November 8, 2016

VIFO VYA AJALI ZA BARABARANI VYAPUNGUA IRINGA , MADEREVA WAVEMBE WAPIGWA FAINI ZAIDI YA TSH BILIONI MOJA .............

WAKATI idadi  ya  vifo  vya ajali  za barabarani mkoani Iringa  imepunguka  kutoka  vifo 172  mwaka 2015 hadi kufikia  vifo 97 mwaka  2016 huku  majeruhi  wamepunguka kutoka 141 hadi  kufikia majeruhi  56 mwaka 2016   kikosi  hicho  cha  usalama barabarani  mkoa wa Iringa kimefanikiwa kukusanya   kiasi cha  fedha kutokana na  faini mwaka  huu mara dufu  zaidi  kutoka  Tsh 835,800,000 hadi  kufikia Tsh 1,218,960,000 kukiwa na ongezeko la  Tsh  383,116,000 sawa na asilimia 31.


Tathimini  hiyo  iliyofanywa na  kamata  ya  usalama  barabarani  mkoa wa  Iringa  ilitolewa juzi na katibu wa kamati   hiyo ya  usalama barabarani mkoa  wa Iringa (RTO) Leopold Fungu mbele ya mkuu wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza  kwenye maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa  usalama yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya  stendi kuu ya mkoa .

Mfungo  alisema  kuwa tathimini  hiyo ya mwaka  huu 2016 imeishia mwezi  Septemba  30  ukilinganisha na tathimini kama   hiyo  iliyofanyika mwaka jana 2015 kwa  kipindi cha Januari mosi hadi Septemba 30  inaonyesha  kuwepo  kwa  upungufu mkubwa wa ajali  na vifo katika mkoa  wa Iringa na kuwa mwaka jana mkoa  ulikuwa na idadi ya ajali  106 wakati  mwaka  huu ni ajali 93 pungufu ni ajali 13  sawa na asilimia 12

Wakati  ajali  zilizosababisha  vifo kwa  mwaka 2015  zilikuwa ni ajali 82 huku mwaka huu  2016  ni ajali 77 kukiwa na  upungufu  wa ajali 5  sawa na asilimia 6  huku ajali za majeruhi  zilikuwa 24 mwaka  jana na mwaka huu ni ajali 16 kukiwa na  upungufu wa ajali 8 sawa na asilimia 33 ya  ajali  zote  zilizotokea mwaka jana .

Katika  ajali   hizo  watu  waliojeruhiwa  ni 141  kwa mwaka  jana 2015 kati yao  wanaume ni 107 na  wanawake ni 34 na mwaka  huu   majeruhi ni 56 wakiwemo  wanawake 9 na wanaume 47   huku  waliopoteza maisha  kwa  mwaka jana   wanaume 114 na  wanawake 58 na kufanya  jumla kufikia  watu 172  ila idadi hiyo kwa mwaka huu  imepungua kutoka wanawake 8 na  wanaume 89 na  kufanya  jumla yote kufikia 97.

Hata   hivyo  alisema  ajali za pikipiki maarufu kama  boda  boda  pia zimeweza  kupungua kutoka ajali 41 mwaka jana  2015 hadi kufikia ajali 35 mwaka huu kukiwa na upungufu wa ajali 6 kati ya ajali  hizo mwaka jana  ajali  za vifo zilikuwa 34 zilizopelekea  vifo vya  watu 36 na majeruhi 8 wakati  mwaka huu ajali hizo 35 zimepelekea  vifo 34 na majeruhi 10 kuwa  kwa ajali za pikipiki vifo  vimepungua  asilimia 12 .


Huku makosa ya kawaida ya usalama  barabarani mwaka 2015 yalikuwa ni 27,787 na  mwaka huu kikosi cha usalama barabarani  kimefanikiwa  kuongeza  nguvu na  kuwa na makosa  40,632  ikiwa ni  ongezeko la makosa  12,845 sawa na asilimia 32  kutokana na makosa  haya  kiasi cha  fedha kilichokusanywa  kwa faini mwaka  huu kimeongezeka kutoka  Tsh 835,800,000 hadi  kufikia Tsh 1,218,960,000 kukiwa na ongezeko la  Tsh  383,116,000 sawa na asilimia 31.

Alisema mafanikio  ya  kuthibiti  ajali za barabarani mkoani  Iringa yamepatikana kutokana na ushirikiano  mzuri uliopo kati ya  jeshi la  polisi  kikosi cha usalama barabarani , Sumatra , Tanroads , Bima na TRA ambao kwa  pamoja  wamekuwa  wakifanya kazi kama  timu .

Pia  alisema oparesheni  mbali mbali zinaendelea katika mkoa wa Iringa ikiwa ni pamoja na  kutumia askari  wasiovaa sare  kupima mwendo kasi kwenye  barabara  mbali mbali  japo  alisema baadhi ya ajali ni kutokana na ubovu wa miundo mbinu na uzembe kwa madereva kama kuendesha vyombo  hivyo  huku  wakiwa  wamelewa .

MWISHO0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE