November 7, 2016

Trump: Wasomali wanaeneza itikadi kali Marekani

Mgombea wa urasi nchini Marekani Donald Trump asema jamii ya Wasomali nchini Marekani inaenneza itikadi kali

Mgombea wa urasi nchini Marekani Donald Trump asema jamii ya Wasomali nchini Marekani inaenneza itikadi kali 
 
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameishambulia jamii ya Wasomali wanaoishi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani ,akiwalaumu kwa kueneza maoni yenye itikadi kali nchini humo.

Alitumia mfano wa kisa cha shambulio la kisu lililotekelezwa na mhamiaji raia wa Somalia mnamo mwezi Septemba katika mji wa St.Cloud ,akisema kuwa wakaazi wa Minnesota wameteseka vya kutosha.

Bwana Trump ambaye alikuwa katika ziara ya kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumanne amesema kuwa iwapo atakuwa rais atahakikisha kuwa wakaazi wa maeneo wanashauriwa kabla ya wakimbizi kupelekwa ili kuishi.
Hivi ndivyo alivyosema Trump:
"Viongozi wetu wana ujinga kiasi gani? Wana Ujinga kiasi gani kuruhusu mambo kama haya kutokea? Hapa Minnesota mumekabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na ukaguzi mbovu wa wakimbizi, huku idadi kubwa ya Wasomali wakiingia katika jimbo hili bila wakaazi kufahamishwa,bila usaidizi wenu ama hata ruhusa.

Huku wengine wakijiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State na kueneza maono yao ya itikadi kali katika kila pembe ya nchi pamoja na dunia nzima kwa jumla.

Kwa kweli ni vigumu kuamini na kila mtu anasoma kuhusu mikasa inayotokea Minnesota...Mumeona kisa cha shambulio la kisu katika eneo la St Cloud.

Serikali ya Trump haitasajili wakimbizi bila usaidizi wa jamii ya eno hili.Hilo ndilo wanaweza kuwafanyia kwa sababu mumeteseka vya kutosha."

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Jumanne 8 Novemba, 2016.

1 comments:

Mbele said...

Mimi nimeishi katika jimbo hili la Minnesota tango mwaka 1991. Kwa ujumla, ingawa wako watu wanaomshabikia Donald Trump, walio wengi, pamoja na viongozi, wamekuwa na msimamo wa kuwakaribisha wa-Somali. Minnesota ni jimbo linaloongoza capa Marekani kwh kuwa na wa-Somali wengi. Donald Trump amefika hapa na kusema aliyoyasema, lakini alichoshindwa ni kufahamu hisia za walio wengi katika jimbo hili, ambalo lina historia ya miaka mingi ya kukiunga mkono chama cha Democratic. Ninahisi amegonga mwamba.

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE