November 16, 2016

MASHINDANO YA SPANEST CUP YATINGA ROBO FAINALI KWA TIMU NANE KUFUZU

Mratibu wa  mashindano ya SPANEST Cup 2016  Godwell Olle Meing’ataki (kulia)  akiwakabidhi  vifaa vya  michezo  Kiongozi wa  timu ya  Itunundu Fc Eliopa Maurosi  na afisa mtendaji wa kijiji  cha Itunundu  Halima Kunzugala  wakati wa  zoezi la kugawa vifaa kwa  timu nane kati ya 22  zilizofuzu hatua ya  robo fainali ya  ligi hiyo  ya Spanest maalum kwa vita dhidi ya ujangili katika  hifadhi ya Taifa ya  Ruaha
MASHINDANO ya  kupiga  vita  ujangili  wa  wanyama pori katika   hifadhi ya  Ruaha  mkoani Iringa  yajulikanayo kwa  jina la  Spanest Cup yaingia  hatua  ya  robo fainali kwa  timu  nane  kati ya  22 kufuzu kucheza hatua   hiyo  inayoanza leo.

Akikabidhi  vifaa kwa  timu   hizo jana mratibu wa  mashindano hayo  Godwell Olle Meing’ataki alisema lengo la ligi hiyo yenye kauli mbiu “Piga Vita Ujangili Piga Mpira Okoa Tembo” ni kuwaunganisha vijana katika upigaji vita  ujangili wa wanyamapori wakiwemo Tembo na  kuwa  mwisho  wa ligi hiyo itatolewa  takwimu ya simu zilizopigwa kufichua ujangili .


Alisema kuwa toka  kuanza kwa lingi  hiyo  wananchi  wamekuwa  wakipewa  elimu ya namna ya  kuwafichua  watu  wanaojihusisha na vitendo  vya ujangili na  kuwa  hadi  sasa  mbali ya  kuwepo kwa changamoto mbali mbali  ikiwemo ya  baadhi ya  timu kuonyesha nidham mbaya  wakati wa mechi  ila vijana wameonyesha  kiwango kikubwa uwanjani.

Hivyo  alizitaka  timu  mbali  mbali ikiwemo  timu ya  Lipuli Fc kutuma viongozi wake  katika mashindano hayo  ili  kutafuta  wachezaji kwani  vipaji vilivyoibuliwa  kutokana na ligi  hiyo ya  Spanest  ni vya hali ya  juu na upo uwezekano mkubwa wa vijana hao  kuchezea  timu kubwa kama Simba na Yanga .


Alizitaja  timu  zilizofanikiwa  kuingia hatua ya robo fainali na pointi  zake katika mabano    kwa  tarafa ya  Idodi  kuwa ni Kitisi (12), Nyamahana(6) , makifu (5)na mapogoro(12)  wakati  tarafa ya Pawaga ni  Luganga (14), Itunundu (12),Kinyika(16) na Mbugani (10).


Mratibu  huyo  alisema  kwa  ajili ya  kukimbizana na muda wa   vijana  hao  kuingia katika  shughuli za  kilimo wamelazimika  kupanga ratiba fupi zaidi kwa  hatua ya robo faina  hadi fainali  ili kumaliza  ligi hiyo mapema na vijana kuingia mashambani .

Hivyo  alisema  robo fainali ya  kwanza  itakuwa na  timu  za Nyamahana  itacheza na  timu ya Kitisi  kwenye uwanja wa Nyamahana    huku Makifu na Mapogolo zitacheza   uwanja wa Makifu Novemba 17 mwaka huu  ,  Luganga na Kinyika  zitacheza katika uwanja wa Luganga  na Itunundu  na Mbugani  zitacheza uwanja wa Itunundu  Novemba 18 mwaka huu .

Meing’ataki alisema    katika  robo faina ya  pili ya ligi   hiyo ya Spanest Cup 2016  Novemba 19  timu ya  Kitisi itacheza  na Nyamahana  katika  uwanja wa Kitisi  na Mapogolo  itacheza na  Makifu  kwenye  uwanja wa Kinyika   wakati Novemba 20 itakuwa ni hitimisho ya robo fainali ya  pili kwa   timu ya  Kinyika  kucheza na Luganga kwenye uwanja wa Kinyika na  Mbugani na Itunundu  zitacheza  uwanja wa Mbugani  na  kuwa  mechi  zote  zitaanza kwa  wakati na  kila timu  kuhakikisha  saa 9 ;00 Alasiri inakuwepo uwanjani ikiwa  imevaa sare kabisa .


Mratibu    huyo  alisema  kuwa hatua ya  nusu fainali  itachezwa  Novemba 22 na fainali  itachezwa  Novemba 26  mwaka huu iwapo ratiba   hiyo haitavurugika  na fainali hiyo itachezwa tarafa ya Idodi .

Mshindi wa kwanza atapata kikombe, medali ya dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh 300,000, kutembelea Hifadhi ya Ruaha.

Mshindi wa pili atapata medali ya fedha, mipira 2, cheti na Sh 200,000 taslim huku mshindi wa Tatu akipata medali ya shaba, cheti na Sh 100,00 huku mshindi wa nne atazawadiwa  Sh 50,000

1 comments:

台達徵信社 said...

良心和熱情是台達徵信社所有同仁的動力來源,完美解決客戶的每一項任務是我們唯一的目標。

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE