Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 28, 2017

WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

POWA
Enles Mbegalo
WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku  tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.
Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa  Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.
“Wadau  watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu
litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao,
usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana
vifungashio.

SEREKALI YA RIDHISHWA NA KASI YA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI

BOM1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akionyeshwa Picha na Rais wa Kampuni ya China National Materials Company Ltd (SINOMA),  Peng  Jianxin  ambaye Kampuni yake inatarajia kujenga kiwanda cha Cement Mkoani Tanga  mwisho kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana  Maritin Shigela , Shughuli hiyo imefanyika leo 28 February 2017 katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Ostabay Dar es salaam
Picha na Pmo
BOM2
BOM3
Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa akisoma Hotuba leo 28 February 2017 ya ufunguzi wa Mkutano kuhusu nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano Mkutano huo Umefanya  katika Ukumbi wa  Kikwete Ikulu Dar es salaamPicha na Pmo
BOM4

WAZIRI MKUU ANUSA MADUDU MINADA YA MADINI

MUH1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akifafanua jambo katika kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Februari 27, 2017, kwa ajili ya kujadili masuala ya madini. Watatu kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na  ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
MUH2
MUH5
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo katika kikao alichokiitisha kuhusu masuala ya madini kati yake na viongozi wa Serikali, viongozi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One na baadhi ya wachimbaji wadogo ,kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam jana  Februari 27, 2017. .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MUH4
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao alichokiitisha kuhusu masuala ya madini kati yake na viongozi wa Serikali, viongozi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One na baadhi ya wachimbaji wadogo,kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam jana  Februari 27, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………
*Amuagiza Kamishna wa Madini aende Mererani
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafuatilia kwa makini minada ya madini inayofanyika nchini kwa sababu anazo taarifa za kukiukwa utaratibu kwenye minada hiyo.
Amesema ukiukwaji huo unachangia kutobadilika kwa mapato ya mauzo yatokanayo na mnada hata kama kuna vito viliyokakatwa au havijakatwa.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 27, 2017) wakati akihitimisha kikao alichokiitisha kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kilichojumuisha Mawaziri wa Fedha pamoja na Nishati, Mkuu wa Mkoa wa Manyara na watendaji wake, Mbunge wa Simanjiro, wamiliki wa mgodi wa Tanzanite One, watumishi waliofukuzwa kazi na wachimbaji wadogo.
Alisema licha ya kuwa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT) kinasifiwa kwa kuongeza mapato ya madini, bado kuna kazi ya ziada inabidi ifanyike kwenye minada hiyo ili Serikali iweze kunufainika na madini hayo.
“Uzoefu wa kwenye minada ya korosho unaonyesha kuwa wanaushirika ndiyo wanaiba fedha za wakulima. Nimekuwa ninafuatilia kwa muda sasa uendeshaji wa hii minada na sijaridhishwa na uendeshaji wake. Hakuna tofauti ya bei madini ya Tanzanite yanapokuwa yamekatwa au la,” alisema.
Kwa mujibu wa wataalamu wa madini na vito, inapotokea kuna madini yamekatwa bei inapaswa kuwa juu ikilinganishwa na madini ghafi yanapouzwa moja kwa moja.
Amemuagiza Kaimu Kamishna wa Madini, Bw. Benjamini Mchwampaka (ambaye alihudhuria kikao hicho kwa niaba ya Kamishna wa Madini) aende Mererani na kufuatilia utendaji kazi wa mgodi wa Tanzanite One na suala zima la teknolojia zinazotumika kiwandani hapo.
Waziri mkuu aliitisha kikao hicho kufuatia ahadi aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mererani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara Februari 16, 2017 kwamba akimaliza ziara ya mkoa huo ataitisha kikao na wawekezaji wa Tanzanite One baada ya kupokea malalamiko kwamba hali ya watumishi ilikuwa nafuu wakati kampuni hiyo ilipokuwa inamilikiwa na wazungu kuliko ilivyo hivi sasa.
Ili kuhakikisha ukusanyaji wa mapato katika sekta ya madini unaongezeka, Waziri Mkuu amemwagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) aimarishe ukaguzi kwenye viwanja wa ndege vya Arusha na Kilimanjaro (KIA),
“Kamishna wa TRA na watu wako inabidi mjipange kwa sababu kuna njia nyingi za ukwepaji kodi zinafanyika kwenye sekta ya madini wakiwemo hata hawa wachimbaji wadogo. Simamieni utaratibu wa kufuatilia kodi, nendeni kule walipo, msisubiri waje kuwaletea malipo ofisini. Wasipokuja je? Au wakija wakakuta mmetoka ofisini je?” Alihoji Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu uelewa wa sheria miongoni mwa wachimbaji wadogo, Waziri Mkuu alisema Wizara ya Nishati na Madini kupitia kwa Kamishna wa Madini wanapaswa kutoa elimu na uelewa wa kisheria kwa wachimbaji hao ili kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye maeneo mengi nchini.
“STAMICO na Kamishna wa Madini fanyeni kazi pamoja, waelewesheni wachimbaji wadogo kuwa uwepo wa vitalu maana yake kuna mipaka ambayo pia inajumisha utoaji wa leseni kwa wenye vitalu hivyo. Kwa hiyo, waelimisheni kuwa mtu hapaswi kwenda upande wa pili wa mtu mwenye leseni, akifanya hivyo atakuwa anavunja sheria.”
“Ninyi ni wadau wakubwa wa sekta hii kwa hiyo mnapaswa kushiriki katika zoezi la kutoa elimu. Mnayo maeneo mengi ya uchimbaji lakini yana migogoro, mfano ni kule Ngaka na Kiwira. Maeneo yote haya yanahitaji usimamizi mzuri. Mnayo Bodi, Mwenyekiti yupo kwa hiyo mnatosha kuifanya kazi hii,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa mgodi wa Tanzanite One waboreshe mahusiano yao na vijiji vilivyo jirani na mgodi huo. “Kuweni karibu na wananchi ili wajue umuhimu wenu na uwepo wenu na waweze kusaidia kulinda mali zenu. Shirikianeni na Halmashauri na Baraza la Madiwani, tangazeni kazi zenu za CSR ili wananchi wajue mmechangia nini katika kusaidia maendeleo yao,” alisema.
Kuhusu suala la watumishi waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu (OWM-Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Erick Shitindi asimamie suala lao na kuwapatia majibu kuhusu hatma ya suala hilo.
Watumishi hao walikuwa wanawakilisha wenzao 201 ambao walifukuzwa kazi Februari 8, 2016 kwa sababu ya kufuatilia maslahi yao vikiwemo malipo ya saa za kazi za ziada (overtime), mishahara ya miezi miwili, malipo ya NSSF, vitendea kazi na usalama wa kazi migodini.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BODI YA TAIFA YA MAZINGIRA

1 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao kazi ambacho kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Mazingira uliyo ongozwa na Mwenyekiti wake Ali Mfuruki.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Mazingira uliyo ongozwa na Mwenyekiti wake Ali Mfuruki.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TAARIFA RASMI YA SERIKALI KUHUSU POMBE ZA VIROBA

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mamkamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali, alipozungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo.
2
Katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali,  kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Faustin Kamuzora na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira, Waziri Makamba alizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo.
Capture
Mtakumbuka tarehe 20 Februari 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa tamko la Serikali la utaratibu utakaotumika kutekeleza agizo la kusitisha utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba)kuanzia tarehe 1 Machi 2017. Utekelezaji wa katazo hili utazingatia Ibara ya 8(1) (b) na 14, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake zilizotungwa kupitia kifungu 230 (2) (f) cha sheria hiyo, na Sheria ya Leseni za Vileo Namba 28 ya mwaka 1968 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.
Napenda kusisitiza na kuujulisha umma wa Tanzania kuwa utekelezaji wa maamuzi haya ya Serikali kuhusu usitishaji uingizaji, uzalishaji, uuzaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya kufungia pombe kali utaanza rasmi tarehe 01 Machi, 2017, katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Operesheni ya kukagua utekelezaji wa agizo la serikali la usitishaji utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeshwa nchini kote kuanzia tarehe 2 Machi 2017 kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama na Kamati za Mazingira katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na Mtaa.  Kamati hizi zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na nakala Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mnamo terehe 24 Februari 2017, kiliitishwa kikao cha Mawaziri na viongozi wa taasisi za Serikali kujadili mpango wa utekelezaji wa zuio hili. Katika kikao hicho, Wizara na taasisi za Serikali zilipewa majukumu mbalimbali, kama ifuatavyo:
  1. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuzingatia umuhimu wa ujazo katika utozaji kodi, imeanzisha mfumo wa stempu za Kielektroniki ili kudhibiti ujazo wakati wa uzalishaji kwa ajili ya kupata mapato stahiki. Aidha, Mamlaka itahakikisha kwamba wazalishaji na waingizaji nchini wa malighafi ya pombe kali (ethanol) wamesajiliwa na kwamba mfumo wa ufuatiliaji wa usambazaji malighafi hiyo unawekwa. Wazalishaji na waingizaji wa malighafi hiyo watawauzia wale tu ambao wamepewa kibali na pia watatakiwa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu (3) ya kiasi cha ujazo kilichouzwa na wateja waliouziwa ambao wamesajiliwa. Uuzaji wa malighafi kwa watengezaji wa pombe kali ambao hawajasajiliwa itakuwa ni kosa la jinai kulingana na Sheria.
  1. Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye msajili wa kemikali za viwandani na majumbani, atasajili makampuni na taasisi zinazoingiza kemikali za viwandani na majumbani nchini ikiwa ni pamoja na Ethanol. Msajili atawajibika kutoa taarifa sahihi za majina ya makampuni na watu binafsi na taasisi zinazohusika, kiasi kilichoingizwa na kimetumika, pamoja na madhumuni ya matumizi.
  1. Kulingana na sheria ya Leseni ya Vileo Na 28 ya Mwaka 1968 na marekebisho yake ya mwaka 2012, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika operesheni hii itaratibu zoezi hili katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa yote Tanzania bara kwa kuhakikisha kuwa wanaofanya biashara ya pombe ya kawaida na pombe kali (spirit) na watumiaji kinyume na masharti ya leseni za vileo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika operesheni hii watakukagua viwanda vyote vinavyojihusisha na uzalishaji wa vileo na vifungashio vya aina mbalimbali vya kufungia pombe kali kama vimekidhi viwango vya kitaifa Ukaguzi katika viwanda vya plastiki utachunguza kama kuna mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kwa ajili ya pombe kali. Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kama haitumiki kwa kuzalisha bidhaa zingine katika kiwanda husika, mwenye kiwanda atalazimika kutoa ufafanuzi wa hatima ya mitambo hiyo. Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki itakayokutwa inaendelea kuzalisha pombe kali na kufungashia vifungashio vya plastiki itakamatwa na kutaifishwa na wahusika watashtakiwa.
  1. Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee, kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na mabwana afya katika operesheni hii watatoa elimu kwa umma na kukagua maeneo yote yanayotumika kuhifadhia, kuuza na kusambaza vileo vya aina zote, na kushiriki kukamata vileo ambavyo vipo kinyume cha sheria na kanuni.
  1. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Idara ya Habari Maelezo, itasaidia kutoa elimu kwa umma kuhusu suala hili.
  1. Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Jeshi la Polisi, na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, itashiriki katika operesheni, ikiwemo kwenye masuala ya inteligensia.
  1. Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, wataratibu operesheni.
Kama tangazo letu la tarehe 20/2/2017 lilivyoonesha muda wa nyongeza unaweza kutolewa kwa wazalishaji halali ambao wataonyesha ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, na kwamba watahitaji muda mchache kufanya hivyo, na ambao watatimiza masharti kadhaa na kupata kibali maalum kabla ya tarehe 28/2/2017. Hadi sasa Serikali imepokea maombi ya wazalishaji 9. Tutangaza kesho iwapo kuna ambao wamekidhi masharti au la. Kanuni za upigaji marufuku pombe hizi zipo tayari.
Pia tumepokea malalamiko kwa wazalishaji wengi kwamba zoezi hili limekuja ghafla na wengine wana malighafi na bidhaa kwenye maghala. Ukweli ni kwamba Serikali ilitoa taarifa Bungeni, kuanzia mwezi Mei 2016, na mara kadhaa baada ya hapo, na rekodi zipo, kuhusu hatua hizi. Vilevile, taarifa ya Serikali iliyotangaza kupiga marufuku pombe za viroba ziliripotiwa kwa ukubwa stahiki kwenye vyombo vya habari, ikiwemo kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, mwezi Agosti 2016. Katika taarifa zote za nyuma, Serikali ilitangaza kwamba hatua hiyo itaanza tarehe 1 Januari 2017. Hatua hizi zimechelewa kwa miezi miwili. Iwapo, baada ya taarifa hizo za Serikali, kuna mzalishaji ameagiza malighafi au kutengeneza au kuhifadhi pombe za viroba, au kuchukua mkopo kwa ajili hiyo, atakuwa amefanya hivyo akijua madhara yake.
Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa  zoezi hili la upigaji marufuku matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili wale wanaozalisha na kuuza au kuhifadhi waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watakaokiuka zuio hili.
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
28/02/2017

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. 

Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi. 

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Prosper Kwigize akizungumza na viongozi wa vyombo vya habari jamii wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
     
 Kutoka kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.

MKANGANYIKO MWINGINE WENYE UTATA KWENYE WIZARA YA ELIMU


Tume ya Vyuo Vikuu  Tanzania ( TCU) imetoa ufafanuzi   kuhusu  wanafunzi 8,357 waliotajwa  kuwa hawana sifa stahiki  za kuendelea na elimu ya juu na kudai kwamba kulikuwa na dosari katika taarifa zao.

Taarifa kutoka  TCU  kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana  moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa hiyo imesema  wanafunzi wote walioorodhesha  katika taarifa iliyotolotewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea  na masomo yao ya kawaida.
“TCU inapenda kuuarifu umma  kuwa ,uhakiki wa ubora  wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa kifungu 5(1)(b)c) cha Sheria ya Vyuo vikuu Sura ya 346 YA Sheria za Tanzania,’’imesema taarifa hiyo.
SERIKALI YAISHUKURU AfDB KUKUBALI KUFADHILI MIRADI YA UJENZI WA BARABARA NA USAFIRISHAJI WA UMEME ILI KUFUNGUA KANDA YA MAGHARIBI

dot2
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM)
dot1
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam. 
dot3
Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
dot4
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
dot5
Mmoja wa Wakurugenzi anayeiwakilisha nchi yake katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) akipongeza juhudi za Serikali katika kuwataulia wananchi wake matatizo ya kiuchumi wakati wa Mkutano kati ya Wakurugenzi hao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) jijini Dar es salaam.
dot6
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia)  katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
dot7
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
dot8
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa AfDB, Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe, kutoka Afrika Kusini (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wengine wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya AfDB baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
dot9
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa Mkutano kuhusu Hali ya uchumi nchini Tanzania katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi.
Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.
Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.
Pia mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya  ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.
“Katika kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya  ukuaji wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.
Aidha amewaeleza wageni juu ya jitihada za Serikali ya Mhe. Dkt. John  Pombe Joseph Magufuli za kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupambana na rushwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Waziri Mpango ametumia fursa hiyo kuomba AfDB kusaidia kujenga uwezo wa Tanzania kukabiliana na majanga yakiwemo ya matetemeko ya ardhi, ajali kubwa za majini na kwenye migodi. Maeneo mengine ambayo AfDB imeombwa kuisaidia Tanzania ni uvunaji wa rasilimali za bahari (blue economy), kuelekeza mitaji katika Sekta ya kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi.
Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameipongeza Benki ya AfDB kwa kuwa mdau mkubwa wa Maendeleo ya nchi za Afrika na hasa Tanzania kwa kuwa imekuwa mnufaika mkubwa wa program/ miradi inayofadhiliwa na  Benki hiyo.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wageni hao watakapokuwa wakitembelea miradi mbalimbali inayogharamiwa na AfDBi katika siku takribani tano ambazo watakuwepo nchini
Kwa upande wa Wakurugenzi Watendaji wa AfDB wanaoziwakilisha nchi zao, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio ya kiuchumi kwa kuwa Tanzania imekuwa na viashiria vingi ambavyo vinaonesha uchumi wa Taifa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Aidha wameitaka Tanzania kuendeleza jitihada za kupambana na Umaskini hasa katika maeneo ya vijijini na kuongeza fursa za ajira ili kuharakisha maendeleo. Pia wameipongeza Serikali kwa mikakati waliyonayo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa  miaka mitano kwa kuwa unaendana na vipaumbele vya Benki hiyo.
Benki hiyo imeitaka pia Tanzania kushiriki na kuchangamkia fursa za miradi ya kikanda hasa katika Nishati ya Umeme, Barabara na Reli na pia kuhakikisha utawala bora.

MTOTO LATIFA ALIYEIBIWA SAA 2 ASUBUHI IRINGA MJINI APATIKANA USIKU KIJIJI CHA MKUNGUGU

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa amembeba mtoto huyo.
Leo mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.
 
Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema ” nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toak asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona” .
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini.
 
Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtot huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto. Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala.
 
Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla “pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu” alisisitiza
 
Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi. Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3.