke aliomba aruhusiwe kulala na aondoke asubuhi kwani usiku huu ilikuwa hatari kwa maisha yake. Akaruhusiwa kulala chumba cha watoto. Mme aliamshwa na moto uliokaribia kumuua.

Sasa imethibitika mkewe ndiye aliyechoma nyumba akijaribu kumuua mmewe! Uchunguzi umeonyesha alienda kununua petroli akaja akawasha moto ulioua watoto wao wawili na kumuunguza vibaya mmewe!
               

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE