November 4, 2016

IRUWASA WAANZA KUFUNGA MITA ZA MAJI ZA LUKU IRINGADisplaying LUKU MAJI.jpg
MAMLAKA maji  safi na maji taka  mjini Iringa (IRUWASA) imeanza kuwafungia wateja  wake  mita za  kisasa  za  kulipia kabla ya huduma  mita za  Luku kwa  ajili ya  kuboresha  huduma  hiyo na  kuepuka usubufu usio wa  lazima.

 Hadi   sasa  jumla ya mita  286 zimekwisha fungwa kwa wateja wake na  zoezi hilo  linaendelea  ili kuwafikia wateja wote kuingizwa katika mita  za LUKU.

Afisa huduma kwa wateja ambaye amekaimu nafasi ya Afisa  Mahusiano wa IRUWASA Shabani Ally   akizungumza na Matukio Daima amesema kua Mita hizo zinautofauti mkubwa sana na zile za zamani kwani mita zile hata ifike mwezi hazikati maji mpaka wakukatie wao wenyewe lakini hizi za luku zinajikata zenyewe kulingana na jinsi ulivyolipia na zinaepusha usumbufu wa kufatilia kwa wananchi nani ambaye hajalipa na nani amelipa.

“Mita hizi ambazo tumewafungia wananchi, wafanyabiashara pamoja na sekta binafsi bado hatujaingiza katika mfumo wa ulipiaji wa kutumia miamala ya simu lakini wateja wanatakiwa kufika ofisini ili waweze kulipa na tunawapatia token ambayo watakwenda kujaza huko majumbani mwao na kupata huduma hiyo ya maji”. Alisema  Ally.

Aidha  Ally aliwawataka wananchi ambao wanaendelea kutumia mita za zamani kulipia katika mitandao yao ya simu ili kuepusha usumbufu na kukaa katika foleni kungoja kulipia katika ofisi za IRUWASA. 


Lakini pia pia Bwana Shabani amewaomba wananchi kuendelea kuwafichua watu ambao wanaendelea kujiunganishia maji kinyemelela na kua atakae fichua atapewa zawadi ya shilingi laki mbili.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE