November 17, 2016

KIJIJI KINACHOONGOZA KWA UJANGILI KUANIKWA WAKATI WA FAINALI YA SPANEST CUP

                                                      Na MatukiodaimaBlog 
 
FAINALI ya kombe la mashindano   ya soka yenye lengo la  kupambana na vitendo  vya  ujangili  katika  Hifadhi ya  Ruaha  mkoani Iringa yaliyoandaliwa na mradi Kuboresha Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST)  kuweka  wazi takwimu za timu ambazo  zinaongoza kwa ujangili .

Mratibu wa mashindano hayo  Godwell Ole Meing’ataki aliyasema  hayo  wakati  akizungumza na waandishi  wa habari kuhusiana na lengo  la kuanzishwa kwa mashindano hayo  .


Alisema  kuwa   toka  kuanza kwa mashindano hayo zimetolewa namba maalum kwa ajili ya  wananchi  kupiga  simu na  kutoa taarifa za ujangili katika hifadhi ya Ruaha na taarifa   hizo  zimekuwa  zikirekodiwa na siku ya fainali zitatolewa mbele ya  mkuu wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  ambae ni mwenyekiti wa kamati ya  ulinzi na usalma mkoa 


Mratibu  huyo  alisema kumekuwepo na utaratibu  wa  kutoa   elimu ya  kupambana na ujangili  ambayo  imekuwa  ikitolewa kabla ya  kuanza  michezo hiyo na wakati wa  mapumziko kwa  wananchi  wanaofika  kushuhudia mashindano hayo  na  kuwa kupitia mashindano hayo elimu kwa  vijiji vyote 24 vinavyoshiriki mashindano hayo vimepata.


Meing’ataki alisema  timu zote zinazoshiriki mashindano hayo  zinatoka vijiji  vinavyozunguka  hifadhi ya  Ruaha  na  kuwa  iwapo timu moja  wapo kati ya  nane  zilizofuzu  hatua ya  robo  fainali  itafanikiwa  kuchukua  kombe itakuwa ni balozi mwema wa  kupambana na ujangili katika kijiji  husika na  kama kijiji  chao  kinaongoza  kwa ujangili  pia umma utaelezwa .

Meing’ataki alisema zawadi kwa mshindi wa kwanza atakayepata kombe, medali, seti moja ya jezi, cheti na kutembelea hifadhi ya Ruaha imeongezeka kutoka Sh 300,000 hadi Sh Milioni moja.
Kwa upande wa mshindi wa pili atakayepata medali, cheti na mipira miwili imeongezeka kutoka Sh 200,000 hadi Sh 700,000 na ya mshindi wa tatu anayepata cheti na medali imeongezeka kutoka Sh 100,000 hadi Sh 500,000 na  kuwa  lengo si  kutoa  zawadi  hizo  lengo ni  kutoa  elimu zaidi ya  kulinda hifadhi ya  Ruaha .

Hata   hivyo  aliomba  wananchi kuendelea  kufichua majangili kwa  kupiga namba 0800751212 bure  na  kuwa  iwapo mmoja kati ya  wachezaji ataonekana  kujihusisha na  ujangili hatua kali  zitachukuliwa  dhidi  yake kwani kauli mbiu ya mashindano hayo PIGA MPIRA OKOA TEMBO ni kauli mbiu yenye lengo la  kulinda wanyamapori wetu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE