Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2016

MKESHA WA MWAKA MPYA NDANI YA UWANJA WA SAMORA IRINGA ,KARIBU MWAKA 2017 -LIVEHOTUBA YA MWENYEKITI

ð Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kassim M. Majaliwa,

ð Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina J. Masenza,

ð Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa,

ð Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Richard Kasesela,

ð Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Mji wa Iringa,


ð Waheshimiwa. Maaskofu, Wachungaji na Viongozi wawakilishi wa makanisa, madhehebu na dini mbalimbali,

ð Waheshimiwa. Wabunge mbalimbali wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

ð Waheshimiwa wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali,

ð Viongozi mbalimbali wanaowakilisha vyombo mbalimbali vya serikali,

ð Waheshimiwa. Wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa,

ð Wawakilishi kutoka katika Halmashauri mbalimbali,

ð Wawakilishi kutoka katika Makampuni mbalimbali,

ð Marafiki wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali waliopo hapa, na wanaotusikia na kutuona katika vyombo vya habari mbalimbali duniani,

ð Wageni waalikwa,

ð Watanzania wenzetu,

ð Mabibi na mabwana.
ð Itifaki yote imezingatiwa
Ndugu Mgeni Rasmi, Ni Jambo la furaha sana tunapokutana usiku wa leo mahali hapa ili kulipeleka Taifa letu mbele za Mungu kwa dua na maombi. Kwetu imekua ni kujitoa na utii endelevu kwa maono haya ambayo Mungu alitupa takriban mwaka wa 19 leo.

Maono na mzigo ndani ya mioyo yetu ni kuutumia usiku wa kila Tarehe 31 Desemba kila mwaka katika uwepo wake kuliombea Taifa letu la Tanzania, na imekuwa shauku ya wengi kuwa Mungu pekee ndiye tumaini la ukombozi wa Taifa letu.

Ndugu Mgeni Rasmi, dhumuni kubwa la mkesha wa mwaka huu – “Mkesha Mkubwa®Kitaifa -Dua Maalum,” kwanza, ni kutoa shukrani zetu kwa Mungu kwa ajili ya kutuvusha salama wakati wa Uchaguzi Mkuu ambapo kulikuwa na viashiria dhahiri vya uvunjifu wa Amani yetu, pia kulikuwa na uwezekano wa kuvurugika kwa Umoja na Mshikamano wetu Kitaifa. Ni Dhahiri kwamba Mungu ametujibu dua na maombi yetu tuliyoomba katika mkesha maalum wa kuombea Uchaguzi uliopita uliofanyika katika viwanja hivi hivi. Leo hii tunashuhudia Watanzania wakiwa na Amani, Umoja na Mshikamano licha ya hiyo hali iliyokuwa ikitarajiwa kutokea.

Pili, ni kukuombea wewe Mhe; Waziri Mkuu ikiwa ni pamoja na kuitikia mwito wa Raisi wetu Mpendwa Daktari John Pombe Magufuli  wa mara kwa mara kwa Watanzania Kwamba tuombee Nchi yetu, kwa Mungu ikiwa ndiyo tegemeo la pekee la kuilinda Nchi yetu, kukuongoza,  kukuwezesha na kukupa hekima na busara katika kuliongoza Taifa hili,kwa kuwa wewe ndiye mtendaji Mkuu wa shughuli zote za Serikali ili tufikie malengo ya maendeleo na ustawi wa watu wote.
Pia kuiombea Serikali yako kwa Mungu ili iweze kwenda na kasi  katika utendaji sambamba na kauli mbiu  ya, “Hapa kazi tu” katika kuwaletea Wananchi maendeleo.

Tatu, ni kufanya dua kwa Taifa letu ili  liendelee kuwa na Amani na Utulivu kama andiko kutoka katika Bibilia Takatifu kitabu cha 1 Timotheo 2:1-2 linasema [nanukuu]:

1Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
(mwisho wa kunukuu).
Kama Watu wote tujuavyo Taifa bila Amani na Utulivu hakuna shughuli yeyote ya maendeleo inayoweza kufanyika,Aidha Tunamwomba Mungu alinusuru Taifa Letu kwa kuzingatia kwamba Taifa limekumbwa na mikasa mimgi na mikubwa iliyogusa hata Viongozi wetu Serikali,Hata kuyumba kwa mwelekeo mzima wa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla Tunaamini kwamba jawabu halisi ni kumwomba Mungu aingilie kati kwani kwake Yeye HAKUNA LISILOWEZEKANA.

Hata hivyo Taifa letu limeanza kuona mabadiliko chanya katika juhudi zako za kupambana na umaskini, rushwa, magonjwa, matendo maovu, kugawanyika kwa familia, uonevu dhidi ya watoto, uchawi na kazi nyingine za Kishirikina.

Ndugu Mgeni Rasmi, tunapenda kukuhakikishia kuwa hatutakuacha peke yako katika mapambano hayo. Sisi viongozi wa kiroho tuko bega kwa bega na wewe katika upande wa dua na maombi hadi Tanzania yetu mpya itakapokuwa mahali pema pa-kuishi. 

Ndugu Mgeni Rasmi, tunaamini kwamba ni wajibu wa kila raia mwema wa Tanzania, bila kujali kwamba wewe ni mwanaume au mwanamke, mtoto, kijana au mzee, kuomba na kuleta badiliko chanya katika Taifa letu.

Ni maombi yetu kwa Mungu kwamba Haki itumike katika kutafuta mustakabali wa Taifa letu, Mungu ameibariki Nchi yetu kwa kila kitu hapa nataja baadhi tu Rasilimali Watu, Bahari, Mito mikubwa Maziwa Ardhi yenye rutuba Mbuga za wanyama Maliasili, Madini, Gesi, Mafuta.

Hivyo tunawasihi Watanzania wote, walio ndani na nje, marafiki na wote wenye nia njema popote walipo duniani, kuungana nasi usiku huu tunapolia pamoja kwa SAUTI MOJA kwa Mungu Mkuu ili aiponye TANZANIA.

Tunaendelea kuamini kwamba Jawabu la Mahitaji ya Watanzania Wote litatoka kwa MUNGU kama alivyo Ahidi katika Neno lake Takatifu Kitabu cha
 2Nyakati 7:14(Nanukuu)
Ikiwa Watu Wangu, Walioitwa kwa Jina Langu,Watajinyenyekesha, na Kuomba ,na kunitafuta uso,na kuziacha njia zao mbaya;basi,nitasikia toka mbinguni na kuwasmehe dhambi yao,na kuiponya Nchi yao.
(Mwisho wa kunukuu)

Hivyo, Ndugu Mgeni Rasmi, ni jambo la hekima na busara kuiacha siku hii ya Disemba 31 kuwa ni siku maalum kwa Watanzania kukusanyika pamoja na kufanya Dua kwa Taifa letu.

Ndugu Mgeni Rasmi, tunapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa jumuiya zote za makanisa, dini na madhehebu mengine, na mtu mmoja mmoja ambao wamesimama nasi kwa miaka yote kuchangia na kuisimamisha kazi hii. Na kwa wale ambao ndio wamejiunga nasi kwa mara ya kwanza, tunawakaribisha kwa moyo mkunjufu na tunawaahidi kwamba kwa pamoja tutalijenga Taifa letu

Zaburi 20:3, [nanukuu]: “Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako”. [Mwisho wa kunukuu]

Mwisho tunapenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa moyo wako wa upendo na ushirikiano wako kwa Watanzania wote kwa kuitikia wito wetu wa kuja kuomba Mungu pamoja nasi usiku huu tunasema Mungu akuzidishie heri na baraka tele wewe pamoja na familia yako.


MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA WATU WAKE!

LIVE WAUMINI IRINGA WASUBIRI MWAKA 2017 UWANJA WA SAMORA MGENI RASIMI WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA

Mkesha  wa mwaka 2016  kukaribisha mwaka 2017  uwanja  wa Samora   Iringa usiku  huu
wakuu  wa  wilaya  ya  Iringa  ,Kilolo  na  Mufindi  wakiwa  katika  mkesha
RC  Iringa  kushoto  akiwa  katika mkesha  kumwakilisha waziri  mkuu

IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA KANISA LA KKKT USHARIKA WA IRINGA MJINI USIKU HUU

Mwimbaji  wa  kwaya  ya  vijana  kanisa  la  kiinjili la  kilutheri Tanzania  (KKKT)  usharika  wa  Iringa  mjini  Jemida  Kulanga  akifurahi  na mtoto  wake  baada ya  kubatizwa  usiku  huu  wakati  wa  mkesha wa  mwaka  mpya  2016
Askofu mteule  wa  dayosisi  ya  Iringa  mchungaji  Gavile  akifanya  ibada ya  ubatizo
Askofu  Dkt  Mdegela na mkewe  wakipokea maelekezo nje ya kanisa  muda  wa  kuelekea katika mkesha uwanja  wa  samora
Twasubiri  kuaga  mwaka 2016
Jeshi la  polisi  laweka  ulinzi  nyumba  za  ibada
Waumini  wakiwa na furaha ya  kuaga  mwaka  2016
Ibada  ya  Kipaimara  kwa muumini mmoja