January 25, 2017

MAAJABU AU MAUZA UZA CHUI WA AJABU AZUA TAHARUKI KUBWA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA


Na MatukiodaimaBlog
AMA kweli  ukistaajabu  ya  musa utayaona ya  filiahuni kwa mara ya kwanza  chui  wa  ajabu azua taharuki   kubwa  kwa  wagonjwa na wauguzi  katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  baada  ya  kuibuka mnyama huyo aina ya  chui  katika mazingira  ya  tatanisha  .

Akizungumzia   mtandao wa matukiodaimaBlog juu ya tukio  hilo muunguzi  mfawidhi  wa Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  Rustica Tung’ombe  alisema  kuwa  tukio   hilo  limetokea  majira  ya saa 7 na  saa 8  usiku  wa  kuamkia leo jumatano  na  kuwa  chui  huyu  alionekana  nje  eneo la wodi namba 6 .

Alisema  kuwa   kwa taarifa  ambazo  zimeripotiwa na muuguzi  msimamizi  wa  zamu  usiku   kuwa  wanawake  ambao  walikuwa  wakitoka  kunyonyesha  watoto  wao  wodini   waliweza  kukimbia  huku  wakipiga kelele za  kuomba msaada baada ya  kukutana na  chui  huyo .

“ Kulikuwa na kundi  la kwanza la  akina  mama waliotoka  kunyonyesha  watoto  wao  lilipita eneo hilo na  kundi la pili lilifuata  na mwanamke mmoja kati yao  alikuwa nyuma akifuata  wenzake na  ndipo  alipomshuhudia  chui  huyo na  kuanza  kupiga  kelele ……wauguzi  walipochungulia madirishani walipata  uhakika  kuwa mnyama   huyo ni chui “ alisema

Kutokana na kuwa na uhakika  juu ya mnyanya  huyo  kuwa  ni chui walilazimika  kuomba msaada kwa askari magereza  ambao   wamepakana na hospitali hiyo  kwa ajili ya  kutoa msaada .

Alisema  baada ya  kufika  askari magereza  pamoja na  kundi kubwa la  wananchi kwa  ajili ya  kupambana na chui   huyo ghafla  mbwa  aliibuka nyuma ya  chui  huyo na  kuanza  kumfukuza chui  huyo ambaye  aliruka  ukuta wa uzio na   kutoweka kusikojulikana.

“ Wakati askari  magereza  wanajiandaa  kupambana na  chui  huyo  alitokea  mbwa ambaye  kweli hatujui  alitokea  wapi na kuanza  kumfuatilia  chui   huyo ….. hili ni  tukio la aina yake  na halijapata  kutokea katika Hospitali  hii maana  hapa  ni mjini na hatujui chui  huyu kafikaje hapa”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE