February 6, 2017

DC LUDEWA AANDELEA NA ZIARA YA KIKAZINa Maiko Luoga ludewa

Ni katika ziara ya siku tatu kikazi ktk kata za Mwambao wa ziwa nyasa iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh Andrea Tsere na kulazimika siku ya jana katika kijiji na kata ya lifuma wilayani Ludewa.

Kikubwa alichokifanya huko ni kutatua migogoro ya Ardhi iliyodumu kwa muda mrefu ikihusisha familia tofauti migogoro hiyo ilikuwa katika vijiji vya Nindi, Lupingu,Lifuma na Kijiji cha makonde.

Miongoni mwa migogoro hiyo ni pamoja na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka ishirini sasa baina ya familia mbili ikiwemo familia ya bw. Mussa Henjewele pamoja na familia ya Assa haule ambao ni wakazi wa Kijiji cha Nindi kata ya Lupingu iliopo mwambao mwa ziwa nyasa wilayani Ludewa.

Mgogoro huo wa Ardhi uliohusisha familia hizo mbili Kati ya Mussa Henjewele na bw. Assa Haule unadaiwa kusababishwa na familia ya bw. Mussa Henjewele ambaye alikaribishwa katika eneo la familia ya bw. Assa Haule tangu mwaka 1993 akidai ataishi hapo kwa muda ili achunge mifugo yake lakini baadae bw. Mussa akalifanya eneo hilo kuwa milki yake kinyume na makubaliano.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika kikao hicho cha usuluhishi wa mgogoro huo wakiwemo wazee baada ya kupewa nafasi ya kujieleza mbele ya mkuu wa wilaya ya Ludewa wamesema kuwa eneo hilo ni mali halali ya familia ya Bw. Assa Haule na Familia ya Bw. Mussa Henjewele iliomba kipande cha Ardhi kwa lengo la machungio ya mifugo kwa muda lakini baadae familia hiyo ya Bw. Mussa ikavamia eneo la Bw. Assa Haule zaidi ya Ekari 20 na kuzua mgogoro huo.

Hatahivyo bw. Mussa Henjewele alipoulizwa na mkuu wa wilaya ya Ludewa juu ya mgogoro huo alisema kuwa anaamini kuwa eneo hilo Ni mali yake lakini baadae akaamua kuweka wazi kuwa eneo hilo si mali yake ila yeye hana mahali pa kuishi na kuiomba familia ya Assa haule kumsaidia eneo ili aendelee kuishi hapo.

Baada ya familia hiyo ya bw. Mussa Henjewele kukiri wazi mbele ya mkuu wa wilaya ya Ludewa kuwa Nikweli eneo hilo si maliyake ndipo familia ya bw Assa Haule ikakubaliana na ombi la bw. Mussa Henjewele juu ya kumgawia kipande cha Ardhi ili aweze kuendesha maisha yake kwa masharti ya kutoingilia eneo alilokatazwa kuingia kwa mara nyingine.

Mara baada ya familia hizo mbili kukubaliana kuumaliza mgogoro huo ndipo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh Andrea Tsere Akatoa maagizo kwa wataalamu wa Ardhi kwenda kuweka mipaka ya kudumu katika eneo lililokuwa na mgogoro ikiwemo kupanda miti,kuandaa Ramani pamoja na kuandaa muhtasari wa makubaliano hayo ili hapo baadae kwa yeyote atakaekiuka makubaliano hayo aweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia Mh Tsere amehamasisha wazazi wa wanafunzi wanaoishi katika maeneo yote ya kandokando mwa ziwa nyasa kuhakikisha wanachangia chakula kwaajili ya Matumizi ya watoto wao wawapo mashuleni hiyo ni kwa wanafunzi wa shule za msingi pamoja na Sekondari.

Mh Tsere amesema kuwa Amefanya ziara katika kata nyingi wilayani Ludewa lakini ameshangazwa na wazazi wa Kata ya makonde ambao hawajaona umuhimu wa kuchangia chakula cha mchana kwa watoto wao wakidai kuwa Elimu bure hivyo amewaelimisha kisha amemwagiza mtendaji wa kata ya makonde kuhakikisha hadi siku ya Ijumaa watoto wale wa shule ya secondary makonde na shule za msingi zilizo katika Kata hiyo wanaanza Kupata chakula shuleni hapo na mzazi asiyepeleka chakula shuleni akamatwe alale Lokap hadi hapo atakapokubali kuchangia chakula ili watoto waweze kuwa bize na masomo darasani.

Baadhi ya wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wilayani Ludewa wamesema kuwa wao wanatumia chakula cha migongo hawana mahindi mkuu wa wilaya ya Ludewa amesema kuwa chakula wanachokula wao majumbani ndicho wanachotakiwa kuchangia mashuleni ili watoto wao waweze kupata chakula shuleni.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE