Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2016

KITISI FC MABINGWA SPANEST CUP 2016

Timu ya Kitisi Fc ndio mabingwa wa kombe La spanest 2016 baada ya kuifungwa kwa penati timu ya Kinyika FC leo  katika michezo wa fainali

TANZIA :RPC SINGIDA PETER KAKAMBA AFARIKI DUNIA

Habari za kusikitisha ambazo mtandao huuwa matukiodaima blog umezipata ni kuwa aliyekuwa
kamanda wa polisi mkoa wa Singida ( RPC)  Peter Kakamba amefariki dunia Usiku wa kuamkia leo  jumatano

Kakamba ambae alihamishiwa mkoani Singida akitokea mkoa wa Iringa alilazwa hospitali ya Taifa ya jijini Dar es Salaam

Mtandao huu wamatukiodaimablog umepatakuthibitisha taarifa hizi kwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi

Taarifa zaidi tutazidi kuwajuza

TRUMP AMPA CHEO ALIYEMPINGA RAIS OBAMA

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tom Price kuwa waziri wa Afya katika serikali yake.

Bw Price, 62,amekuwa katika Bunge la Congress akiwakilisha jimbo la Georgia na ni mtaalam wa upasuaji wa mifupa ambaye amekuwa akiongoza kamati ya bajeti katika Bunge la Wawakilishi.

Atatekeleza jukumu muhimu katika mipango ya chama cha Republican wa kubatilisha mpango wa bima ya afya ulioanzishwa na Rais Obama, ambao hufahamika sana kama Obamacare.

Wakati wa kampeni Bw Trump aliapa kwamba ataibatilisha sheria hiyo ambayo imekuwa ikitazamwa kama moja ya mambo makuu aliyoyafanya Bw Obama wakati wa utawala wake.

Lakini amesema kwamba kuna baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ambavyo atavihifadhi.

NDEGE YAANGUKA YAUA WACHEZAJI KATI YA ABIRIA 76 KATI YA 81

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 81, wakiwemo wachezaji na maafisa wa moja ya klabu kubwa za soka nchini Brazil, imeanguka ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuua watu 76.
Polisi wamesema watu watano walinusurika lakini watu wengine wote waliangamia.
Ndege hiyo ya kukodishwa ilikuwa safarini kutoka Brazil ikipitia Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji na maafisa wa timu ya Chapecoense.

Klabu hiyo ilikuwa imepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya mji wa Medellin.

Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo, la pili kwa umuhimu Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano lakini sasa imesitishwa.
Timu hiyo inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kulaza San Lorenzo ya Argentina.
Mechi hiyo ilikuwa inatazamwa kama kubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ndogo.
Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol) limesema kwamba limesitisha shughuli zake zote kwa sasa.
Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.
Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema: "Tunamuomba Mungu awe na wachezaji, maafisa, wanahabari na wageni wengine watu ambao walikuwa wameandamana na ujumbe wetu."
Wamesema hawatatoa taarifa nyingine hadi ibainike kiwango kamili cha mkasa huo.
Taarifa zinasema watu wawili kutoka kwa timu hiyo - Alan Ruschel na Danilo - huenda wamenusurika.
Telemundo Deportes wameandika kwenye Twitter kwamba Ruschel ameathiriwa na mshtuko lakini ana fahamu na anazungumza. Aidha, ameomba aruhusiwe kukaa na pete yake ya harusi na awaombe jamaa zake.
Ndege hiyo ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya saa sita usiku saa za huko (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege, marubani walisema ndege hiyo ilikuwa imepata matatizo katika mfumo wake wa umeme.
Meya wa mji ulio karibu wa La Ceja amethibitisha kwamba mchezaji mmoja wa miaka 25 ni miongoni mwa manusura.
Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura.
Hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.
Hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura.

November 29, 2016

HOTEL ZA KITALII UWAPO IRINGA NI IRINGA SUNSET HOTEL NA RUAHA HILTOP LODGE UWAPO HIFADHI YA RUAHA IRINGA ,SAFIRI HIFADHINI NA INTERCONTINENTAL TOURS & SAFARI

Wakurugenzi wa  Hotel ya kitalii ya  Ruaha Hiltop Lodge iliyopo  hifadhi ya  Ruaha  Iringa ambao  wanapatikana kwa simu  0784726709 au katika Tovuti yao ya  www.ruahahiltop.com
Hotel ya Sunset Ipo  mjini Iringa eneo la Gangilonga  jirani na MSD  ni hotel ya  kisasa ya  kitalii  huduma  zao ni bora  kuliko sehemu nyingine na kila mwisho wa  wiki  kuna usiku wa kuchoma nyama  wasiliana nao kwa simu namba 0754 669854/0787469854 Email ;iringasunset@gmail.com
Kwa usafiri  wa  uhakika  katika  hifadhi  zote za  kusini  ni 0766 040 058  / 026 270 2622  ofisi  tupo jengo la Imucu au benk ya  posta katikati  ya mji  wa Iringa room namba 15 emailinfo@intercontinetaltour.com
Aina  ya  vyumba vilivyopo ni Single 45,000,Double 65,000 Family 85,000

KILELE CHA MAONYESHO YA UTALII TANZANIA MKOANI IRINGA ,CHUO KIKUU HURUA CHA TANZANIA WAHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA CHUO HICHO

Watendaji   wakuu wa  chuo  kikuu Huria  cha Tanzania  tawi la  Iringa  wakiwa katika banda la chuo  hicho  wakati wa maonyesho ya utalii Tanzania  viwanja  vya  Kichangani Iringa  leo  ,kutoka  kushoto  ni mhadhiri mwandamizi wa  chuo  hicho Dr Bukaza Chachage , Mhadhiri  na mwanafunzi wa udaktari  Nasra Habibu , Majaliwa  afisa masoko wa  chuo , Mustapher Kiswanywa  ambae  pia mhadhiri   ,Ridhiwani  na Winfrida  Sanga Mkutubi wa  chuo  hicho 
Banda  la Chem & Cotex  Iringa 

NANI BINGWA SPANEST CUP 2016 NI KINYIKA FC NA KITISI FC

 Image result for Mashindano ya  Spanest
KESHO  ni kesho ni  Kinyika Fc ama Kitisi Fc  kujinyakulia kombe la ubingwa  la   mashindano  wa  soko ya Spanest 2016 yenye  lengo la  kupiga vita vitendo vya ujangili katika  hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa    kombe litakaloambatana na pesa tasilimi Tsh milioni moja na ziara ya  kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha bingwa kujulikana  .
 
Mratibu  wa Mashindano hayo  Godwell ole  Meing’ataki   alisema  kuwa mchezo  wa fainali unachezwa  kesho  jumatano katika  uwanja wa Kimande Pawaga na  mgeni rasmi atakuwa mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela .
 
Zawadi  kwa  washindi  mbali ya mshindi wa kwanza mshindi wa  pili atapewa  medali, cheti na mipira miwili  na pesa Sh 700,000 , mshindi wa tatu atapewa TSh 500,000 .
 
Pia  alisema kabla ya mchezo wa fainali  utakaozikutanisha   timu za  Kinyika Fc  ya  tarafa ya pawaga na Kitisi Fc ya tarafa ya  Idodi  ili  kupata  bingwa na mshindi wa  pili wa kombe  hilo kwa mwaka 2016 huku Mapogolo Fc ya tarafa ya  Idodi itacheza na Itunundu Fc  kupata  mshindi  wa tatu na  wa nne .
 
Hata   hivyo  alisema kumekuwepo na utaratibu  wa  kutoa   elimu ya  kupambana na ujangili  ambayo  imekuwa  ikitolewa kabla ya  kuanza  michezo hiyo na wakati wa  mapumziko kwa  wananchi  wanaofika  kushuhudia mashindano hayo  na  kuwa kupitia mashindano hayo elimu kwa  vijiji vyote 24 vinavyoshiriki mashindano hayo vimepata na  kuwa  elimu  hiyo na leo itatolewa na itaendelezwa na timu  zote .
 
Pia alitaka   wananchi kuendelea  kufichua majangili kwa  kupiga namba 0800751212 bure  na  kuwa  iwapo mmoja kati ya  wachezaji ataonekana  kujihusisha na  ujangili hatua kali  zitachukuliwa  dhidi  yake kwani kauli mbiu ya mashindano hayo PIGA MPIRA OKOA TEMBO ni kauli mbiu yenye lengo la  kulinda wanyamapori wetu  na  kuwa  zaidi ya watu 2000  wamekuwa  wakishiriki  viwanja mbali mbali kila mchezo unapochezwa  kushuhudia na kupewa  elimu ya  vita dhidi ya ujangili

November 28, 2016

*MKAPA AONYA:* MAAGIZO, AMRI ZA VIONGOZI ZITAUA ELIMU.

Wakati Serikali ikiendelea na mkakati wa kubadilisha mfumo wa elimu, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amesema maagizo na amri za viongozi zinazotolewa bila ya kuwa na majadiliano, zitaitumbukiza shimoni elimu ya Tanzania.

Mbali na hilo, Mkapa, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, amesema idadi ya wanachuo wanaodahiliwa vyuo vikuu nchini, ni lazima iendane na ubora wa miundombinu pamoja na bajeti ya Serikali badala ya kujaza wanafunzi wakati hakuna fedha za kutosha na hivyo kuwa mzigo.

Mkapa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya saba ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambako alikuwa mgeni rasmi.

Mkuu huyo wa Udom alisema maagizo peke yake, hayaondoi matatizo ambayo yamejitokeza katika siku za hivi karibuni.

Alisema njia bora ya kuboresha elimu nchini ni kwa wadau kukutana katika meza ya mazungumzo ili wajadili changamoto zinazowakabili na kueleza nini kinatakiwa.
“Amini nawaambia, maagizo peke yake hayaondoi matatizo tuliyonayo ndani ya elimu, bali niwaombe wadau pamoja na wizara husika kuwa wakae meza ya mazungumzo ili wazijadili changamoto hizo,” alisema Mkapa.

Alisema kama maagizo yataendelea bila ya kuwepo na majadiliano elimu ya Tanzania itakuwa imewekwa rehani na kwamba katika kipindi cha miaka michache nchi haitakuwa kwenye ubora wa elimu kama ambavyo wengi wanadhania.

Alisema hayo wakati kukiwa na malalamiko ya wanafunzi yanayotokana na kuondolewa kwenye orodha ya wanaotakiwa kupata mikopo, huku wanafunzi waliokuwa wakisoma kozi maalumu ya ualimu wa sayansi wakiondolewa na vyuo binafsi vya elimu ya juu vikilalamikia kutopangiwa wanafunzi.

Pia serikali ilitangaza kubadilisha upangaji wa madaraja ya matokeo ya elimu ya sekondari kutoka mfumo wa kupanga kwa kutumia GPA na kurudisha mfumo wa divisheni.

Kwa kawaida mgeni rasmi kwenye mahafali ya vyuo vya elimu ya juu huwa hahutubii, lakini Udoma ilimuomba aseme machache baada ya kutunuku wahitimu.
“Katika machache mliyotaka niseme ni pamoja na kuwataka Serikali waache kutegemea wawekezaji, maana vyuo vyenyewe vimewekezwa. Bado nasisitiza kuwa wafanye mikutano ya pamoja na waitane kwa haraka wazungumze bila ya kutegeana,” alisema.
Awali mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Gaudensia Kabaka alimweleza Mkapa kuwa Udom inakabiliwa na kazi kubwa mbili ambazo ni kutopelekewa fedha kutoka Bodi ya Mikopo pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi waliotoka Chuo Kikuu cha St Joseph ambao wamefanya chuo kipate shida ya namna bora ya kuwasaidia kwani masomo waliyokuwa wanasoma hayaeleweki.

Mwezi Februari, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ilifuta hati ya usajili ya kampasi mbili za Chuo Kikuu cha St Joseph za Sayansi ya Kilimo na Teknolojia na Chuo cha Tehama na kusema wanafunzi 2,046 waliokuwa wakichukua shahada na stashahada wangehamishiwa vyuo vingine.

Kuhusu changamoto ya fedha, Mkapa alisema Bodi ya Mikopo imewakwamisha kwa kiasi kikubwa kutokana na kutopeleka Sh6.5 bilioni ambazo ni ada ya wanafunzi katika mwaka wa masomo 2015/16.

Mwenyekiti huyo alisema deni hilo limeharibu taswira nzima ya Udom na kuwafanya wadau washindwe kuwaamini katika utoaji wa huduma mbalimbali, kama kushindwa kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba za watumishi.

Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alisema kulikuwa na jumla ya wahitimu 4,839 wa kuanzia ngazi ya astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili, na shahada ya uzamivu.

*Chanzo* : www.mwananchi.co.tz

MABADA YA PIPI IVORI IRINGA NA ASAS DAIRIES LTD YAWAVUTIA WENYE MAONYESHO YA UTALII KITAIFA IRINGA

Mfanyakazi  wa kampuni ya  Ivori Iringa  watengenezaji  wa  bidhaa  tofauti tofauti  zikiwemo  pipi ,Cocoa ,Ivori Tomato .n.k akipanga bidhaa   katika maonyesho ya  utalii Kitaifa  Iringa  kumbuka  bidhaa  za Ivori Iringa  zinapatikana  nchi  nzima ni  bidhaa bora zaidi
Wananchi  Iringa  wakitembelea  banda la  Asas Dairies  Ltd  Iringa  kupata  bidhaa mbali mbali  katika maonyesho ya  utalii kitaifa  Iringa  kumbuka bidhaa  za Asas Dairies  Ltd ni  bidhaa bora  ambazo zimechukua  tuzo ya  ubora  kwa  zaidi ya miaka mitatu  sasa  nchini Tanzania  furahia bidhaa bora  za Asas Dairies Ltd 

MAONYESHO YA UTALII KITAIFA IRINGA , JIVUNIE BIDHAA ZA IRINGA FOODS& LOGISTICS LTD

Wananchi  mjini  Iringa  wakitembelea banda la Iringa  Foods & Logistic Ltd watengenezaji wa pipi aina mbali mbali  pamoja na Snacks zenye  ubora  zaidi  jivunie bidhaa bora kutoka  Iringa  tembelea  maonyesho ya  utalii Tanzania katika  viwanja vya Kichangani mjini Iringa
Bidhaa mbali mbali  zinazotengenezwa na Iringa Foods Logistics Ltd bidhaa  zetu zinapatikana  nchi  nzima   wasilia nasi  kwa  simu namba 026 2725265 /0655 84 87 17
Chuo  Kikuu  Iringa  walivyoshiriki vema maonyesho ya  Utalii Tanzania
Chuo  Kikuu Huria  Cha  Tanzania  tawi la Iringa   wakitoa maelekezo  mbali mbali katika banda  lao  lililopo  viwanja vya maonyesho ya Utalii Tanzania kichangani mjini Iringa

November 27, 2016

VIJANA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Hebron Mwakagenda akitoa mafunzo kuhusu katiba ya zamani pamoja na katiba mpya kwa vijana kutoka wilaya zote za jiji la Dar es Salaam leo. (Picha na Geofrey Adroph)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa  wilaya zote za jiji la Dar Es Salaam.
Katibu Mtendaji wa TYVA, Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo na madhumuni ya mjadala wa katiba na vijana uliyofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar Es Salaam
Mbunge wa Viti Maalumu, (CUF), Riziki Lulida akizungumzia changamoto wanazozipata kama wabunge wenye ulemavi katika katiba pamoja na kutoa maoni kuhusu uundwaji wa katiba mpya
Mbunge wa Viti maalum Pemba-Zanzibar, Mheshimiwa Zainabu Mussa Bakari akizungumzia Haki na Wajibu wa mwananchi Kikatiba wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililowashirikisha vijana mbalimbali kutoka wilaya tano za jiji la Dar es Salaam ili kujadili katiba mpya lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es salaam Salma Mwasa (CUF) akizungumza na vijana kuhusu balaza la vijana katika katiba inayopendekezwa ili kuweza kuleta utatuzi wa matatizo tyao ili serikali iwasikie wakati wa kongamano lililowakutanisha vijana kutoka katika wilaya mbalimbali za jiji la Dar.
Baadhi ya vijana wakichangia mada
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika leo ambao wameazimia kuendelea kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.