February 22, 2017

AMNESTY WAMSHUKIA RAIS TRUMP NA VIONGOZI WAKE .....

        Amnesty inataja matamshi ya Bw Trump kama "Kampeini yenye sumu"                    Amnesty inataja matamshi ya Bw Trump kama "Kampeini yenye sumu"                

Shirika la Amnesty International limemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wengine nchini Uturuki, Hungary na Ufilipino.
Shirika hilo limesema viongozi hao wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi, kwa manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.
Katika ripoti yake ya kila mwaka, Amnesty inaelezea mwaka 2016, kama mwaka wa matamshi yaliyojaa chuki huku hofu ikapanda zaidi na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikia tangu miaka ya 1930, wakati Adolf Hitler, alipoingia uongozini nchini Ujerumani.
Amnesty inaikosoa pakubwa jamii ya kimataifa kuhusiana na namna inavyoshughulikia mzozo wa wakimbizi nchini SyriaHaki miliki ya picha AFP
Image caption Amnesty inaikosoa pakubwa jamii ya kimataifa kuhusiana na namna inavyoshughulikia mzozo wa wakimbizi nchini Syria
Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki.
Inasema mataifa mbalimbali duniani yanaendesha ajenda potovu ambayo inawahujumu wakimbizi ambao wanashutumiwa kwa makosa ambayo hawakutenda huku pia wakidhulumiwa kijumla.
Mawaziri

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE