October 6, 2016

YAMOTO BEND KUPAGAWISHA WAKAZI WA IRINGA MJINI KESHO IJUMAA OCTOBA 7 UKUMBI WA V.I.P KWA BUKU 10 TU


WAKAZI  wa  mji  wa  Iringa  ijumaa ya  kesho  wanatarajia  kuiona kwa  shangwe  ya  aina  yake  baada ya  wasanii  wa bend ya Yamoto  kujipanga  kutoa burudani ya  kufa  mto  katika  ukumbi wa club V.I.P uliopo mjini hapa .

Wasanii hao ambao  wanatamba na  vibao  vyao kadha wa kadha   wanategemea  kutua mjini  Iringa  kutokea  mikoa ya nyanda za  juu kusini  ambao  wamekuwa na ziara  ya  burudani kwa  wakazi  na  wapenzi wa muzik  huo wa dansi  hapa  nchini .

 Burudani  hiyo  inaletwa mjini Iringa kwa udhamini mkubwa wa Radio  Nuru Fm pamoja na Club V.I.P inatarajiwa  kuanza  kupagawisha  wana  Iringa  kuanzia majira ya saa moja  usiku na  kuna  kila dalila  ya nyomi kubwa  kufulika katika  ukumbi  huo kutokana na hamu  kubwa ya  wana Iringa  kutaka  kupokea  burudani toka kwa Yamoto.

Hata  hivyo  wengi wao  wanadai  kiingilio  cha Tsh 10,000 ambacho  kimewekwa kwa ajili ya  kupata  burudani hiyo  bado ni  kidogo  ukilinganisha na umaarufu wa wasanii hao  wa Yamoto  Bend.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE