November 9, 2016

MANISPAA YA IRINGA YAFUNGA OFISI ZA POSTA NA MAKAMPUNI BINAFSI KWA KUKWEPA KODI

Mgambo  wa  Manispaa ya  Iringa  akifunga ofisi  za Posta  Iringa  katika  oparesheni  inayoendelea na  kufunga ofisi  za  wadaiwa  sugu wa  kodi


Ofisi  za  EMS zilizopo  jengo la  Posta Iringa  zikiwa zimefungwa  na Manispaa ya  Iringa kwa  kushindwa  kulipa kodi 
Mkurugenzi  wa Manispaa ya  Iringa Dr  Wiliam Mafwere  akizungumza na mtandao  huu wa matukiodaima Blog 

 HALMASHAURI ya  Manispaa ya  Iringa  imeanza  zoezi la  kufunga  ofisi  za taasisi za umma  ikiwemo ofisi ya  Posta Iringa  kwa  kushindwa  kulipa kodi ya service level kwa wakati .

 Mkurugenzi  wa Manispaa ya  Iringa Dr  Wiliam Mafwere ameueleza mtandao huu wa matukiodaimaBlog  kuwa  zoezi  hilo linaendelea na  kuwa  jumla ya  kampuni  na mashirika 36   zinadaiwa na baadhi  vimefungiwa   likiwemo  shirika la  Posta na kuwa  zoezi  hilo linaendelea kwa  wote  ambao  wamepewa  barua  za kutakiwa  kulipa .

Alisema  kuwa baadhi ya  kampuni ikiwemo TTCL Iringa wamekwisha  lipa baada ya kufungiwa na tayari  wamefunguliwa  pia zipo taasisi nyingine za  serikali ambazo  zimefungiwa na  kulipa deni lake  pamoja na ofisi hizo za umma   pia zipo  super Market na  vituo vya mafuta ambavyo  vimefungiwa .

Mkurugenzi huyo  alisema  baada ya  kukamilisha   wadaiwa  sugu hao 36  zoezi  litaendelea kwa  wadai wa kodi za mabango ambao bado hawajalipia kodi.

1 comments:

Anonymous said...

hivi,niulize: hawa manispaa wa iringa sio wateja wa shirika la posta iringa? kama ndiyo, je, hakuna njia nyinginezo za kistaarabu za kuwadai hao Posta kwa mtindo wa kutumia huduma zao bila ya kulipa taslimu lakini wakikatwa malipo hayo kupitia akaunti yao manispaa watakayo ifungua Posta kwa madhumi hayo? nazungumzia hapa malipo ya huduma kwa huduma, mpaka hapo biashara ya Posta itakapo tengemaa, kuliko kudhalilishana kiasi hicho? Fikiria, ni wateja wangapi wa Posta watakao athirika kwa kukosa huduma zao, tukifahamu fika kwamba shirika la Posta hapa nchini ni moja tu? somtimes busara tu zinasaidia sana. Mawazo yetu yasiwe pesa tu, kuna njia nyingi za kulipana, please, for god sake !

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE