February 22, 2017

ALIYEKUWA MKUU WA UJASUSI GAMBIA AKAMATWA

  Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh                                                                 Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh                

Maafisa wa polisi nchini Gambia wamemkamata aliyekuwa kiongozi wa kitengo cha upelelezi nchini humo ambaye anadaiwa kuongoza afisi ambayo wanaharakati wa kibinaadamu wanasema iliwatesa na kuwaua wapinzani wa Yahya Jammeh.
Yankuba Badgie alikamatwa pamoja na mfanyikazi mwengine wa zamani katika kitengo hicho siku ya Jumatatu, kulingana na msemaji wa polisi.

Bw Jammeh alibuni kitengo hicho mwaka aliochukua mamlaka kupitia mapinduzi 1994 na kupata sifa ya kuwa kitengo cha serikali kinachoogopwa zaidi, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Afisa huyo sasa ni wa kwanza wa ngazi za juu wa serikali ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh tangu kiongozi huyo aende mafichoni nchini Equitorial Guinea baada ya viongozi wa kimaeneo kupeleka majeshi yao nchini Gambia ili kumshinikiza kuondoka madarakani.

Alipoteza uchaguzi mnamo mwezi Disemba kwa rais mpya wa Gambia Adama Barroow awali alikuwa amekubali kushindwa lakini baadaye akataka kufutilia mbali matokeo hayo.(chanzo  BBC)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE