Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

January 31, 2017

MAJESHI YA SENEGALI YAMKAMATA KAMANDA WA RAIS KING'ANG'ANIZI JAMMEH WA GAMBIA


Yahya Jammeh
Yahya Jammeh

Vikosi vya nchi za Afrika Magharibi vimemkamata kamanda mmoja wa cheo cha juu nchini Gambia, na kupata silaha kweye makao ya kibinafsi ya rais wa zamani aliye uhamishoni Yahya Jammeh.

Jenerali Bora Colley, mkuu wa kikosi maalum alikamatwa katika nchi jirani ya Senegal.


Vikosi vya kikanda pia vimevamia nyumba ya bwana Jammeh iliyo kijiji mwao eneo la Kanilai na kupata silaha.
Jenerai Colley alikuwa kamanda wa zamani wa kambi ya jeshi ya Kanilai ambapo Jammeh alikuwa na mpango wa kahamia akistaafu, kabla ya kulazimishwa kukimbilia uhamishoni kwa kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa Disemba mosi mwaka 2016.


Walinzi wanne wa mke wa Jammeh, Zainab, pia nao walikamatwa kwenye mji wa mpaka wa Karang nchini Senegal.


Vikosi vya kikada vimekuwa vikimsadia Raia Adama Barrow kuchukua hatamu za uongozi, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi tangu bwana Jammeh akimbilie uhamishoni zaidi ya wiki moja iliyopita.

RAIS TRUMP AMFUTA KAZI KAIMU MWANASHERIA MKUU MAREKANI

Donald Trump amfuta kazi mwanasheria mkuu

  • 31 Januari 2017
                    Kaimu mwanasheria mkuu wa Marekani Sally Yates
Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.

Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.


Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.


Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.


Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.


Taarifa hiyo ya ikulu imesema kuwa bi Yates ni dhaifu kuhusu mipaka na dhaifu zaidi katika maswala ya uhamiaji


Hatahivyo wanachama wa Democrat walipuuzilia mbali kufutwa kwake.
Seneta Chuck Schumer ,kiongozi wa chama alisema katika taarifa kwamba mwanasheria mkuu anafaa kuwa mtiifu kwa sheria na sio ikulu ya Whitehouse.

RUFAA YA MSHITAKIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI YAVUTIWA SUBIRA ......


Image result for Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi
NA MATUKIODAIMABLOG
RUFAA  ya askari  kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon   aliyehukumiwa   kufungwa  jela miaka 15 na mahakama  kuu kanda ya Iringa mwaka jana  kwa kuhusika na mauwaji ya bila kukusudia dhidi ya mwanahabari  wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi bado haijulikani siku ya  kuanza kusikilizwa .

Akizungumza  na   mwandishi wa MatukiodaimaBlog aliyefika mahakamani  hapo  leo kufuatilia rufaa hiyo ,Naibu msajili wa mahakama kuu ya Tanzania Iringa   Agatha Chugulu  alithibitisha  mahakama   hiyo kupokea  rufaa iliyowasilishwa na wakili Lwezaula Kaijage ambae ndie alikuwa akimtetea askari Simon na  kuwa  tayari rufaa hiyo ilitumwa mahakama kuu  .

" Rufaa  zote  zilizotufikia  zimeandaliwa na zilishatumwa  mahakama  kuu ila  lini zitapangwa  kusikilizwa  hilo  lipo  juu ya uwezo  wangu ni  hadi hapo  vikao husika vya rufaa mahakama kuu zitakapopanga  na sisi  tutaletewa barua kwa ajili ya  kuwajulisha  wahusika....  bado hawajapata taarifa ya  lini  rufaa zitawafikia " alisema naibu msajili  huyo 

Mshitakiwa   huyo  alikata  rufaa ya kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Iringa chini ya jaji Dk Paulo Kiwelo
Rufaa hiyo ilikatwa  Julay 29 mwaka jana siku mbili toka ilipotolewa hukumu hiyo na wakili wake wa utetezi , Lwezaula Kaijage ambaye siku ilipotolewa hukumu hiyo alisema ni mapema mno kuzungumzia hatua atakayochukua baada ya hukumu hiyo.
“Kesi siyo ya kwangu ni ya mshtakiwa, mimi nilikuwa na mtetea tu, nikishapata hukumu itabidi nikutane naye, nisikie maoni yake, niangalie sheria, mwenendo wa shauri, niangalie ni kitu gani ambacho mahakama ilijielekeza vibaya katika kufiakia uamuzi huo na kama itaonekana kipo tutaangalia hatua za kuchukua,”

Mwanahabari  Mwangosi  aliuwawa mwaka  2012  katika  kijiji  cha  Nyololo  wilaya ya  Mufindi  mkoani Iringa  wakati  polisi  wakipambana na  wafuasi wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema)  waliokuwa  wakikaidi  amri ya  kusitisha  zoezi la uzinduzi  wa matawi ya  chama  hicho kwa  ajili ya  kupisha  shughuli  za senza  ya  watu na makazi kuendelea kwa  muda  uliokuwa  umeongezwa .

MWISHO

BILIONI 2,570.1 ZALIPA MADENI NJE YA NCHI

index 
Na;  Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2016 hadi kufikia Desemba, 2016 Serikali imetumia jumla ya shilingi Bil. 2,570.1 kulipia madeni ya ndani na nje yaliyoiva.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango aliyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi wa Taifa.
“Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2016 hadi kufikia Desemba, 2016 Serikali ilitumia jumla ya shilingi Bil. 2,570.1 kulipia madeni ya ndani na nje yaliyoiva. Kati ya kiasi hicho malipo ya deni la ndani ni shilingi Bil. 1,822.3 na deni la nje ni shilingi Bil. 747.8 ,” alifafanua Dkt. Mpango.
Ameeleza kuwa katika malipo ya deni la ndani yanajumuisha malipo ya mtaji (rollover) ya shilingi Bil. 1,367.1 na malipo ya riba ya shilingi Bil. 455.2.
Aidha Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kupeleka fedha katika Halmashauri  kwa kuwa ndiko utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi yanapofanyika.
Hivyo basi, katika robo ya kwanza ya mwaka 2016/2017, Serikali ilipeleka jumla ya shilingi Bil. 114.7  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi mengineyo katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Aidha, katika robo ya pili ya mwaka, Serikali iliongeza mgao wa fedha zilizoenda kwenye Halmashauri ambapo kiasi cha shilingi bilioni 203.4 zilipelekwa.
Dkt. Mpango alitaja madai mengine yaliyolipwa na Serikali katika kipindi cha kufikia Juni 30, 2016 kuwa ni kiasi cha Shilingi Bil. 3,113.7 ambazo ziliwasilishwa ikiwa ni madai ya wakandarasi, watumishi, wazabuni na watoa huduma mbalimbali.
Serikali ilifanya uhakiki kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali ilibainika kuwa madai halali yalikuwa shilingi Bil. 2,934.2 na madai yaliyokosa vielelezo na hivyo kukosa uhalalli yalikuwa shilingi Bil. 179.5.
Vile vile katika kipindi cha nusu mwaka wa 2016/17, Serikali imelipa jumla ya shilingi Bil. 600.2 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi Bil. 42.35 zilikuwa kwa ajili ya madai ya watumishi, shilingi Bil. 49.46 kwa ajili ya wazabuni, shilingi Bil. 11.2 kwa ajili ya watoa huduma, shilingi Bil. 30.0 kwa ajili ya madai ya vyombo vya Ulinzi na Usalama, shilingi bil. 67.2 kwa ajili ya wakandarasi mbalimbali ikijumuisha shilingi Bil. 2.0 kwa ajili ya makandarasi wa maghala na skimu za maji.

CUF YA PROFESA LIPUMBA YAJIBU MAPIGO KUHUSU RUZUKU WALIYOPEWA NA HAZINA

 
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam leo kuhusu ruzuku ya chama hicho iliyopokelewa kupitia akaunti namba 2072300456 ya Benki ya NMB Tawi la Temeke. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar na Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud.
Meza Kuu. Kutoka kulia ni Kamanda Mkuu, Athumani Hamadi,Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima, Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Masha Amour.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.

TAARIFA KWA UMMA 
 
The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) chini ya Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kinaishukuru na kuipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kukipatia Chama chetu Ruzuku yake inayopatikana kwa Mujibu wa Sheria ya vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992.
 
Pamoja na Ruzuku ya CUF kuzuiwa kwa Muda wa miezi mine (4) kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi Desemba 2016 kutokana na sintofahamu ya uongozi wa Kitaifa wa CUF, Msajili hakuona haja ya kuendelea kuizuia wakati shughuli za chama zinafanyika kila siku. Kuendelea kuizuia Ruzuku halali ya chama ni kukizuia kufanya kazi zake halali za kisiasa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika chaguzi mbali mbali za kiserikali zinazoendelea nchini. 
 
Waheshimiwa wanahabari, Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia katiba ya CUF ya mwaka 1992, Toleo la 2014 alijiridhisha kuwa Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ndiye Mwenyekiti halali wa CUF kwa kuwa mchakato wa kukamilisha kujiuzulu kwake haukukamilika kabla yeye kutengua barua yake ya kujiuzulu.
 
Mnamo Tarehe 23 Septemba 2016 , Msajili aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa CUF kumjulisha msimamo na mwongozo wa wake  kuwa  “Mwenyekiti wa Taifa wa CUF ni  Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba”
 
Baada ya Katibu Mkuu kupokea barua hiyo aliamua kupinga Uamuzi huo wa Msajili wa Vyama vya Siasa uliotokana na Malalamiko ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wapatao 324 kati ya 343 ambao walilalamikia uvunjifu wa Katiba ya CUF unaofanywa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
 
Maaalim Seif na timu yake walienda mbali kwa “kuikimbia ofisi yake” iliyoko hapa Ofisi Kuu ya CUF Buguruni na kukimbilia Mafichoni kusikojulikana na kusababisha kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kiutendaji.  Hivyo, Mwenyekiti wa Taifa aliamua kufanya mabadiliko ya Kurugenzi za Chama kwa kumujibu wa ibara ya 91(1)(f) ya katiba ya CUF, nainukuu:
 
“Mwenyekiti wa Taifa atateua kutoka miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa au wanachama wajasiri kuwa wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wa Chama pamoja Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti na kufikisha uteuzi huo mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa kuthibitishwa”. 
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 95(3) ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992, Toleo la 2014, Nainukuu:-
  “Naibu Katibu Mkuuatakayemfuatia Katibu Mkuu kwa madaraka ni Yule anayetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anotoka Katibu Mkuu”.  Kwa kifungu hicho, Katibu Mkuu anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu yoyote ile, Naibu Katibu Mkuu Bara ndiye anakaimu Ukatibu Mkuu mpaka atakaporejea ofisini kuendelea na majukumu yake.
 
Hii inatokana ukweli wa kikatiba uliowekwa kwenye ibara ya 105 (1) ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992, Toleo la 2014, Nainukuu:-
  
 “Pale ambapo mwanachama yeyote wa Chama mwenye madaraka kwa mujibu wa masharti ya katiba hii, kwa sababu yeyote ile, hawezi kutekeleza kazi zake kwa muda, mwanachama anayemfuata kwa madaraka kwa mujibu wa katiba atakaimu nafasi yake”. 
 
Hivyo, kwa mujibu wa ibara hii na ile ya 95(3) Ni suala la kikatiba lisilo na shaka kwa Mheshimiwa Magdalena Sakaya (Mb) ambaye ndiye anayemfuata Katibu Mkuu kwa Madaraka kukaimu ofisi ya Katibu Mkuu mpaka atakaporejea ofisini kwake Buguruni. Kwa hiyo, Mhe Sakaya ataendelea kufanya majukumu yote ya Katibu Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CUF. Na Katibu Mkuu hapaswi kulalamika.
 
Kuhusu masuala ya fedha, Kwa mujibu wa kanuni ya jfedha ya mwaka 2014, ibara ya 22(2)(a) (B):-“Masuala yote ya fedha yanasimamiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi na ndiye Mshauri Mkuu wa Katibu Mkuu kuhusu Masuala ya Fedha”. 
 
Na kwa kuwa Katibu Mkuu ni Ofisi siyo mtu, anapokuwa hayupo ofisini Naibu Katibu Mkuu Bara atatekeleza majukumu yote ya ofisi ya Katibu Mkuu kama Kaimu Katibu Mkuu.  Ni aibu kwa Mwalimu Seif kulalamika wakati anaijua katiba ya CUF na anajua kuwa amekimbia ofisi mwenyewe ndiyo maana Mhe Sakaya anafanya kazi alizozikimbia kwa kushirikiana na wakurugenzi walioteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa mujibu wa Katiba.
 
Waheshimiwa wanahabari, Chama Chetu kimepokea sehemu ya malimbikizo ya ruzuku ya CUF Kiasi cha Tsh. 369,366,671/=. Tumepokea Ruzuku hiyo kupitia Akaunti namba 2072300456 ya The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi)  NMB Tawi la Temeke. Hii siyo akaunti Mpya ya Chama kama inavyodaiwa Maalimu Seif na genge lake.
 
Akaunti hii ilifunguliwa zaidi ya miaka Kumi iliyopita na Katibu Mkuu kwa ajili ya kupokea na kutoa fedha za CUF kwa wilaya ya Temeke. Na kwa mujibu wa Kanuni ya Fedha ya CUF ya mwaka 2014, ibara ya 23(1)(f) Nainukuu: –
  
“Chama ngazi ya Taifa kinaweza kufungua akaunti tofauti au kubadili matumizi ya akaunti iliyopo kwa ajili ya kazi au shughuli maalum kadri itakavyoona inafaa. Akaunti hizo zilizofunguliwa utawekwa utaratibu maalum wa kuzihudumia”.
 
Kwa kuzingatia hali iliyopo, Tuliona kubadilisha matumizi ya Akaunti ya The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), Tawi la Temeke itumike kupokelea Ruzuku ya Chama toka serikalini ili iweze kufikia katika mikono salama kwa ajili ya uendeshaji wa Shughuli za Chama.
 
Waheshimiwa wandishi, Baada ya kuipokea Ruzuku hiyo, tayari tumeshaitumia katika harakati za Kiuchaguzi katika Chaguzi za marudio ya Udiwani katika kata 14 ambapo CUF imefanya vizuri sana katika kata tatu (3) ambazo ni Nkome (Geita), Malya (Kwimba) na Kijichi (Temeke). 
 
Waheshimiwa wandishi, Ikumbukwe kuwa Tangu  Mwalimu Seif na Genge lake wakimbie Ofisi Kuu Buguruni Tarehe 23 Septemba 2016, shughuli za chama zilikuwa zikiendelea kufanyika japokuwa hatukuwa tunapata ruzuku toka Serikalini. Wanachama wetu walikuwa na ari zaidi ya kukichangia chama ili kuendeleza harakati za ukobozi wa Haki sawa kwa Wote. Kwa mapenzi makubwa ya Chama chake Mheshimiwa Mwenyekiti wetu Profesa Ibrahim Haruna Lipumba alikuwa Msitari wa mbele kukisaidia chama kwa kujitolea na hata kukikopesha chama ili tutekeleze Majukumu ya ujenzi wa chama.
 
Waheshimiwa wanahabari, Hii si mara ya kwanza Mhe Profesa kukisaidia chama Chetu. Ipo mikataba kadhaa ambayo Mwenyekiti wetu amewahi kukikopesha chama fedha zake mwenyewe.
 
Waheshimiwa wandishi, Ni jambo la kusikitisha kuwa kwa takribani mwaka mmoja hasa baada ya Mhe Profesa Lipumba kuwa nje ya uenyekiti wa Taifa wa CUF, Wilaya zote za Tanzania Bara zilisitishiwa Ruzuku toka Ofisi kuu wakati wilaya zote za Zanzibar zikiwa zinaendelea kupokea ruzuku. Kwa kweli huu ni uonevu mkubwa kwa wanaCUF wa Tanzania Bara na huu ni mpango wa Makusudi wa Maalim Seif na genge lake.
 
Baada ya kupokea Ruzuku hiyo, Tumeamua kuzipelekea ruzuku Wilaya zote za Tanzania Bara alau ruzuku ya miezi mitatu mitatu kwa kila wilaya. Mpaka sasa tumeshatuma ruzuku katika wilaya 82 ambapo Tsh. 66,300,000/= zimetumika. 
 
Ikumbukwe kuwa Wilaya zinazotakiwa kupokea ruzuku ni wilaya zote zilizofanya uchaguzi wa ndani ya Chama ambapo Jumla ya wilaya 104 zina uongozi halali wa chama. Kwa mantiki hiyo, wilaya 22 bado hazijapewa Ruzuku kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo Akaunti zao kuwa dormat kwa muda mrefu, na nyingine kutowasilisha akaunti namba zao ofisini. 
 
Hivyo, tunatoa wito kwa viongozi wa Wilaya zote wa CUF kwenda benki kuangalia taarifa ya fedha ya akaunti zao kisha kutupa taarifa. Lakini pia ni wajibu wao kufanya matumizi ya fedha hizo kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni ya Fedha za CUF kwa kuwa hizo ni fedha za umma.
 
Waheshimiwa wandishi, tumesikitishwa na tamko la inayojiita Bodi ya wadhamini ya CUF eti fedha zimeibwa na wanazuia viongozi wa wilaya wasichukue fedha zilizoko kwenye akaunti zao. Kwa mujibu wa ibara ya 98(1) nainukuu:- 
 
“ Kutakuwa na Bodi ya wadhamini itakayoteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kipindi cha miaka mitano (5) na mjumbe anaweza kuteuliwa tena baada ya muda kumalizika”. 
 
Ndugu wandishi, Bodi ya CUF iliteuliwa kwa mara ya mwisho Januari 2010, hivyo ilimaliza muda wake Januari 2015.  Haijawahi kuteuliwa tena na haijawahi kulipiwa Mchango wa kila mwaka RITA tangu 2013. Kutokana, sheria za nchi na katiba ya CUF, Bodi hiyo ni mfu kwa hiyo haina uwezo wa kushughulikia na kusimamia masuala yoyote ya fedha za CUF. How can a dead body talk about financial matters?. 
 
Wakiwa wanajua ukweli huo, bado wanakubali kutumika kwa maslahi ya Maalim Seif. Hii ni kuthibitisha kuwa “Mbwa mzee hafundishwi mbinu mpya za kuwinda”. Ni kweli Maalim Seif, Bashange na Katau wamezeeka, ni sawa mbwa wazee wasioweza kutumia mbinu mpya za kujijenga kwa wanachama wa CUF bali wanazidi kujifedhehesha. 
 
Ndevu zao ni ishara ya kupitwa na wakati. Ni bora watuachie vijana tujitanabahishe kwa mbinu za kisasa za kuiweka kweli ndani ya CUF na Watanzania kwa ujumla. Kama Maalim Seif alikuwa simba wa vita vya miaka 1980, kamwe hawezi kuwa simba wa vita ya 2016/2017. Huwezi kuwa Katibu Mkuu ambaye unapeleka Ruzuku Zanzibar kupitia Michango ya Wabunge lakini ukawa hutaki Wilaya za Tanzania Bara zipate Ruzuku. Huu ni ubaguzi uliokithiri na sisi hatutaukubali.
 
Tunaiomba ofisi ya Gavana wa Benki kuu kutupilia mbali ombi la Bodi ya wadhamini ya CUF isiyo halali kwa kuwa imepitwa na wakati na inakiuka hata katiba ya CUF ibara ya 98(1) na (2) inayotaka bodi iundwe na jumla ya wajumbe 9 ambapo 3 kati yao lazima wawe wanawake lakini bodi feki ya Mwalimu Seif ina wanaume watupu ndiyo maana wanailalamikia RITA eti wametoa siri za ufeki wao. 
 
Na kama wanahisi RITA wameghushi nyaraka, waende Polisi wakafungue mashitaka dhidi ya RITA, japokuwa nalo ni jambo gumu kwao maana wao ni Bodi mfu, hawana uwezo wa kushitaki wala kushitakiwa.
 
Waheshimiwa wanahabari, kwa sasa Maalim Seif anamlaumu kila mtu. Anamlaumu Jaji Mutungi kwa kusema ukweli, anawalaumu Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kuupinga udikiteta wake Mkutanoni, anamlaumu Gavana wa Benki, anailaumu RITA, anamlaumu Jaji Kihiyo, anamlaumu Rais Shein, anamlaumu Jecha, anamlaumu Profesa Lipumba eti anakuja kuzuia asipewe urais wa Zanzibar lakini cha ajabu hajilaumu mwenyewe kwa udikiteta wake ndani ya CUF na tamaa yake ya kupenda fedha za Lowasa kuliko utu na thamani yake kwa jamii.
 
Mwisho, tunamtaka Mwalimu Seif na Genge lake waende kwa amani watuachie CUF yetu. Hata Mapalala ailianzisha CUF lakini alipoonekana anaisaliti aliamua kuiacha CUF kwenye mikono salama. “Yeye sasa ni Simba mzee hawezi mawindo ya wakati huu”.
 
Imeandaliwa na;-
Thomas D.C Malima
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa)

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MARAIS MBALIMBALI ETHIOPIA

 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
  Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. 

PICHA NA IKULU

MKWASA KATIBU MKUU MPYA WA YANGA


Klabu ya Yanga leo imemtangaza aliyewahi kuwa kocha wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kuwa Katibu Mkuu wake.
Boniface Mkwasa, Katibu mkuu Yanga Sc
Mkwasa anajaza nafasi iliyokuwa wazi kwa muda mrefu huku ikikaimiwa na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Jonas Tiboroha
Baada ya klabu ya Yanga kumtangaza Mkwasa kushika nafasi hiyo, mwenyewe amefunguka na kusema kuwa hana nia yoyote ya kurudi kwenye kiti kama kocha wa klabu hiyo kwani anadai anaamini walimu wote waliopo kwenye benchi la ufundi.
Mkwasa aliweka wazi msimamo huo mapema baada ya baadhi ya watu kuhisi huenda labda amekuja Yanga kuongeza nguvu katika benchi la ufundi 
"Nimekuja Yanga SC kufanya muunganiko kati ya waalimu na Sekretarieti na pia sina nia yeyote ya kurudi kwenye kiti cha kufundisha kwenye klabu ya Yanga SC kwani sina shaka yeyote juu ya walimu waliopo kwenye benchi la ufundi" alisema Boniface Mkwasa Katibu mkuu Yanga SC

BILIONI 13.9 KUJENGA NYUMBA ZA WAALIMU


indexNa: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi bilioni 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 wa shule za msingi  nchini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Juliana Daniel Shonza juu ya mpango wa kuboresha miundombinu ya elimu vijijini kama vile nyumba za walimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya walimu.
“ Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi Bil. 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 11.14 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 661 kwa shule za sekondari,” alifafanua Jafo.
Aliendelea kwa kusema kuwa, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMESII) imekamilisha ujenzi wa nyumba 146 kati ya nyumba 183 ambazo kila nyumba wataishi walimu Sita (6 multi-unit houses).
Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa nyumba  hizo umegharimu shilingi bilioni 21.9 ambapo nyumba 37 zinaendelea kujengwa kwa gharama  ya shilingi bilioni 5.5 na zinategemea kukamilika tarehe 30 Aprili, 2017.
Kuhusu ulipaji wa madeni ya walimu, Jafo amesema kuwa Serikali imeendelea kulipa madeni kadri yanavyojitokeza na kuhakikiwa ambapo katika mwezi  Oktoba, 2015 Serikali ililipa madeni ya shilingi bilioni 20.12 kwa walimu 44,700 na shilingi bilioni 1.107 zililipwa mwezi February, 2016 kwa walimu 3221.

DKT. MWAKYEMBE AZINDUA RASMI OFISI ZA WIZARA YAKE MKOANI DODOMA:

dz1
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua rasmi Makao Makuu ya Wizara yaliyopo katika jengo la Masomo ya Biashara na Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako Wizara imehamia rasmi makao maku ya Serikali mkoani Dodoma
dz2
Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
dz3
Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
dz4
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
dz5
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe katika picha ya pamoja na watumishi na wageni wake mara baada ya kuzindua rasmi  ofisi za wizara mjini Dodoma ambako wizara imehamia rasmi mkoani Dodoma
dz6
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe aksalimiana na viongozi mbalimbali kabla ya  kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
dz7
……………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Ofisi za wizara yake mkoani Dodoma na kuwataka Watumishi wa wizara waliohamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.
Dkt Mwakyembe amezindua rasmi makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria yaliopo mkoani Dodoma katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya wizara hiyo na watumishi wake 31 kuhamia rasmi makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.
Baada ya uzinduzi huo Mhe. Mwakyembe alisema kitendo cha kuhamia mkoani DODOMA ni utekelezaji wa agizo la kuhamia makao makuu ya Serikali ambalo lilitolewa mwezi Julai mwaka 2016 na hivyo watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kama walivyokuwa Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanda ya Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof Kikula na watumishi 31 wa wizara ambao wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo la Serikali.
Awamu ya Kwanza yenye watumishi 31 wa wizara wakiongozwa na Waziri Dkt Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju imehamia rasmi mkoani Dodoma. Awamu ya pili na ya tatu zitafuata utaratibu ambao umewekwa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.
Kufuatia kuhama rasmi kwa ofisi za wizara sasa mawasiliano yote yatafanywa kupitia anuani ya Katibu Mkuu Sanduku la Posta 315 Dodoma, namba ya simu ni 026 2321680, nukushi ni 026 2321679 na baru pepe ni ile ile ya km@sheria.go.tz

AZAM FC YAJINOA DHIDI YA NDANDA FC , YAZUNGUMZIA HALI ZA MAJERUHI WA MECHI YA SIMBABAADA ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za kiafya za baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.

Wachezaji wa Azam FC waliokuwa majeruhi ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’, Stephan Kingue waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, ambao matajiri hao walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.

Wengine wanaouguza majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.

“Bocco hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada ya wiki moja,” alisema.

Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuendelea na mikikimikiki ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.

RC SHIGELLA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA,AVITAKA KUONGEZA UZALISHAJI


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Mjini Tanga cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na mmoja kati ya wamiliki wa kiwanda cha kuzalisha chuma cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kulia ni Mhasibu wa kiwanda hicho,Sikander Husein Omari na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akimsikiliza kwa umakini Mhasibu wa kiwanda cha chuma cha (Uniqeu Steel Meel),Sikander Hussein Omari  wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akionyeshwa namna chuma zinavyozalishwa kwenye kiwanda cha Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akitazama namna chuma zinazozalishwa kwenye kiwanda cha chuma cha Uniqeu Steel Meel) wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  akitazama namna chuma akiwa amepanda kwenye chuma hizo kuona ubora wake  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akimuonyesha kitu mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili(Habari Tanga RahaBlog.

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 

Na Richard Mwaikenda
MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
 Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah

 Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
 Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
 Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
 Sasa ni wakati wa msosi
 Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
 Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga