February 26, 2017

CCM IRINGA TUACHANE NA WALIOTUSALITI 2015 - MBUNGE KABATI

Mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa  Iringa kupitia  chama  cha mapinduzi (CCM)Ritta Kabati (kulia)  akimakabidhi jana  mwenyekiti  wa CCM Iringa mjini Aded Kiponza mifuko  10 ya  saruji kwa  ajili ya  ujenzi wa ofisi  ya tawi la Ruaha
Msanii kada  wa Chadema  aliyerejea  CCM Nyamidela akitembe  nyongo
Mbunge   Ritta kabati wa tatu  kulia wakiwa na viongozi  wengine wakimsindikiza  msanii  wa Chadema aliyejiunga CCM
Msanii  NYamidella akieleza  ubovu  wa  Chadema  kupitia  sanaa
MBUNGE  wa  viti  maalum mkoa  Wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) amewataka wanachama  wa CCM mkoani Iringa kuwa makini na wanachama  wanaotaka kuwania nafasi mbali mbali  za  uongozi wasiwe watu  wanaotafuta maslahi  yao ndani ya CCM ama kutumiwa  na  wapinzani wakati wa uchaguzi mkuu kukihujumu chama  hicho.

Kwani  alisema kupotea kwa jimbo la Iringa mjini na Halmashauri ya manispaa ya Iringa mwaka 2015 kwa chama cha  Demokrasia na maendeleo (chadema) kushinda   uchaguzi mkuu jimbo hilo ni kutokana na hujuma chafu zilizofanywa na baadhi ya viongozi na  wanachama  wa CCM kwakutanguliza maslahi yao  jambo ambalo halipaswi kujirudia.

 Akizungumza  wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za ajili matawi mbali mbali likiwemo la  Kigamboni na Ruaha mbunge
,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka 40  ya CCM ila pia kuandaa misingi mizuri ya chama  hicho  kuelekea chaguzi za chama mwaka huu na uchaguzi mkuu 2020.

“ CCM ni  chama kizuri  sana na uzuri mwenyekiti wetu Taifa  Rais Dkt John Magufuli hivi  sasa amekirejesha chama katika heshima kubwa lazima  tumuunge mkono ili kuwa na uimara  huu hadi wakati wa uchaguzi mkuu tuanze  sasa kupitia uchaguzi wetu ndani ya chama  kuwaondoa wasaliti ambao tunawajua” 

 Alisema  kuwa  kwa  upande wake ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na  huku akihimiza wanachama wa CCM kushikamana kwa  kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii

 “Ni aibu kwa CCM  kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi ni  vizuri  kuwa na ofisi zetu  kila tawi  na  kupitia  ofisi  hizo wasaliti watachujwa “

Mwenyekiti  wa CCM  Irina mjini  Abed Kiponza aliwataka
wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya  hizo  za  chama na  kuwa lengo la chama  kuona nguvu  ya pamoja  inakuwepo

“ Ni kweli tulipoteza Jimbo  na Halmashauri ya Iringa mjini  mwaka  2015 hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama
maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa mjini  kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.

Mwenyekiti   huyo  alimpongeza mbunge Kabati  kwa mchango huo wa  kuchangia ujenzi wa ofisi kuwa umelenga kuleta maendeleo katika jimbo la Iringa mjini  huku akimtaka mbunge  huyo kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.

“Kila tunakopita kuna malalamiko ya  wananchi  kunyanyasika na viongozi wa serikali za  mitaa ambao ni Chadema mfano hapa  kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE