January 24, 2017

AJALI YA BASI LA VITU LAINI NA LORI YAUA MMOJA IRINGA

MTU mmoja amethibitika kupoteza maisha katika ajali ya basi la Vitu Laini lenye namba za usajili T910 linalofanya safari zake kati ya Lulanzi Kilolo na Iringa baada ya kuligonga lori lenye namba T724 AVV scania lililobeba Mbao

Ajali hiyo imetokea asubuhi hii eneo la Tagamenda Mjini Iringa wakati basi hilo likitoka Kilolo kuja mjini Iringa sanjari na mwelekeo wa Lori hilo 

Chanzo kimeelezwa ni mwendo kasi wa basi hilo na kutokuwa makini katika kona 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amefika eneo La tukio pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama amethibitisha hilo0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE