November 19, 2016

KOMBE LA SPANEST TIMU YA MAPOGOLO NA KITISI ZAFUZU KUCHEZA NUSU FAINALITimu ya Kijiji cha KITISI na MAPOGOLO Zimefanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali kwa Tarafa ya IDODI baada ya matokeo ya Michezo ya leo

KITISI wakiwa Nyumbani Wameweza kushinda Magoli 3 kwa 1 na hivyo kufuzu wakiwa wamejikusanyia Point zote 6 baada ya kushinda michezp yote miwili ikumbukwe mchezo wa awali wakiwa ugenini walishinda Goli 1 kwa 0

Na kwa upande wa mchezo wa MAPOGOLO dhidi ya MAKIFU mchezo umemalazika kwa sare ya Bila kufungana 0-0 na hivyo Timu ya Mapogolo inafuzu kwa faida ya goli la ugenini iliyopata katika mchezo wao wa awali uliomalizika kwa kufungana goli 2-2

Yafuatayo ni matokeo kamili ya michezo ya leo
MATOKEO

19 Nov 2016
TARAFA YA IDODI

RATIBA YA ROBO FAINALI YA PILI (MECHI ZA MARUDIANO)

 TARAFA YA IDODI


KITISI Vs NYAMAHANA
3-1

Wafungaji wa Magoli Kitisi

Batony Mgilu dk 12
Batony Mgilu  dk 25
Dani Abdalah dk 39

Mfungaji wa Nyamahana
Joram Issa Dk 76 kwa Penati.

MAPOGOLO vs MAKIFU
0-0

Na kwa matokeo haya sasa Timu ya MAPOGOLO na KITISI watakutana katika mchezo wakumpata Bingwa wa Tarafa  ya IDODI ambae atashinda  atakutana na bingwa wa tarafa ya PAWAGA Katika kumpata  Bingwa wa SPANEST CUP 2016.

RATIBA YA KESHO MZUNGUKO WA ROBO FAINALI YA PILI

TARAFA YA PAWAGA
20 Nov 2016
KiNYIKA vs LUGANGA
MBUGANI vs ITUNUNDU

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE