November 9, 2016

WAZIRI NAPE APOKEA VIFAA VYA MICHEZA TOKA KAMPUNI YA STAR TIMES LTDImage result for waziri Nape 
                                    Waziri  Nape

Na Anitha Jonas – WHUSM

Timu za Mpira wa Miguu za watoto wa Mikoani pamoja na Timu za Mpira wa Miguu kwa Wanawake zilizoko katika mashindano ya ligi kuu zinatarajiwa kupatiwa msaada wa Mipira na Jezi hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akipokea msaada wa mipira 100 na jezi 100 kutoka kwa Kampuni ya Startimes Ltd kwa ajili ya kusaidia timu zenye uhaba wa vifaa vya michezo nchini katika mikoa yote.

“Wizara inaendelea kuthamini michezo toka ngazi ya chini na sasa inaendelea kufanya mazungumzo na uongozi wa Startimes nchini kusaidia kuzungumza na wadau wa michezo nchini China kuja kuwekeza hapa katika sekta ya michezo pamoja na kutusaidia upatikanaji wa vifaa vya michezo kwa urahisi zaidi kwani vingi hupatikana kwa gharama kubwa”, amesema Mhe. Nnauye.

Pamoja na hayo Waziri Nnauye alitoa ombi kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia kujenga vituo vya kulea vipaji vya michezo nchini kwa watoto kama ilivyo kwa kituo cha JK Park kilichopo Jijini Dar es Salaam kwani kwa kupitia vituo hivyo kutasaidia kuibua vipaji mbalimbali vya Michezo na kuinua sekta ya michezo kwa Taifa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Startimes Tanzania  Bw. Leo Liofang amesema kuwa kampuni yao itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Wizara katika kuendeleza sekta ya michezo nchini na misaada ya vifaa vya michezo itakuwa endelevu kwa lengo la kuhakikisha michezo inaboreshwa.

Hata hivyo Waziri Nnauye aliupongeza uongozi wa TFF kwa kusimamia Ligi Kuu ya Wanawake mbali na kwamba kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vifaa na kuwaahidi kuwasaidia kufanya jitihada za kutafuta wadhamini.

Halikadhalika aliendelea kusema kuwa serikali ingependa kuona ligi hiyo inakuwa endelevu kama ilivyo kwa ligi mbalimbali za michezo nchini.

                               ******************MWISHO ******************

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE