November 4, 2016

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KUFANYIKA KESHO MKOANI IRINGA

watu  wenye  ulemavu  wakishiriki maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Iringa
Mwenyekiti  wa kamati ya  usalama barabarani  mkoa wa Iringa Salim Abri akizungumza  wakati wa maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa  usalama barabarani mwaka jana
Maandamano ya  wiki ya nenda kwa usalama barabarani

 WAKATI  kesho wadau  wa  usafiri  mkoa wa Iringa  wanataraji  kushiriki  katika maadhimisho  ya  wiki ya nenda kwa  usalama  iliyopangwa  kufanyika katika  viwanja  vya stendi kuu ya mabasi yaendayo  mikoani ,watu  wenye  ulemavu mjini hapa   wamefurahishwa na utendaji kazi wa  usalama barabarani ambao  wamekuwa  wakiwasaidia  kuwavusha hasa maeneo yenye alama  za kuwapisha  watembea kwa  miguu.

Wakizungumza na mtandao huu wa matukiodaimaBlog baaadhi ya  walemavu hao  wamesema  kuwa  kazi nzuri  inayofanywa na askari wa kikosi  cha usalama barabarani katika  kusimamia  usalama barabarani  wao  imekuwa  ikiwapa faraja  zaidi kwani matukio ya  walemavu  kugongwa na vyombo  vya moto yanazidi kupungua  siku hadi siku.

Kwani  walisema  kama  zipo  changamoto kwao  katika  kuheshimiwa barabarani  basi ni chache  tofauti na  zamani ambapo matukio ya walemavu kugongwa  yalionekana  kushika kasi.
 
Zaina  Juma alisema  kuwa  bado  wanaomba  elimu  zaidi  kuendelea  kutolewa kwa madereva na  ikiwezekana madereva   wazembe  kuendelea  kufutiwa leseni  zao na kuwa  hatari kubwa  kwa  walemavu kugongwa kwa  sasa  ipo kwa baadhi  ya madereva  boda boda  ambao si makini barabarani.

 Hivyo  alisema inapendeza  kesho  madereva  boda  boda na madereva  wengine pamoja na wananchi  kujitokeza  kwa  wingi katika maadhimisho hayo  ili  kuweza  kupata  elimu ya usalama barabarani.

Kwa  mujibu  wa ratiba  ya maadhimisho  hayo mkoani  Iringa yanataraji  kufanyika katika  eneo la  Stendi  kuu ya mabasi ya mikoani kuanzi mida ya  saa 2 asubuhi na kabla ya  hapo maadhimisho hayo  yatatanguliwa na maandamano 

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE